Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.

Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
Sitaki kuikukumbuka ile dawa, sio kwa kuwashwa kule, siku tatu mtu unawashwa tu unajikuna tu kama mwendawazimu
 
Ukimaliza tu kuinywa basi jua kuwa umejikatia leseni ya siku 3 bila kuoga.

Pia kabla ya kunywa hakikisha una vifaa tiba kama gunzi la muhindi lililokauka kwa ajili ya kupooza miwasho midogo dogo, na kama iyo haitoshi basi kuwa na kisu butu kupoozea ile miwasho ya ghafla pale kwenye unyayo wa mguu

Tukirudi kwenye kutapika, basi jua utatapika kila chakula ulichokula, kikiisha ndipo utakapoanza kutapika maji na baadae nyongo ya njano na kijani kwa wale ma concord
Kutapika nyongo ilikuwa ni lazima, ile dawa jamani.....khaa!
 
Hii dawa ndio ilinifanya nichukie dawa.
Nakumbuka nilikuaga nakunywa dawa bila kukunja sura mpaka siku nimerudi kutoka shule naumwa. Kufika bibi akanikorogea chai ya rangi akaniwekea na dawa (Chloroquine) nikanywa.. nilitapika isivyo kawaida. Kuanzia hapo nikachukia chai yenye sukari nyingi na sikuwahi kulamba tena sukari. Hata nikiona mtu analamba sukari nasisimkwa mwili. Nikaogopa dawa na kuchukia mpaka leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mamake hiyo dawa kuwasha kwake ni noma,nilishukuru nilipoanza kutumia fansidar ikawa inafanya kazi haraka bila kuwashwa na kutapika.
 
Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.

Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.

Kunywa Q-kwini bila Piriton ilikuwa haiwezekani
 
Back
Top Bottom