alibaaliyo
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 622
- 567
Nimesikia na kusoma habari za chombo cha habari BBC za Wahaya wa wilaya ya Misenyi kukatazwa kuzika kwenye miji yao. Ni mila zao , tamaduni zao za kuhifadhi miili ya wapendwa wao ktk miji yao (nyumbani). Jambo ambalo limesababisha wananchi kuzika wapendwa wao usiku.
Majibu ya Mkuu wa Wilaya ni kuwa lazima kupanga Wilaya ili kupisha maendeleo kama kusambaza umeme, maji na gesi.
Hivi ni kweli waweza kubadiliaha mila za watu ghafla namna hiyo bila watu kukubaliana. Mila ni suala si rahisi kulibadilisha kwa sheria na vitisho.
Wabobezi wa sociolojia wanaweza kusaidia hapo.
Mimi kama Mtanzania nimesikitishwa sana na maamuzi hayo yasitojali tamaduni za wananchi. Hivi kama ni kulipa fidia maendeleo yanapoletwa wananchi wakishirikishwa kuwa kukubali kutolipwa fidia maendeleo yakija kuna shida gani.
Hivi ni kweli Watanzania wanakuwa na hofu mpaka kuzika usiku?.
Hayati JPM wakati ugonjwa wa korona umeingia alisema kuwa watu wazike wapendwa wao kwa mujibu wa tamaduni zao. Wizara ya afya itoe ushirikiano nao kuona Watanzajia wanazika wapendwa wao kwa mujibu wa matakwa ya familia.
Busara kama hizi tunazihitaji ktk maswala yanayohusu tamaduni za watu.