Waheshimiwa, siri ya sisi kuwa masikini hii hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waheshimiwa, siri ya sisi kuwa masikini hii hapa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by vukani, Jan 2, 2012.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  JE HIVI UNAJUA:

  Kwamba tofauti kati ya nchi masikini na nchi tajiri haitokani na umri ambao nchi inayo. Na hilo tunaweza kulitambua kwa kuangalia nchi kama India na Misri.

  Kwamba zina zaidi ya miaka 2000 tangu kuwepo kwake hapa duniani lakini bado ni nchi masikini.

  Kwa upande mwingine nchi kama Canada, Australia na New Zealand ambazo miaka 150 iliyopita zilikuwa ni nchi masikini na zisizohesabiwa kama nchi zenye uchumi imara, lakini leo hii ni nchi zenye maendeleo makubwa na tajiri sana.

  Tofauti ya nchi tajiri na masikini haitokani na nchi kuwa na maliasili na rasilimali za kutosha.

  Nchi kama Japan, ni visiwa vidogo ambavyo karibu asilimia 80 vimezungukwa na milima na haina ardhi ya kutosha kwa kilimo na ufugaji, lakini ni nchi yenye uchumi imara sana.

  Ni nchi ambayo inaagiza malighafi kutoka nje na kuzalisha bidhaa mbalimbali na kuziuza karibu ulimwenguni kote.

  Mfano mwingine ni nchi kama Switzerland ambayo hailimi zao la Cocoa, lakini ni nchi ambayo inazalisha bidhaa ya chocolate yenye ubora hapa duniani. Ni nchi ambayo inalo eneo dogo kufaa kwa ufugaji lakini wameweza kuwa wazalishaji wazuri wa mazao ya mifugo yenye ubora wa hali ya juu kama vile Jibini.

  Tukisema Rangi, Kabila au Dini kuwa ndio kipimo cha tofauti ya nchi tajiri na msikini ni kujidanganya bure.

  Wale wahamiaji kutoka nchi masikini ambao katika nchi zao walikozaliwa walionekana kuwa wavivu kupindukia ndio wazalishaji wakubwa katika nchi hizo tajiri.

  Je tofauti yake ni nini hasa?

  Tofauti ni mtazamo wa watu katika nchi hizo masikini, ambapo unachagizwa na elimu na utamaduni usio na tija ambao umekuwepo kwa miaka mingi

  Kwa kuangalia tabia na mienendo ya watu wa nchi zenye maendeleo na tajiri utagundua kwamba asilimia kubwa ya watu hao inafuata kanuni zifuatazo katika maisha yao.

  Kanuni hizo ni hizi zifuatazo:

  · Maadili
  · Uadilifu
  · Kuwa na dhima au wajibu
  · Kuheshimu sheria na taratibu
  · Kuheshimiana na hasa kuheshimu uhuru wa mtu mwingine
  · Kupenda kazi
  · Kujinyima na kuweka akiba na hatimaye kuwekeza katika biashara.
  · Kujituma
  · Kwenda na muda

  Ni watu wachache sana katika nchi masikini wanaofuata kanuni hizo katika maisha yao.

  Sisi sio masikini kwa sababu eti tuna uhaba wa maliasili au mazingira yaliyotuzunguka ni magumu.

  Sisi ni masikini kwa sababu tuna tatizo la mtazamo na namna ya kufikiri.

  Kama unaitakia mema nchi yako, basi sambaza huu ujumbe kwa watu wengi nchini kwako ili waujue ukweli huu:

  Makala hii nimeitafsiri kutoka katika mtandao.

  Nakiri kuwa tafsiri ni yangu kama kutakuwa na mapungufu naomba mnivumilie.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Okay,uloyaweka hapa yana mantiki
   
 3. Karhumanzira

  Karhumanzira Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa mara ya kwanza jk kataja sababu ya kwanini sisi masikni kuna kipindi flan nyuma aliulizwa akasema hajui

  Sababu aliyoitaja ni kwamba hatuna wawekezaji
   
 4. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  good research.
   
Loading...