Wahenga waliliona hili la Kikwete na viongozi wa dini

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
1,662
'Mkuki mtamu kwa nguruwe,ila mchungu kwa binadamu'. si kila siku tunasikia viongozi wetu wa dini tena kwa maono wanakemea na kusema baadhi ya viongozi wa nchi ni wala rushwa/mafisadi? Kwa nafasi yao wametekeleza wajibu wao kukemea maovu, je wao nani wa kuwakemea?

J.K akisema kuna baadhi ya viongoz wa dini ni wauza poda, ni vibaya, kwani yeye si ni mtanzania, tena Rais? Na je kwan nini uwongo hamna viongozi wa dini wauza unga?

Na alivyosema viongoz wa dini, kwani dini ni wakristo tuu? Jamani hebu tusimchukie kikwete hivyo.
 
Yaani huyu Mokiwa ana confidence sijapata kuona khaaaaa...yaani anaamrisha kondoo wamdharau mtoto wa kikweehee
 
hakutakiwa kusema tu,alitakiwa kuongezea kwamba tumewakamata au kutoa maelezo hatua gani zimechukuliwa kukomesha hiyo kitu,sasa nae anakuja na hadithi kama tunazosimuliana kijiweni!!
 
Rais angekuwa amewataja hao wahusika kusingekuwa na mjadala juu ya kauli yake.sasa amehutubia mwisho akaacha maswali yasiyo na majibu angali yeye mwenyewe ndiyo ana majibu.
Kuwataja hao watumishi wa dini ingekuwa ni hatua mojawapo ktk kuwakomesha wanaojihusisha na biashara hiyo kwani huenda watumishi hao wanafanya madili hayo kwa kutumia migongo ya misaada inayotolewa nje kwa mashirika ya dini.
 
'mkuki mtamu kwa nguruwe,ila mchungu kwa binadamu'. .si kila siku tunasikia viongozi wetu wa dini tena kwa maono wanakemea na kusema baadhi ya viongozi wa nchi ni wala rushwa/mafisadi!?kwa nafasi yao wametekeleza wajibu wao kukemea maovu. . .jee wao nani wa kuwakemea,J.K Akisema kuna baadhi ya viongoz wa dini ni wauza poda,ni vibaya,kwani yeye si ni mtanzania,tena rais?na je kwan ni uwongo hamna viongozi wa dini wauza unga? Na alivyosema viongoz wa dini,kwan dini ni wakristo tuu?. .jamani hebu tusimchukie kikwete hvyo.

Inaelekea kuwa una upeo mdogo sana kutambua majkumu ya viongozi wa dini na yale ya Raisi wa nchi. Tatizo hapa ni kuwa Raisi badala ya kutumia vyombo vya ulinzi vilivyo chini yake anaishia kuwataka wahalifu kuacha uhalifu wanaofanya ambao unawaumiza vijana wa kitanzania kwa kiwango kikubwa. Mimi nilitarajia Rais afike pale kusema kuwa tayari viongozi fulani na fulani wapo mahakamani kwa kujihusisha na biashara hiyo.

Kuhusu viongozi wa dini kukemea maovu, huo ndio ukomo wa majakumu yao kwa kuwa hawana madaraka ya kutenda kama aliyonayo Rais.
 
tatizo si kuwa hakuna viongozi wa dini wanaojihusisha na hiyo biashara, maana hata mimi ningekuwa nafanya hiyo biashara naweza nikajifanya mtumishi wa mungu tena nikafungua kanisa langu nikaliita kwa jina ninalotaka, lazima ningepata waumini tu, MOKIWA hakuwa mnafiki, hakutaka JK aseme kinafiki (UDINI, ALILISEMEA KWENYE SHUGHULI YA DINI YA KIKRISTO) alitaka awataje bila kuuma uma maneno.
 
Hili suala lingechukua sura hii na mtiririko huu isingeleta utata:

>Raisi angewaita viongozi wa dini mbalimbali (wahindu, islaam, wakristo, wale wa dini za jadi nk). Anao uwezo huo (mbona anawaita wazee wa Dar anapowahitaji ?)

>angehakikisha vyombo vya habari vipo pia

>Angelizungumzia suala la dawa za kulevya kwa mapana yake.

>Mwisho angemwachia mhusika wa vyombo vya usalama awataje wahusika na hatua zilizochukuliwa (kwenye mkutano huo huo au hata baadaye tarehe tajwa)

Hii ingeondoa utata na hisia za agenda ya siri

Huu ni mtazamo tuu
 
'mkuki mtamu kwa nguruwe,ila mchungu kwa binadamu'. .si kila siku tunasikia viongozi wetu wa dini tena kwa maono wanakemea na kusema baadhi ya viongozi wa nchi ni wala rushwa/mafisadi!?kwa nafasi yao wametekeleza wajibu wao kukemea maovu. . .jee wao nani wa kuwakemea,J.K Akisema kuna baadhi ya viongoz wa dini ni wauza poda,ni vibaya,kwani yeye si ni mtanzania,tena rais?na je kwan ni uwongo hamna viongozi wa dini wauza unga? Na alivyosema viongoz wa dini,kwan dini ni wakristo tuu?. .jamani hebu tusimchukie kikwete hvyo.
Naomba uelewe.Hakuna mtu anayepinga yeye kuwanyoshea kidole viongozi wa dini wauza unga.Tunachokataa ni busara akiyotumia.Kama raisi, he had a better alternative.Pili kwa sababu yeye mwenyewe ana shortcomings nyingi mno,hana moral authority ya kuwakemea na kuwanyoshea kidole wengine.
 
Wengi wanaolalamika si kwa kuwa Kikwete kasema uwongo au ukweli kuhusu viongozi wa dini kujihusisha na madawa ya kulevya bali ni kwa kuwa anawafahamu hao, na uwezo anao, nguvu anazo, na sababu anazo, ni kwanini asiwe na nia thabiti na kuwakamata na kuwashitaki? Hatutetei mediocrity hapa!
 
tushawajuwa wauza unga Tanzania wala hatupati shida tena anaelalamika ndio muhusika huyo Ahsante sana muheshimiwa Rais kwa kututajia wauza unga, kazi ya kutaja majina hio si yako watataja wahusika kwenye idarea hiyo
Bado natafakari, nitarudi baadaye
 
'mkuki mtamu kwa nguruwe,ila mchungu kwa binadamu'. .si kila siku tunasikia viongozi wetu wa dini tena kwa maono wanakemea na kusema baadhi ya viongozi wa nchi ni wala rushwa/mafisadi!?kwa nafasi yao wametekeleza wajibu wao kukemea maovu. . .jee wao nani wa kuwakemea,J.K Akisema kuna baadhi ya viongoz wa dini ni wauza poda,ni vibaya,kwani yeye si ni mtanzania,tena rais?na je kwan ni uwongo hamna viongozi wa dini wauza unga? Na alivyosema viongoz wa dini,kwan dini ni wakristo tuu?. .jamani hebu tusimchukie kikwete hvyo.

Na alivyosema viongoz wa dini,kwan dini ni wakristo tuu?.
Kama alikuwa anawataka viongozi wa dini zote je masheikh walikuwepo pale?
Je ilikuwa wakati sahihi kulisema hilo alilolisema?
Unategemea kwa kauli kama hizi nani anapendezwa nazo?
Je siku hiyo ilikuwani maalum kupiga vita dawa za kulevya?
Utakubaliana na mm kwamba kikwete sio mbayuwayu?kwa sababu hata kama alikuwa anadesa ile hotuba akili za kuambiwa si unachanganya na zako?
Je wewe unaamini kikwete anachukiwa kwa sababu ya kusema ukweli au unafiki wake?
 
Hadithi za kikwete na madawa ndo hizohizo,aliwah sema ana rist ya majina ya wauza unga mpaka leo hakuna hatua iliyochukuliwa.Kikwete anakurupuka sana tatz kwa nini asitaje ili kuwapprove wrong viongozi wa dini?otherwise tunamdharau kama alivosema mokiwa
 
'Mkuki mtamu kwa nguruwe,ila mchungu kwa binadamu'. si kila siku tunasikia viongozi wetu wa dini tena kwa maono wanakemea na kusema baadhi ya viongozi wa nchi ni wala rushwa/mafisadi? Kwa nafasi yao wametekeleza wajibu wao kukemea maovu, je wao nani wa kuwakemea?

J.K akisema kuna baadhi ya viongoz wa dini ni wauza poda, ni vibaya, kwani yeye si ni mtanzania, tena Rais? Na je kwan nini uwongo hamna viongozi wa dini wauza unga?

Na alivyosema viongoz wa dini, kwani dini ni wakristo tuu? Jamani hebu tusimchukie kikwete hivyo.
Swala siyo kukemea maovu, hoja ni uliye na mamlaka na wewe kupiga kelele kama vile umesahau kwamba ukiwa makini wewe katika kuwajibika kwa mujibu wa sheria unaweza kuleta mabadiliko makubwa kuliko hawa wasio na jeshi, wasioweza kuunda chombo chochote kutekeleza wanachokitaka. Na kuhusu viongozi wa dini moja kupiga kelele hilo halina mjadala aliongea katika mazingira ya kikristo akiwa na wakristo ulitaka wajibu waislamu kwani aliongea akiwa nao hayawahusu wao katika hili ni wapita njia, mgeni wa mtu anapoongea akiwa ndani ya nyumba kuingilia ni ushamba na upunguani wa akili kama badala ya kuhakikisha watu wako wanaenda kwa mujibu wa mafundisho ya yule unayemuamini bali ni kufuatilia yule wa upande mwingine anaongea nini maana yake kuwepo kwako ni kwa kuwa yule yupo asipokuwepo basi wewe hautakuwepo, hii safi sana.
 
Tatizo hapa siyo kuwakemea viongozi wa dini, tatizo ni pale rais anapogeuka kuwa vuvuzela kwenda anapayuka kadamnasi na kulalamikia maswala ambayo yako ndani ya uwezo wake kuyashughulikia.
Yeye kama presda angeweza hata kuwaita hao maaskofu na kuwaonya. Au angeweza kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria. Lakini hakufanya hivyo, badala yake akaamua kulirusha hadharani!
Nadhani alifanya kwa wrong motive ya kutaka kuwatisha maaskofu, matokeo yake imekula kwake. Kalikoroga mwenyewe, alinywe.
 
ccm eeeh,ccm eeeh ccm kwa kuwatukana wakristu, ccm nambari wani. ccm weee ccm weee, ccm na udini nambari wani!!!!
 
nafikiri kaamua kutumia busara na kuwasamehe kwa style hiyo. mbona akisamehe wafungwa hamlalamiki? cha msingi wajirekebishe kama sio sikio la kufa...
 
Back
Top Bottom