Waheshimiwa wabunge ambao ni wagonjwa kwa muda mrefu sana wajiuzulu!

President Elect

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
693
212
Kuna baadhi ya wabunge hawajahudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu sana, wengine tangu waapishwe kuwa wabunge, kutokana na maradhi ya muda mrefu. Kwa heshima kubwa na kwa kujali afya zao, na pia kutoa fursa kwa watu wengine kutumikia wananchi katika majimbo yao, ni jambo la kiungwana kama watajiuzulu ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Naomba kuunga mkono hoja.
 
1.Celina Kombani-Ulanga magharibi
2.Cyril Chami-Moshi vijijini
3.Mark Mwandosya-Rungwe
4.LIVINGSTONE LUSINDE-ugonjwa wa akili
 
Muda mrefu sana ni miaka/miezi/wiki ngapi?
Policy ya bunge kuhusu kusimamishwa kazi kutokana na ugonjwa inasemaje?
 
Muda mrefu sana ni miaka/miezi/wiki ngapi?
Policy ya bunge kuhusu kusimamishwa kazi kutokana na ugonjwa inasemaje?

Nadhani hapa swala sio muda na Policy ya Bunge Pekee, lakini issue ni uzalendo kwa wananchi wao na mapenzi kwao wenyewe na Familia zao.

Ifikie wakati tuwe waungwana wakweli, Wabunge kama Mwandosya, Mwakyembe na huyo Chami tunategemea kuona busara na tunaweza kutumia maamuzi yao ya kuachia ngazi kama kipimo cha imani yao kwamba wanauwezo ama nia ya kweli ya kuwaletea wananchi wao mabadiriko kwa kutuonyesha mfano wa mapenzi yao kwao wenyewe na afya zao.

Hawa watu kutokana na maradhi yanayowasumbua ni wazi kwamba, kwanza sio haki kwa nafsi zao wenyewe kuendelea na mikeke mikeke ya kisiasa ambayo inaweza ikaingilia mtiririko mzuri wa uhamarikaji wa afya zao kitu ambacho ni usumbufu mkubwa kwao binafsi na kwa familia zao, lakini pia, uwezo wao wa kuwatumikia wananchi umepungua kwa kiwango kikubwa sana ukizingatia umuhimu wa nafasi wanazoshikiria kwenye jamii zao na Taifa Kwa ujumla.

Nakubaliana asilimia mia na mzambia kwamba hawa ndugu wanastahili kupumzika kwa manufaa yao binafsi na familia zao lakini pia kwa manufaa ya wapiga kura wao na Taifa kwa Ujumla.

Itoshe tu kusema kwamba wananchi ambako wenzetu hawa ni wabunge wanastahili kupata huduma bora za kuwakilishwa bungeni na maswala mengine ya kimaendeleo kwa ufanisi zaidi kama majimbo mengine na kwamba wajibu wa maendeleo ya wananchi ni yetu wote sio wabunge peke yao,watoe nafasi kwa wananchi wengine kuendeleza japo apo walipofikia.
 
Muda mrefu sana ni miaka/miezi/wiki ngapi?
Policy ya bunge kuhusu kusimamishwa kazi kutokana na ugonjwa inasemaje?

kumbe nawe huwa unaingia humu kwenye hard disussions kama unasolve hesabu za circle and sphere? Maana mada za huku ni sawa na unagonga kitu cha hesabu tena pure maths, tofauti na kule mmu&chit chats kule ni kama unasolve kiswahili na history..karibu mwanamalundi.
 
Kuna njia nyingi za kushiriki katika vikao;waweza kuwa nje ya vikao ukaweza kuwasilisha mawazo yako kupitia maandishi.
 
Viongozi wetu (pamoja na baadhi ya watumishi wa umma) hakuna mahali kazi yao inapimwa.Lakini kama tutatumia mahudhurio yao ofisini kuwakilisha huduma yao kwa umma basi tutakuwa sawa kuwataka waachie ofisi. Maana yake hapa ni kwamba kama utendji kazi wa viongozi wetu ungekuwa unapimwa objectively, wasingeendelea kushikilia nafasi wakati wakijua hawaperform chochote (si kwa wagonjwa tu, hata kwa wazima).
 
kama bado ni mawaziri na aliyewateua anaona bado wanafaa kuongoza wizara wakiwa vitandani. itakuwa vigumu kwao kuwa na uzalendo wa kuachia ngazi za ubunge kwa vile mkuu bado anawahitaji
 
Kuna baadhi ya wabunge hawajahudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu sana, wengine tangu waapishwe kuwa wabunge, kutokana na maradhi ya muda mrefu. Kwa heshima kubwa na kwa kujali afya zao, na pia kutoa fursa kwa watu wengine kutumikia wananchi katika majimbo yao, ni jambo la kiungwana kama watajiuzulu ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Naomba kuunga mkono hoja.
Marehemu Sumari aliugua kabla ya uchaguzi. Ajabu, amelipwa posho ya mafuta ya gari hadi mauti ilipomkuta. Hayo mafuta alikuwa anasafiria kwenda wapi? Wanatuibia sana hawa.
 
Kuna baadhi ya wabunge hawajahudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu sana, wengine tangu waapishwe kuwa wabunge, kutokana na maradhi ya muda mrefu. Kwa heshima kubwa na kwa kujali afya zao, na pia kutoa fursa kwa watu wengine kutumikia wananchi katika majimbo yao, ni jambo la kiungwana kama watajiuzulu ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Naomba kuunga mkono hoja.

Wanachukuwa poshooo?
 
1.Celina Kombani-Ulanga magharibi
2.Cyril Chami-Moshi vijijini
3.Mark Mwandosya-Rungwe
4.LIVINGSTONE LUSINDE-ugonjwa wa akili

Blue afya yake imeimarika kwa sasa na atakuwa mjengoni soon.
Red atakuwa anahudhuria kliniki pale mirembe so hatoweza kufika bungeni kwa sasa
 
Ifike mahali maslahi ya Taifa yawekwe mbele, haiwezekani mtu kama Mwandosya ambayea ameugua kwa karibu mwaka sasa kuendelea kushikilia nafasi ya uwaziri.

Rais anapaswa kuliona hili kwa kuwa pamoja na kuathiri nafasi yake ya uwaziri kwa sababu za kiafya lakini pia anaathiri utendaji wa wizara yake na serikali kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom