Waheshimiwa sana mwigulu nchemba na godbless lema njooni mfanyiwe maombi.

12STONE

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,109
1,475
Kwa makini sana nimefuatilia Nyendo za wanasiasa hawa wawili kwa muda mrefu na kugundua tofauti zao ziko dhahiri.

Ukifuata kanuni za Kibiblia yamkini vijana hawa sasa wanatumika bila wao kujua nafasi walizosimama ni za muhimu namna gani ama ni mbovu na hatarishi kwa usalama wa Taifa kwa kiasi gani.

VIJANA HAWA WAMEGEUKA KUWA MALANGO MAKUU MAWILI HAPA NCHINI MWETU.
A.MWIGULU NCHEMBA:-
Amegeuka na anatumika kwenye nafasi ya Lango la Mauti huku hajitambui,Endapo ni kweli kila mabaya yanayotokea mf.Lwakatare kuhusishwa na Ugaidi,Mabomu ya Soweto-Arusha,Kutekwa na kuteswa kwa Absolom Kibanda na Vurungu zilizotokea kwenye mikutano ya Chadema Tarafa ya Ndago Jimboni kwake Mh. Mwigulu. Tumeyasikia yamesemwa sana huku Mh.Mwigulu akihusishwa ndiye anayeratibu mambo hayo.

Ikiwa ndivyo ilivyo Kwa jinsi hii ili kuepusha Nchi yetu Tanzania Isiingie kwenye machafuko na kumwaga damu ni vema kijana huyu ajitambue mapema -achukue Tahadhari asitumike kama LANGO LA MAUTI.
NA DAWA NI HII MWIGULU NJOO UFANYIWE MAOMBI ILI UGEUKE KUWA BARAKA KWA TAIFA LAKO BADALA YA KULETA LAANA.

B.GODBLESS LEMA:- Kijana huyu mwanasiasa machachari mwenye ujasiri usio na kifani,kapata wapi moyo wakujihatarisha maisha yake kwa ajili ya maslahi ya Taifa letu.

Kwa vyovyote vile Mungu ndiye muasisi wa Ujasiri na ndio maana anasema Mwenye Haki ni Jasiri kama Simba.Lema anajitambua katika kusimamia haki za wananchi wote lakini pia huenda hajui anatumika kama LANGO LA UZIMA,BARAKA NA UFANISI KWA TAIFA.

Siku zote Mungu akitaka kuleta mabadiliko ya kweli yawe ya kiroho,kiuchumi,kielimu,kiafya ama kijiografia kwanza anatafuta mtu sio watu. Mungu anahuluka yakuanza na Mtu mmoja tu kisha atajizalisha na kupata watu wengi.

Mh.Lema Mbunge wa Arusha Mjini wewe ni vema ukajitambua Mungu anakutumia kama chachu nzuri ya mabadilijko hapa Nchini,Angalia usije akadhania ni kwa nguvu zako,Epuka kiburi na majivuno,tafuta mambo ya Unyenyekevu na unyoofu maana hutakufa kamwe mpaka utakapo maliza kazi uliyoitiwa na Mola wako.

Watu wanaweza kukuchafua kadri wanavyoweza lakini uwe na busara na Hekima maana utatumika KAMA LANGO LA MABADILIKO YA MAENDELEO KWA TAIFA LETU.
Sio kwa nguvu zako tu kuna Mkono Mwema wa Mungu uko juu yako.

Tambue na ubakie kwenye siri hii yakukimbilia kwa Mungu,NJOO UFANYIWE MAOMBI ILI UFIKIE LENGO ULILOITIWA.

Angalieni nimewaonya mapema 2015 sio mbali wakati wa uchaguzi mkuu Mjihadhari kila mtu kwa nafasi yake MSIJE MKALIINGIZA TAIFA HILI KWENYE UMWAGAJI WA DAMU.
Kuombewa haulazimishwi ni hiari lakini muhimu sana, WAHESHIMIWA G.LEMA NA M.NCHEMBA NJOONI MFANYIWE MAOMBI.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom