Wahariri wa Vyombo Vya Habari wafukuzwa Malaika Hotel Mwanza?

mkuu vyovyote vile lakini habari hii huwezi kumlaumu Ridhiwani...
mwenye hoteli alikuwa na mamlaka ya kukataa ugeni wa Ridhiwani na kutetea wateja wake wengine
tusikimbilie kulaumu watu tu.Kama yeye Ridhiwani yuko convinced anahitaji security
ya uhakika kwa maisha yake sisi wengine tunaweza vipi kusema hakuna haja ya hilo??????


wanaosema Ridhiwani ni nani ni wapumbavu, hata watoto wa Obama wanapewa security...
muhimu ni kuzingatia hiyo security iko vipi, cost zake,na ni vipi haitakuwa kero kwa wengine
kwa hili aliesababisha kero sio Ridhiwani ni wamiliki wa hoteli
Mkuu unachanganya mapapai na mapera.

Kama wangenyimwa vyumba hapo malaika kwa sababu Ridhiwani tayari alikuwa kesha book room hapo,basi pengine ingemake sense.

Lakini hili la kuwafukuza,halimake sense hata kidogo,kulikuwa na emergency gani ambayo ilihalalisha kuwafukuza?Nchi si ya ufalme hii.Ni ubwanyenye tu na ganzi ndani ya ubongo inayotokana na ulevi wa madaraka,basi.

Nilisema pia kuwa katiba inawapa mwanya,na ulevi unaotokana na ubovu wa katiba ndo mambo kama haya..

Lakini wabongo wa kawaida wala hii si big deal,ndo hapo pa kushangaza.

Nawashauri waandishi waichukulie hii kama changamoto ili kujuwa mwisho wake.
 
Kama serikali inajali usalama wake kwanini asilale ikulu?? Natumain Mwanza kuna Ikulu.

Kwa utamaduni wa watoto wa rais hapa Tz ni kuwa wanapata ulinzi wa kawaida ambao hautamsumbua raia yoyote kwenye mipango yake kama ilivyo kuwa kwa watangulizi wake.

Haya ni matumizi mabaya sana ya hela ya mwananchi. Mie namshauri Ridhiwan ajipange kwani 2015 sio mbali, je ataendelea kulindwa au ndo ataingia mtaani kama sisi? Pia awe mwangalifu asiishie jela kwani jasho la mlala hoi halipotei bure.

Na pia Ridhiwan atambue kuwa yeye sio mtoto wa mfalme ni mtoto wa Kikwere!

Bye!
 
Mkuu unachanganya mapapai na mapera.

Kama wangenyimwa vyumba hapo malaika kwa sababu Ridhiwani tayari alikuwa kesha book room hapo,basi pengine ingemake sense.

Lakini hili la kuwafukuza,halimake sense hata kidogo,kulikuwa na emergency gani ambayo ilihalalisha kuwafukuza?Nchi si ya ufalme hii.Ni ubwanyenye tu na ganzi ndani ya ubongo inayotokana na ulevi wa madaraka,basi.

Nilisema pia kuwa katiba inawapa mwanya,na ulevi unaotokana na ubovu wa katiba ndo mambo kama haya..

Lakini wabongo wa kawaida wala hii si big deal,ndo hapo pa kushangaza.

Nawashauri waandishi waichukulie hii kama changamoto ili kujuwa mwisho wake.

Nakubaliana na wewe mkuu,

Katiba yetu inawafanya viongozi na watendaji wa serikali kuwa kama wapagazi au houseboys/housegirls. Kama katiba ingekuwa inaweka mipaka vizuri, sioni ni kwa jinsi gani RPC angejihangaisha na ulinzi wa kawaida wa mtoto wa rais (labda kama kuna emergency). Pia haya ndiyo yanawafanya hata wakuu wa mikoa kutoa riport ya utendaji kwa first lady na inawezekana hata Ridhiwani naye anapewa kitu kama hicho!

Hata hivyo, hawa ndugu wa viongozi wanatakiwa kutumia common sense na pia kuangalia watangulizi wao. Labda kama wana uhakika kuwa watakuwa ikulu hadi kiama....!! But mifano ya akina Gaddafi inatakiwa kuwa-alert kwamba hilo haliwezekani!
 
ni nafasi nzuri kwao kutumia kalamu zao kuiobomoa CCM NA MAGAMBA YAKE YOTE.
WAMEJUA KARAHA YA KUTUMIWA NA MAGAMBA ENZI ZA UCHAGUZI SASA WAWAELEZE WANANCHI MAOVU YA MAGAMBA
 
Haya ndio mambo yaliyomfanya Seif Gaddafi kuamini kabisa kuwa yeye naye ni mtawala kama babake na kuhamasisha wanajeshi kuwaua wananchi wake ili kumtetea babake. Ndio maana wengine tumependekeza Rais amteua Ridhiwani awe Mshauri wake wa Usalama wa Taifa.
 
Hivi hawa watetezi wa hii rotten system tuliyo nayo sasa Tanzania ni kina nani kihalisia?
 
Wana Jf

Baada ya kutoka Magu Ridhwani kikwete aliamua kuhama hoteli ya Golden Crest na Kuhamia Hoteli ya Malaika uamuzi huu umesababisha wanahabari waliokua wamefikia na kulipia Vyumba katika Hoteli hiyo kuambiwa watoke kwa ajili ya kulinda usalama wa Mtoto wa Rais.

Tukio hili Binafsi limenisikitisha Baadhi wanahabari akiwemo Mzee Teophil Makunga na wanahabari wengine ambao vyumba vyao vilikua vimelipiwa siku tatu zilizopita kuambiwa hawataruhusiwa kufikia Pale kwani Mtoto wa Rais wetu atalala hapo na kwakua atalala hapo wanatakiwa kuondoka kwa ajili ya kulinda usalama wake.

Hili limenishangaza nakujiuliza namna madaraka yanavotumiwa Vibaya,ana ulinzi wa maaskari na sasa hapa amefika RPC.

Jambo hili tujadili ndg zangu nimesikia matukio ya Arusha jinsi Dola anavyo agizwa na huyu ndg nimejionea magu aina ulinzi uliotumika mapolisi,wana usalama kama Waziri mkuu yupo eneo hilo

MwanaMfalme
mtoto wa mfalme.jpg
 
Sometimes men are the masters of their own fate...and sometimes men are the archtect of their own graves....
 
Sometimes men are the masters of their own fate...and sometimes men are the archtect of their own graves....

Hivi huwa hawajui kwamba maisha yenyewe ya duniani ni mafupi mno??? Au wanadhani kwamba wakishapata madaraka basi wanakuwa immortal???
 
Mbona Watoto wa Mwalimu walikuwa hawajikwezi kama huyu!? Kufukuza watu mahotelini eti kwa usalama wao!?
Una hakika? Wakati wa mwalimu hotel kubwa zote zilikuwa za SERIKALI kwa hiyo Usalama ulikuwa thabiti.
 
Familia ya rais ni lazima ipewe ulinzi fikilia kama kuna baya lolote likimpata member wa familia ya rais lazima rais ataathilika ktk utendaji wake wa kazi labda kama tulalamike mambo aliyotoka kufanya huko alikotoka lkn ulinzi ni lazima
Swala ni sheria inasemaje. Ulinzi kupewa mtu lazima uwe wa kisheria na msafara pia. Riz ana ubia na urais wa babake? Hii nchi ni ya kifalme? Ndio maana watu wanauliza, marais watatu waliotangulia hawakuwa na watoto? Kuna siku watalipa kwa matendo wanayoyafanya
 
Huu utaratibu ni mgeni kabisa Tanzania - wa watoto wa viongozi kujitenga na jamii.

Kikwete hajafanya vizuri katika kusimamia uchumi wa nchi hii, lakini nahofia Kikwete may be failing as well when it comes to parenting. Kwa nini amemwingiza mwanawe kwenye front line politics? Very unfortunate.
 
Huu utaratibu ni mgeni kabisa Tanzania - wa watoto wa viongozi kujitenga na jamii.

Kikwete hajafanya vizuri katika kusimamia uchumi wa nchi hii, lakini nahofia Kikwete may be failing as well when it comes to parenting. Kwa nini amemwingiza mwanawe kwenye front line politics? Very unfortunate.
Tatizo ni kichwa cha...............Mtoto wake nae ana kichwa cha ......................
 
Una hakika? Wakati wa mwalimu hotel kubwa zote zilikuwa za SERIKALI kwa hiyo Usalama ulikuwa thabiti.

Hata kama usalama hauko thabiti katika hotel hiyo, bado management ingeweza kuomba kuongezwa ulinzi hapo Malaika Hotel na hivyo huyo Ridhwan kulala hapo na hao Wahariri wakaendelea na shughuli zao kama wapangaji katika hotel hiyo bila ya kudhalilishwa.
 
Mkuu hio Hotel ndio hawajui maana ya customer care na promotion..., au waandishi cha kufanya ni kuandika kwa muda wa wiki nzima kwenye magazeti jinsi Malaika unaweza ukafukuzwa anytime ukija ugeni...

This is Bad for Business for Malaika..., na kwa mwendo huu itabidi Riz aache kutembelea mikoani sababu hizi ni disruptions. Pia inabidi washauri wake wamshauri hii kujifanya anaishi above the rest ina-backfire sana, nadhani baba yake angekuwa rais wakati anasoma angetafutiwa shule yake mwenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kuna mtu alinambia kuwa, "it is too expensive to make just one enemy, especially if it could be avoided"!!!

Huyu dogo na baba yake wanaendelea kuwatengeneza maadui kila siku....shida ni kwamba wanaanza kuwafanya watu wengine walipie gharama za matendo yao...Very pathetic!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
ngoja niwambie sometime muhusika hana makuu ila wapambe.nilisha safiri na mkuu mmoja tukalala njiani nyumba ya wageni mkuu alikuwa simple tu.alivyoandikisha jina mwenye hoteli alimpigia simu ocd hatimaye mkuu wa wilaya ukaletwa ulinzi bila mgeni kuomba wala kujua.sometime ni kujipendekeza tu kwa watu
 
Too much! Inabidi tuweke wazi mipaka ya wanafamilia wa rais wanatakiwa wapewe hadhi gani maana yake hali ya sasa haikubaliki kabisa. Kuna msemo kwa madaraka aliyonayo rais tukimpata rais kichaa tutajilaumu.
 
Back
Top Bottom