Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

inawezekana hata haya matatizo ya wanaume wa dar uume kutosimama nyuzi 90 umechangiwa na haya madawa unakuta mwanaume mzima akifungua zipu kukojoa inabidi achutame kama mwanamke kwani bila hivyo mkojo utaloanisha suruali yote.
 
nilikuwa nikizimeza hizo au Kwinini.. maskio yanalia diiiii iiiiiiii siku nzima.
Umenikumbusha mbali ongezea na kuona maruweruwe ,unakuwa wa kulala tu,mi mpaka bi mkubwa alihisi ashanipoteza nikapewa dozi ya maziwa ya THT fasta
 
Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.

Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
hii dawa ilikuwa na ndugu yake aliyeitwa quinine(kwainini).... dah yan nlikuwa nikiumwa nahisi kupona ghafla nliposikia hizi dawa.... ilikuwa pia kifua kikisumbua kuna jamaa walimwita mkojo wa punda.
 
Mi nakumbuka nilikuwa nafinyanga kwenye tongi la ugari nameza bila kutafuna lkn ikifika tumbon tu kosa mdomo wote unakuwa mchungu.
 
hii dawa ilikuwa na ndugu yake aliyeitwa quinine(kwainini).... dah yan nlikuwa nikiumwa nahisi kupona ghafla nliposikia hizi dawa.... ilikuwa pia kifua kikisumbua kuna jamaa walimwita mkojo wa punda.
pia kulikuwa Na sindano inaitwa crystapen
 
Mm sijajua mpaka leo ule muwasho kutoka kwenye unyayo, aise nishakunywa kma mara mbili yaaani hekaheka lake zaid ya siku tatu, vitu kama bunzi la mahindi, magamba ya nazi ni kitu cha kawaida sana kwa ajiri ya kujikunia.
Sasa itokee unajikuna maji yamekumwagikia ndipo hapo utakapojua aiseeee, lengo la zile dawa kuwa vile cjajua kabisa ni nini
 
Mm sijajua mpaka leo ule muwasho kutoka kwenye unyayo, aise nishakunywa kma mara mbili yaaani hekaheka lake zaid ya siku tatu, vitu kama bunzi la mahindi, magamba ya nazi ni kitu cha kawaida sana kwa ajiri ya kujikunia.
Sasa itokee unajikuna maji yamekumwagikia ndipo hapo utakapojua aiseeee, lengo la zile dawa kuwa vile cjajua kabisa ni nini

Kibaya zaidi ukijikuna muwasho ndio unazidi, zile dawa aliyezitengeneza sijui alikuwa anawaza nini?
 
000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000077000m007777
 
Chloroquine bado zipo kwenye soko la Tz ingawa si kwa wingi...hutumiwa na watu wenye ugonjwa wa Seli Mundu(Sickle Cell Disease) kama kinga ya Malaria.....hii dawa ilinifanya niwe mshabiki wa sindano...ni mbaya kuliko chochote nilichowahi kuingiza kinywani.
 
chroloquine sina ham nayo aseeh ilikuwa nikinywa masikio yangu yanabadili quality ya sound yani usikivu wangu ulikuwa kama cassete ya radio inayoplay huku nyuzi zinatoka. ilikuwa ina-edit masikio yangu dah!
 
Dah mim mpka leo SIKIO LANGU LA KULIA HALISIKIII KABISA YAANI TOKA MWAKA 2003 NILIPOMEZA DAWA HIYOOO DAHHHHH CHROLOQUINEEEEE...
 
Dah mim mpka leo SIKIO LANGU LA KULIA HALISIKIII KABISA YAANI TOKA MWAKA 2003 NILIPOMEZA DAWA HIYOOO DAHHHHH CHROLOQUINEEEEE...
 
Yaani amini maneno yangu, ile ndio dawa inayotibu marelia mpaka leo hii.
 
Niko darasa la 5 nilikosea dose, ile 4x4x2, basi nikanywa asubuhi, mchana na ucku jamani asikuambie mtu. Usifanye mchezo roho inapotaka kuacha mwili, Kaka yangu ananiuliza dawa zako ziko wapi? Nikamjibu nimemaliza, wewe alikoroga mavi ya ng'ombe nadhani alichanganya na ya watu, nyie msisikie habari ya kufa.
Huku nje watu kilio, wanajua siamki, nikapewa maziwa fresh lita 4, nikanyweshwa na hivyo vinyesi, jamani Mungu yupo, akisema hufi hufi. Nilianza kutapika nilitapika mpaka nilikuwa siwezi kufumbua macho, kwa kifupi kila mtu alijua tu hell!! Mpaka ucku wa saa 4, ndio naenda kulala. Jinsi walivyonitandikia unajua kabisa wananiaga, niliogoshwe nikavalishwa nguo nzuri sana za kwangu kwa akili ya kawaida nilijua wananizuia na hii baridi ninayohisi. Kumbe wenzangu walikuwa wananiaga kuwa hakuna namna. Amini maneno yangu, usiku kama wa saa 7 ninaona kwa macho yangu malaika, mkononi kashika kitu kinatoa damu. Naona kwa macho yangu, akaingiza ule mkono wake tumboni kwangu, akatoa kitu nikahisi maumivu sana, akaweka kile kingine, naona kwa macho. Kushoto kwangu wamelala watu wengi, ambao walikuwa wako tayari ninapokata roho wanisaidie. Lakini wenyewe hawamuoni yule malaika, alipokuwa anaondoka nilipiga kelele kubwa sana, nikagongwa na kitu usoni kwa kishindo kikubwa sana. Niliona nyota kama 200 hivi, jasho lililowesha kitanda chote pamoja na nguo zote. Wakaniamsha wakasikitika sana, nikanywa maji nikalala mpaka kesho yake. Acheni jamani Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom