Wahasibu, wakaguzi 1,911 wafeli mitihani yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahasibu, wakaguzi 1,911 wafeli mitihani yao

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MHASIBU HALISI, Jan 11, 2012.

 1. MHASIBU HALISI

  MHASIBU HALISI Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  JUMLA ya Wahasibu na Wakaguzi 1,911 ikiwa ni asilimia 52 ya wahasibu na wakaguzi waliofanya mtihanai wa ngazi ya ATEC I, ATEC II na mtihani wa awali (Foundation Stage A & B), na mtihani wa kati (Intermediate Stage Modules C & D) na mtihani wa mwisho (Final Stage Module E & F) wamefeli mitihani hiyo.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu (NBAA) jana ndani ya viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Pius Maneno imeeleza jumla ya watainiwa 1,911 wamefeli kati ya watahiniwa 3,670 waliofanya mtihani huo.
  Maneno amesema 740 ikiwa ni asilimia 20.2 wamefahulu mtihani wao na 1,019 ambao ni sawa na asilimia 27.7 watalazimika kurudia mtihani huo kwa masomo walioshindwa katika mtihani huo.


  Akifafanua zaidi, Maneno alibainisha kuwa katika ngazi ya mwisho ‘F’ watahiniwa 183 kati ya 869 waliofanya mtihani huo wamefaulu, wengine 316 watalazimika kurudia mitihani yao huku watahiniwa 370 ikiwa ni sawa na asilimia 42.6 wamefeli katika mtihani huo.
  Alisema watahiniwa 302 kati ya 2,138 wamefaulu mtihani wa taaluma ngazi ya Module ‘E’ na wengine 431 wanalazimika kurudia somo moja, huku watahiniwa 1,405 hawakufaulu mitihani yao.
  “Jumla ya watahiniwa 185 wamefaulu mtihani wa shahada ya juu ya Uhasibu nchini-CPA (T). Idadi hii inafanya jumla ya watahiniwa waliofaulu mitihani ya CPA kufikia 3,608 tangu mitihani hii ianze – mwaka 1975,” alisema Maneno katika taarifa hiyo.
   
 2. MHASIBU HALISI

  MHASIBU HALISI Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Tafiti zisizo rasimi zinaonesha kuwa Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu ya Tanzania(NBAA) imeshajiwekea limit ya kwamba hata watu wasome namna gani , lakini watakaopata CPA kila mitihani inapofanyika haitozidi asilimia 20.

  Kwa hiyo wewe soma mpaka macho yakutoke , lakini ujue hamtofaulu kupita 20% waliyoiweka hao NBAA ! kAA TAYARI KWA KURUDIA NA KURUDIA TENA MITIHANI HADI ZAMU YAKO IKIFIKA NDO UTAIPATA HIYO CPA !
   
 3. Micha

  Micha JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Siamini kama kuna limit ya watu wanaotakiwa kufaulu CPA, kinachodetermine ni uwezo wa mtu na kadri alivyojoandaa kwa mtihani lakini pia kusoma sehemu sahihi na kufanya maswali mengi. Tumeona watu ambao walikuwa ni vipanga vyuoni wakifaulu mitihani ya CPA kirahisi tu tena kwa first sitting kwa sababu wana uwezo, wanasoma, wanaelewa na kufanya maswali mengi. Ukifanya mitihani ya NBAA kwa kujaribu au kama uwezo wako ni mdogo kamwe hautafaulu au utarudia mara nyingi sana!
   
 4. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Tuache mambo ya kufikirika, ni vema tuje na scientific reasons haswa ktk hoja na mambo ya msingi kama academics hii siyo siasa, kwani kwa hoja hii hakuna ukweli hata kidogo, issue hapa ni maandalizi ya zima moto ndiyo chanzo cha matokeo mabaya.
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mtaala wa NBAA ni upi?
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Isije ikawa kuna watu wamegeuza huu ni maradi wao...maana kwa ninavyofahamu watahiniwa hutakiwa kulipa fee kabla hawajaruhusiwa kufanya mitihani hii. Kwa hivyo pengine hii inaweza kuwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha kila sitting wanakuwa na watahiniwa wa kutosha! Si wazo baya kuanza kuangalia kwa karibu vyanzo vya mapato vya bodi hizi na jinsi mapato hayo yanavyotumika!.

  Lakini mwisho wa siku cha muhimu ni kujiandaa vizuri na kufanya mitihani hiyo vizuri ili hata kama kweli kuna hiyo 20% (or whatever threshold they might put), basi na wewe uwe mmojawao.
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mbona tunatishana yahe?
   
Loading...