Wahenga nisaidieni, Nini kilimsibu Fernando Torres kupotea baada ya kuhama Liverpool?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,501
44,611
Naamini wote mnamkumbuka Fernando Torres El Nino.

Jamaa alipotoka Atletico Madrid kwenda Liverpool alikuwa wa moto sana. Alipofika Liverpool hakuhitaji apewe muda, aliuwasha moto kwa haraka. Alikuwa straika tishio, hilo halikuwa na ubishi. Hata mmoja wa mabeki mahiri kwa miaka hyo ndani ya EPL, Nemanja Vidic alikuwa anapata shida ya kumkaba Torres. Ilifikia kipindi Vidic alipata kadi 3 nyekundu katika mechi 3 mfululizo wanazokutana Man Utd Vs Liverpool.

Ila Torres alipohama tu kwenda Chelsea, matatizo yalianzia hapo na hakuwahi kurudi katika ubora wake aliokuwa nao Liver. Mengi yamezungumzwa, ikiwemo Didier Drogba kuhusika ktk misumari.

Je nini kilimfanya Torres apotee kwenye ramani ya soka mara tu baada ya kuhama Liverpool?
 
Torres alijijengea jina na heshima kubwa sana kwetu mashabiki wa Liverpool kiasi kwamba tulimsujudu kama 'mungu'.

Binafsi nilijiita El Nino na mtaani na shule ndio ilikua jina langu. Jamaa alikua anajua sana. Alifumania nyavu kwa kila aina ya style aliyopenda.

Kitendo kilichompa umaarufu zaidi kwetu mashabiki wa Liverpool ni ile kufunga sana hasa team kubwa ambao ni wapinzani kama Man U, Chelsea na Arsenal.

Kama ulivyosema mleta mada ni kweli hata katika Biography yake Nemanja Vidic anakiri kuwa mpaka leo hii mateso aliyoyapata kutoka kwa Torres hatakaa ayasahau maisha yake yote.

Torres alikua idol kwa wana Liverpool, tulimpenda na tukasahau kuwa tunatakiwa tupende team sana kuliko mchezaji binafsi.

Kilichotuumiza zaidi ni namna alivyotuacha kwa style ya aina yake bila kutaraji siku ya mwisho ya dirisha la usajili tarehe 31 January 2011 tena ni baada ya kutuma transfer request siku nne nyuma ambayo uongozi wa klabu uliitupa kapuni. Hii siku ni kati ya siku nilizoumia sana.

Baada ya hapo alibatizwa jina na kuitwa Judas (msaliti) na jezi zake zilichomwa moto kwa wingi na mashabiki tulikua na maumivu makali moyoni kutokana na hali aliyokua anatuacha nayo kama team.

Nadhani maumivu na msononeko wetu ndio ilikua bad karma kwake mpaka ikapelekea kutokuwa Torres yule aliejulikana japo anaweza kujifariji kwa kushinda mataji kadhaa akiwa na Chelsea lakini FT9 nadhani kati ya maamuzi ambayo huwa anajutia mpaka siku hii ni namna alivyoachana na Liverpool.

Still tunakumbuka mazuri yake mengi japo kitendo alichotufanyia dakika za majeruhi kinabaki kuacha jeraha kwenye uhusiano wetu nae.

Once A Red, Always A Red.
YNWA El Nino.
 
Wachezaji huhama wakiwa wamelenga vikombe au pesa nyingi.
Hua hawaangalii hii klabu wanayoenda inaendana na wao? Au itawapa nafasi?

Mfano Alex Song anatoka Arsenal anaenda Barcelona Kocha wa Barca anasema '... tumepata msaidizi wa Busquet, akiumia au akiwa na udhuru Alex atasaidia'
Na bado alienda, tunajua kilichompata.

Torres alienda Chelsea huku kocha akiwa mhubiri wa kupaki mabasi huku akitaka mshambuliaji mwenye nguvu ambaye alikua ni Drogba abaki mbele peke yake akihaha. Torres hakuzoea maisha hayo, alikua anagewa assisst na wakina Gerard akawa anaenjoy maisha.
 
Torres alijijengea jina na heshima kubwa sana kwetu mashabiki wa Liverpool kiasi kwamba tulimsujudu kama 'mungu'.

Binafsi nilijiita El Nino na mtaani na shule ndio ilikua jina langu. Jamaa alikua anajua sana. Alifumania nyavu kwa kila aina ya style aliyopenda.

Kitendo kilichompa umaarufu zaidi kwetu mashabiki wa Liverpool ni ile kufunga sana hasa team kubwa ambao ni wapinzani kama Man U, Chelsea na Arsenal.

Kama ulivyosema mleta mada ni kweli hata katika Biography yake Nemanja Vidic anakiri kuwa mpaka leo hii mateso aliyoyapata kutoka kwa Torres hatakaa ayasahau maisha yake yote.

Torres alikua idol kwa wana Liverpool, tulimpenda na tukasahau kuwa tunatakiwa tupende team sana kuliko mchezaji binafsi.

Kilichotuumiza zaidi ni namna alivyotuacha kwa style ya aina yake bila kutaraji siku ya mwisho ya dirisha la usajili tarehe 31 January 2011 tena ni baada ya kutuma transfer request siku nne nyuma ambayo uongozi wa klabu uliitupa kapuni. Hii siku ni kati ya siku nilizoumia sana.

Baada ya hapo alibatizwa jina na kuitwa Judas (msaliti) na jezi zake zilichomwa moto kwa wingi na mashabiki tulikua na maumivu makali moyoni kutokana na hali aliyokua anatuacha nayo kama team.

Nadhani maumivu na msononeko wetu ndio ilikua bad karma kwake mpaka ikapelekea kutokuwa Torres yule aliejulikana japo anaweza kujifariji kwa kushinda mataji kadhaa akiwa na Chelsea lakini FT9 nadhani kati ya maamuzi ambayo huwa anajutia mpaka siku hii ni namna alivyoachana na Liverpool.

Still tunakumbuka mazuri yake mengi japo kitendo alichotufanyia dakika za majeruhi kinabaki kuacha jeraha kwenye uhusiano wetu nae.

Once A Red, Always A Red.
YNWA El Nino.
Umemaliza kila kitu mkuu, poleni sana!
 
Naamini wote mnamkumbuka Fernando Torres El Nino.

Jamaa alipotoka Atletico Madrid kwenda Liverpool alikuwa wa moto sana. Alipofika Liverpool hakuhitaji apewe muda, aliuwasha moto kwa haraka. Alikuwa straika tishio, hilo halikuwa na ubishi. Hata mmoja wa mabeki mahiri kwa miaka hyo ndani ya EPL, Nemanja Vidic alikuwa anapata shida ya kumkaba Torres. Ilifikia kipindi Vidic alipata kadi 3 nyekundu katika mechi 3 mfululizo wanazokutana Man Utd Vs Liverpool.

Ila Torres alipohama tu kwenda Chelsea, matatizo yalianzia hapo na hakuwahi kurudi katika ubora wake aliokuwa nao Liver. Mengi yamezungumzwa, ikiwemo Didier Drogba kuhusika ktk misumari.

Je nini kilimfanya Torres apotee kwenye ramani ya soka mara tu baada ya kuhama Liverpool?
Pale Darajani alikutana na Tembo akampiga misumari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom