Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,569
Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri manayofanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Taifa hili la Tanzania. Pongezi binafsi ziende kwa Mh. Dr Magufuli kwa kusimamia vema ubora wa miradi ya barabara (Value for Money). Msukumo wangu wa kuwaandikia ni kuhusiana na mradi wa barabara ya Kibosho road kwenda Umbwe; nakupongeza sana Mh. Dr Cyril Chami kwa kuweza kufanya kile walichoshindwa watangulizi wako kama kina Ngawaiya, Lyatonga Mrema, Ngatolaoni na wengineo. Katika kipindi cha ubunge wako utakuwa umeacha historia ambayo itadumu miaka mingi ijayo ya kuweka barabara hiyo lami.
Jumanne ya tarehe 16/10/2012 nikiwa katika shughuli za jamii (msiba) nilibahatika kupita hiyo barabara ya Kibosho road - Umbwe na kujionea kazi inayoendelea ya kushindilia vifusi. Nilipofika maeneo ya Kindi nilishangaa kukuta lami lakini kilichonishangaza zaidi ni ubora wa hiyo lami. Nadhani ile itakuwa ni rangi ya lami inayopakwa kwenye barabara na siyo "tarmac road" inayotengenezwa. Mh. Dr. Magufuli hausiki lakini nafahamu wakaguzi wa hiyo miradi (Tanroads) wanasimamiwa na Wizara yake. Ni kichekesho barabara ya lami na tayari kuna na viraka. Mh. Dr Cyril Chami tafadhali wachukue wataalamu wa barabara toka Tanroads ukakague na kujionea hiyo kazi inayofanyika...ni kiini macho hakuna ubora utakaopatikana kwa mtindo huo wa kuweka lami kama unapaka rangi piusi Mallya Mary Chuwa

Last edited by a moderator: