kikulacho...
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 321
- 224
Sitaki kuikukumbuka ile dawa, sio kwa kuwashwa kule, siku tatu mtu unawashwa tu unajikuna tu kama mwendawazimuNatafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.
Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
Kutapika nyongo ilikuwa ni lazima, ile dawa jamani.....khaa!Ukimaliza tu kuinywa basi jua kuwa umejikatia leseni ya siku 3 bila kuoga.
Pia kabla ya kunywa hakikisha una vifaa tiba kama gunzi la muhindi lililokauka kwa ajili ya kupooza miwasho midogo dogo, na kama iyo haitoshi basi kuwa na kisu butu kupoozea ile miwasho ya ghafla pale kwenye unyayo wa mguu
Tukirudi kwenye kutapika, basi jua utatapika kila chakula ulichokula, kikiisha ndipo utakapoanza kutapika maji na baadae nyongo ya njano na kijani kwa wale ma concord
Na piriton pia zilisaidia!umenikumbusha hapo kwenye kuwasha ila kuna dawa nilipewa calamine lotion ilikuwa inasaidia.
Kujikuna kule mwili mzima tulikuwa tunakuita kupiga gitaa.Sitaki kuikukumbuka ile dawa, sio kwa kuwashwa kule, siku tatu mtu unawashwa tu unajikuna tu kama mwendawazimu
Klorokwini ya Daby mambo?Wengi mnalalamika kuwashwa mbona mimi sikuwahi kuwashwa aisee
Ulitapikwa?
NdioUlitapikwa?
Hata mie siwahi washwa hata siku moja, uchungu tu ule hicho kikombe nilichonywea dawa nilikuwa natamani nikipasueWengi mnalalamika kuwashwa mbona mimi sikuwahi kuwashwa aisee
Pole sanaHii dawa ndio ilinifanya nichukie dawa.
Nakumbuka nilikuaga nakunywa dawa bila kukunja sura mpaka siku nimerudi kutoka shule naumwa. Kufika bibi akanikorogea chai ya rangi akaniwekea na dawa (Chloroquine) nikanywa.. nilitapika isivyo kawaida. Kuanzia hapo nikachukia chai yenye sukari nyingi na sikuwahi kulamba tena sukari. Hata nikiona mtu analamba sukari nasisimkwa mwili. Nikaogopa dawa na kuchukia mpaka leo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.
Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
DahMamake hiyo dawa kuwasha kwake ni noma,nilishukuru nilipoanza kutumia fansidar ikawa inafanya kazi haraka bila kuwashwa na kutapika.