Wahesh; Wabunge WANAWAKE tatizo ni Ninyi, WAUME zenu ama UKWASI wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahesh; Wabunge WANAWAKE tatizo ni Ninyi, WAUME zenu ama UKWASI wenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Feb 15, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina maana ya kumdhalilisha mtu yeyote na kama ikitokea kumuudhi mtu awaye yeyote natanguliza radhi, ila hili limenigusa leo wakati nasikiliza BBC japo lilianza muda mrefu ila limeonekana kuwa sugu Nchini Kenya na hili si lingine bali unyanyaswaji unaofanywa na wanawake kwa waume zao ama kuwapiga au kuwatendea yale ambayo hawastahili kutendewa. Watu wengi wamechangi kuwa wanawake wa Kenya wanafanya hivyo kutokana na uwezo wao kiuchumi ambao ni mkubwa kuliko waume zao.

  Sasa hili limenifanya nami nirudi hapa nyumbani yawezekana hata hapa kwetu haya yanatendeka ila naamini ndugu zangu huku watakuwa wanayaficha kwa kutumia ile ya "lugha usione milango na madirisha ila ndani mna mambo." Pamoja na kuwa wapo ambao hatuwezi kuwafahamu kwa urahisi ila kuna wale ambao tunaweza kuwazungumzia kutokana na maisha waishio nami nimeguswa sana na Wabunge wetu WAMAMA ambao wamo ndani ya BUNGE LA JMT.

  Binafsi nimekuwa nikifuatilia sana Mikutano ya Bunge pamoja na Vikao vyake takribani kila mwaka kuna ule wakati wa utambulisho mara nyingi sana takriban Mikutano yote utakuta ni rahisi sana kwa Spika kutambulisha MKE wa Mhe Mbunge kuliko MUME wa Mhe. Mbunge sasa nashindwa kujua ni kwamba Wamama hawana waume au lah!! Mbaya zaidi unaweza sikia Mume wa Mhe flani kafariki wakati huo unakuta mama yuko magharibi na baba yuko mashariki hivyo naye mama ama anasikia kupitia vyombo vya habari au rafiki zake wa karibu.

  Kuna wengine utasikia wako na waume tena wengine ni wahadhiri waandamizi ila utasikia mama anaishi Mkoa huu na baba anaishi Mkoa ule na wanaweza kukutana tu pale ambapo kuna labda Msiba ama Sherehe katika familia yao. Yani kuna namna flani ambayo kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa whats going on; worse enough kuna vijana wanawake nao wameingia Bungeni juzi juzi ndugu zangu mmewaona walivyo na matamko ya baadhi yao mmeyasikia ama juu ya kuolewa kwao au kutoolewa kwao. Sasa tatizo ni lipi ni UKWASI walio nao hawa watu au waume zao ndo problem manake mi nahisi kama vile nao wanateswa ila wanakula jiwe.

  Ni shida..................................... wanaharakati angalieni namna ya kuisadia hii jinsia ya Adamu bana isiwe mkuki kwa nguruwe.....
   
 2. f

  frontline1 Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hoja yako ni nzuri sana inapaswa kujadiliwa kwa hekima, wengine tumesikia wameamua kuwa wasagaji etc ni tetesi tu kutoka kwenye majukwaa wakati wa kampeni
   
 3. f

  faloyce2001 Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi hawawezi kwenda bungeni na waume zao kwa kuwa wengi wao wameingia bungeni kwa kutumia rushwa ya ngono sasa wanaogopa kugonganisha magari huko dodoma
   
 4. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haya ya chumbani mwa watu haya kuhusu, je hawa wabunge wanajadili au wanatekeleza kile walichotumwa na wananchi hilo ndio la kujadili...................
   
 5. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Wengi wao huwa tunasikia wakipata Ubunge tu wanakamata visungura au serengei boys,hivyo si rahisi kwao kuomba Spika atangaze kuwa ana kisungura, pia huenda hata huyo Mhe kwenye kiti naye ana kisungura, pia inadaiwa kwamba hata waheshimiwa wenye waume zao huwaacha huko walipo na kuamua kwenda mjengoni na visungura.
   
Loading...