Wahenga tukumbushane Klorokwini na mambo yake

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,271
Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.

Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
 
'Kolokwini' ile dawa ina nguvu za ajabu, yaani ikikaribia kugusa ulimi tu ina uwezo wa kukivuta nje chakula chote ulichokula. Dawa chungu kama imetengenezwa na mashetani, halafu bahati mbaya iwe inakuonea, yaani ukinywa ni full kuwashwa kwa muda siku tatu mfululizo bila kupumzika, halafu muwasho wake ni hadi kwenye kinyeo na makende. Ukianza kuwashwa hujitokezi mbele za watu, maana kuna maeneo utashindwa kujikuna. Ukigusa maji hata tone tu kuwasha kunaongezeka mara tatu zaidi.
 
'Kolokwini' ile dawa ina nguvu za ajabu, yaani ikikarubia kugusa ulimi tu ina uwezo wa kukivuta nje chakula chote ulichokula. Dawa chungu kama imetengenezwa na shetani, halafu bahati mbaya iwe inakuonea, yaani ukinywa ni full kuwashwa kwa muda siku tatu mfululizo bila kupumzika, halafu muwasho wake ni hadi kwenye kinyeo na makende. Ukianza kiwashwa hujitokezi mbele za watu, maana kuna maeneo utashindwa kujikuna. Ukigusa maji hata tone tu kuwasha kunaongezeka mara tatu zaidi.
Kosa kwangu ilikuwa kukoga maji baridi....hapo kuwasha ni maradufu, pia nakumbuka miaka ya 80/90 wadada wakitaka kutoa mimba au kujiua waliitumia sana.
 
Dah! hizi dawa, mimi nilikuwa nikizimeza baada ya siku mbili zinaanza kuniwasha na ifikapo si ya nne basi usingizi unakata kwa hiyo naweza kesha macho huku nikijikuna......hatari sana
Mbaya zaidi enzi zile kulikuwa Na radio Tanzania tu Na yenyewe usiku inakata matangazo. Kama kwenu hamna radio kaseti lazima ukeshe
 
Ukimaliza tu kuinywa basi jua kuwa umejikatia leseni ya siku 3 bila kuoga.

Pia kabla ya kunywa hakikisha una vifaa tiba kama gunzi la muhindi lililokauka kwa ajili ya kupooza miwasho midogo dogo, na kama iyo haitoshi basi kuwa na kisu butu kupoozea ile miwasho ya ghafla pale kwenye unyayo wa mguu

Tukirudi kwenye kutapika, basi jua utatapika kila chakula ulichokula, kikiisha ndipo utakapoanza kutapika maji na baadae nyongo ya njano na kijani kwa wale ma concord
 
Mimi kuinywa ile dawa lazima niwe na sukari pembeni, lakini cha ajabu ile dawa ikigusa tu ulimi lazima nitapike. Nikagundua kuifinyanga kwenye tonge la ugali nameza zimazima. Kingine wazee walikuwa watu wa afya so the first option nilikuea naomba nichomwe sindano badala ya kunywa ile dawa. Naamini ile ni sumu mbaya sana waafrica tulinyweshwa
 
Ukimaliza tu kuinywa basi jua kuwa umejikatia leseni ya siku 3 bila kuoga.

Pia kabla ya kunywa hakikisha una vifaa tiba kama gunzi la muhindi lililokauka kwa ajili ya kupooza miwasho midogo dogo, na kama iyo haitoshi basi kuwa na kisu butu kupoozea ile miwasho ya ghafla pale kwenye unyayo wa mguu

Tukirudi kwenye kutapika, basi jua utatapika kila chakula ulichokula, kikiisha ndipo utakapoanza kutapika maji na baadae nyongo ya njano na kijani kwa wale ma concord
Nimekumbuka nikaanza kuwashwa mkuu
 
Natafakari, hivi aliyetengeneza Chloroquine alikuwa anawaza nini hasa ile harufu bado naisikia dawa ile ili upone ni lazima ukimaliza dosage utapike ndipo upate nafuu.

Mara ya mwisho kutumia ilikua mwaka 2000 sijui kama muuguzi yule wa Minaki Dispensary bado yupo 4X4X2 ule uchungu basi sio wa dunia hii olivia common dosage.
Hahahha...mimi nilitumia mwaka 2000 nikiwa Chuo, nilimeza 2, baada ya masaa mawili sura yangu ikawa sawasawa na Mh. Pinda.

Nilisahau kwamba nipo allergic na chloroquine...
 
Ukimaliza tu kuinywa basi jua kuwa umejikatia leseni ya siku 3 bila kuoga.

Pia kabla ya kunywa hakikisha una vifaa tiba kama gunzi la muhindi lililokauka kwa ajili ya kupooza miwasho midogo dogo, na kama iyo haitoshi basi kuwa na kisu butu kupoozea ile miwasho ya ghafla pale kwenye unyayo wa mguu

Tukirudi kwenye kutapika, basi jua utatapika kila chakula ulichokula, kikiisha ndipo utakapoanza kutapika maji na baadae nyongo ya njano na kijani kwa wale ma concord
Nimecheka kama mazuri.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom