Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

Wazungu watu wabaya sana walifanya makusudi kutukomoa sisi waafrika kututengezea hii dawa ya chroloquine,kwanini wao walikuwa wanatumia dawa nyingine tofauti na chroloquine wanapougua malaria wakiwa huku Afrika?
 
Niko darasa la 5 nilikosea dose, ile 4x4x2, basi nikanywa asubuhi, mchana na ucku jamani asikuambie mtu. Usifanye mchezo roho inapotaka kuacha mwili, Kaka yangu ananiuliza dawa zako ziko wapi? Nikamjibu nimemaliza, wewe alikoroga mavi ya ng'ombe nadhani alichanganya na ya watu, nyie msisikie habari ya kufa.
Huku nje watu kilio, wanajua siamki, nikapewa maziwa fresh lita 4, nikanyweshwa na hivyo vinyesi, jamani Mungu yupo, akisema hufi hufi. Nilianza kutapika nilitapika mpaka nilikuwa siwezi kufumbua macho, kwa kifupi kila mtu alijua tu hell!! Mpaka ucku wa saa 4, ndio naenda kulala. Jinsi walivyonitandikia unajua kabisa wananiaga, niliogoshwe nikavalishwa nguo nzuri sana za kwangu kwa akili ya kawaida nilijua wananizuia na hii baridi ninayohisi. Kumbe wenzangu walikuwa wananiaga kuwa hakuna namna. Amini maneno yangu, usiku kama wa saa 7 ninaona kwa macho yangu malaika, mkononi kashika kitu kinatoa damu. Naona kwa macho yangu, akaingiza ule mkono wake tumboni kwangu, akatoa kitu nikahisi maumivu sana, akaweka kile kingine, naona kwa macho. Kushoto kwangu wamelala watu wengi, ambao walikuwa wako tayari ninapokata roho wanisaidie. Lakini wenyewe hawamuoni yule malaika, alipokuwa anaondoka nilipiga kelele kubwa sana, nikagongwa na kitu usoni kwa kishindo kikubwa sana. Niliona nyota kama 200 hivi, jasho lililowesha kitanda chote pamoja na nguo zote. Wakaniamsha wakasikitika sana, nikanywa maji nikalala mpaka kesho yake. Acheni jamani Mungu yupo.
Haaaa haaaa Gullam mavi ya binadamu pole sana mkuu
 
nilikuwa nikizimeza hizo au Kwinini.. maskio yanalia diiiii iiiiiiii siku nzima.

Bora wewe Diiiiiiiii diiiiiiiiiiii, MIMI ILIKUA NI ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii siku 3
 
Niko darasa la 5 nilikosea dose, ile 4x4x2, basi nikanywa asubuhi, mchana na ucku jamani asikuambie mtu. Usifanye mchezo roho inapotaka kuacha mwili, Kaka yangu ananiuliza dawa zako ziko wapi? Nikamjibu nimemaliza, wewe alikoroga mavi ya ng'ombe nadhani alichanganya na ya watu, nyie msisikie habari ya kufa.
Huku nje watu kilio, wanajua siamki, nikapewa maziwa fresh lita 4, nikanyweshwa na hivyo vinyesi, jamani Mungu yupo, akisema hufi hufi. Nilianza kutapika nilitapika mpaka nilikuwa siwezi kufumbua macho, kwa kifupi kila mtu alijua tu hell!! Mpaka ucku wa saa 4, ndio naenda kulala. Jinsi walivyonitandikia unajua kabisa wananiaga, niliogoshwe nikavalishwa nguo nzuri sana za kwangu kwa akili ya kawaida nilijua wananizuia na hii baridi ninayohisi. Kumbe wenzangu walikuwa wananiaga kuwa hakuna namna. Amini maneno yangu, usiku kama wa saa 7 ninaona kwa macho yangu malaika, mkononi kashika kitu kinatoa damu. Naona kwa macho yangu, akaingiza ule mkono wake tumboni kwangu, akatoa kitu nikahisi maumivu sana, akaweka kile kingine, naona kwa macho. Kushoto kwangu wamelala watu wengi, ambao walikuwa wako tayari ninapokata roho wanisaidie. Lakini wenyewe hawamuoni yule malaika, alipokuwa anaondoka nilipiga kelele kubwa sana, nikagongwa na kitu usoni kwa kishindo kikubwa sana. Niliona nyota kama 200 hivi, jasho lililowesha kitanda chote pamoja na nguo zote. Wakaniamsha wakasikitika sana, nikanywa maji nikalala mpaka kesho yake. Acheni jamani Mungu yupo.

duuuhh ninacheka kama mazuri
 
hii dawa ilikuwa na ndugu yake aliyeitwa quinine(kwainini).... dah yan nlikuwa nikiumwa nahisi kupona ghafla nliposikia hizi dawa.... ilikuwa pia kifua kikisumbua kuna jamaa walimwita mkojo wa punda.
Huo mkojo ilkw nikitaka kunywa lazima kuwe na kitu kitamu tamu pembeni haahaa....Hivi bado upo sikuhiz?
 
uzuri ilikuwa si dawa ya kuongeza nguvu za kiume maana kipindi hicho tatizo hilo lilikuwa hamna limeibuka hivi karibuni u yaani watu tungekuwa tunajuwa tu kuwa huyu kanywa chloroquine maana asubuhi wangekuwa wanatembea wanajikuna kama nini
 
'Kolokwini' ile dawa ina nguvu za ajabu, yaani ikikaribia kugusa ulimi tu ina uwezo wa kukivuta nje chakula chote ulichokula. Dawa chungu kama imetengenezwa na mashetani, halafu bahati mbaya iwe inakuonea, yaani ukinywa ni full kuwashwa kwa muda siku tatu mfululizo bila kupumzika, halafu muwasho wake ni hadi kwenye kinyeo na makende. Ukianza kuwashwa hujitokezi mbele za watu, maana kuna maeneo utashindwa kujikuna. Ukigusa maji hata tone tu kuwasha kunaongezeka mara tatu zaidi.
Ilikuwa ni projrct ya kuzalisha mashoga Afrika, Kizazi kilichotumia sana dawa hizo ndo hichi cha akija James delicious.
 
Ilinifanya nimchukie mama yangu mzazi badala ya kumpenda, nakumbuka kuna siku naumwa halafu natetemeka hatari, mama akaniita njoo ukae uku jikoni uotee moto mi napika, aisee nilikaa pale ghafla tumbo likachefuka nikatapikia jungu la Ugali, mama alinipiga na mwiko utazani hajui kama naumwa daaaah ile dawa hapana kwa kweli.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom