Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,641
- 75,656
Watu wa kale ambao walikuwa na 'hakima'
haya bhana. Ila kama nakujua vile.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wa kale ambao walikuwa na 'hakima'
hahahahaaa ntalala nacheka sababu yakoumeniacha hoi mkuu.
una maana akina abbas Mzimba, Akilimali wanaotaka wakabidhiwe timu na akina Kitwana Kondo!?
Sababu inayokufanya wewe kujiita mhenga ni ipi?Mm mwenyewe mhenga
Kupita viunzi vingi katika maisha vigumu na vyepesi,Sababu inayokufanya wewe kujiita mhenga ni ipi?
Wahenga ni watu wenye hekima, busara na uwezo wa kufanya mamuzi sahihi.
Tatizo langu na mimi lipo hapo kwamba ni kama vile walikuwepo zamani tu na siku hizi hawapo. Wahenga walisema....kwa nini hatusemi wahenga wanasema?
Wahenga hao walisema lini??
Na walimwambia nani??
Kwanza sidhani hata Kama hao wahenga walijijua kuwa wanaitwa wahenga!!!
wahenga ni wazee wa zamani ambao kiukweli walikuwa waongo waongo na wanapendwa kutukuzwa au kuonekana wana busara kumbuka haohao walisema polepole ndio mwendo haohao wakasema chelewa chelewa utakuta mwana si wako.
Yaani walitafuta sababu ya kuonekana wapo sahihi kwa kila jambo mfano wa methali hizo juu ukichelewa ukakosa kitu fulani atakwambia nilisema chelewachelewa utakuta mwana si wako na ukifanya harakaharaka ukapata tatizo atasema nilikuasa polepole ndio mwendo vivyohivyo kwa misemo mingine mfano
mvumilivu hula mbivu na ngojangoja yaumiza matumbo.