Wahariri wa Vyombo Vya Habari wafukuzwa Malaika Hotel Mwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahariri wa Vyombo Vya Habari wafukuzwa Malaika Hotel Mwanza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUA GAMBA, Oct 22, 2011.

 1. M

  MVUA GAMBA Senior Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana Jf

  Baada ya kutoka Magu Ridhwani kikwete aliamua kuhama hoteli ya Golden Crest na Kuhamia Hoteli ya Malaika uamuzi huu umesababisha wanahabari waliokua wamefikia na kulipia Vyumba katika Hoteli hiyo kuambiwa watoke kwa ajili ya kulinda usalama wa Mtoto wa Rais.

  Tukio hili Binafsi limenisikitisha Baadhi wanahabari akiwemo Mzee Teophil Makunga na wanahabari wengine ambao vyumba vyao vilikua vimelipiwa siku tatu zilizopita kuambiwa hawataruhusiwa kufikia Pale kwani Mtoto wa Rais wetu atalala hapo na kwakua atalala hapo wanatakiwa kuondoka kwa ajili ya kulinda usalama wake.

  Hili limenishangaza nakujiuliza namna madaraka yanavotumiwa Vibaya,ana ulinzi wa maaskari na sasa hapa amefika RPC.

  Jambo hili tujadili ndg zangu nimesikia matukio ya Arusha jinsi Dola anavyo agizwa na huyu ndg nimejionea magu aina ulinzi uliotumika mapolisi,wana usalama kama Waziri mkuu yupo eneo hilo

  ==============================
  Moderator's correction (info from the team in Mwanza):
  ==============================

  Mwanzo tulinyimwa vyumba kwa sababu kwamba Ridhwani Kikwete na wapambe wake wamezuia vyumba.

  Lakini baada ya uchunguzi wa Kina, Ridhwani hahusiki na alicheck-out tangu asubuhi tangu saa nne asubuhi, isipokuwa hoteli ilikosea upande wa management.

  Tunaomba ieleweke kwamba Ridhwani hahusiki bali wenye hoteli ambao ni wafanyabiashara wenye asili ya kiasia ndio waliotumia jina lake vibaya.

  Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wote.
  ==============================
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Pole zao nyingi sana kwa kudhalilishwa kiasi hicho
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Jasho la watanzania walala hoi linateketea.....yana mwisho lakini
   
 4. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ukiwa na kichwa cha nazi taabu kwelikweli kila kitu utajiamulia hivi ndivyo kodi ya watanzania inavyotumiwa vibaya
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  tatizo lako ni ulinzi wa Riziwani au ni kufukuzwa kwa wahariri wa vyombo vya habari???????

  mimi naona tatizo ni idadi ya hoteli standard hapo Mwanza...
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa uyo mtoto kikatiba tutamwita nani first Boy maana sioni provision katika katiba
  Ila sishangai kwa utajiri alionao ana maadui wengi na pia anahisi kila mtu anamuwinda
   
 7. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Wapenzi na mimi niko Mwanza, nilikua na miadi na mtu ambaye ni mhariru mzito Malaika Beach Resort, nimefika naambiwa wamenyang'anywa vyumba kupisha ugeni wa Ridhiwani Kikwete, hebu jamani nijuzeni maana hata simu ya mtu wangu sina, nimekereka sana na mimi ni mgeni hapa Mwanza. Hata hivyo mmoja wa wahudumu amenambia hata Ridhiwani mwenyewe hayuko Mwanza maana amefika leo na kuondoka maana inawezekana wapambe wake ndio wanatisha watu.
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,666
  Likes Received: 21,892
  Trophy Points: 280
  Seif al Islam bin Gaddafi. Hizo ndizo zilikuwa style zake.
   
 9. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kwani anawindwa? Mbona kina Makongoro, kina Hussein Mwinyi etc. walikuwa wanajichanganya poa tu wakati baba zao ma Rais? Hivi wanataka wakumbukweje hiifamilia, watu washangilie kwa confetti na maandamano siku wanaondoka Ikulu?
   
 10. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Hili nalo litapita
  Shaka ni kama Riz anaelewa athari ya linalopita kwa linalokuja
   
 11. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45

  Si Dodoma ni Mwanza, ila hii inaleta picha mbaya sana
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Ni Mwanza BOSS na siyo Dom...Na wanahabari inaelekea waliambiwa hivyo na Management ya Hotel kwamba mnahamishwa kwa sababu ya usalama wa Ridhwan. Tusubiri labda utawala wa Hotel hiyo wanaweza kuweka bayana nini hasa kilichojiri hadi wahariri hao kufukuzwa hotelini.
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ye nani hapa tanzania mpaka watu wafukuzwe hotelini? na huyo niliki wa hoteli anamana gani kufanya hivyo wkt watu wameshalipia vyumba vyao siku 3 zilizopita? HUU NI UPUMBAVU WA HALI YA JUU SN WA JESHI LA POLISI, HUYO RIZINYAU, NA MMILIKI WA HOTELI
   
 14. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Familia ya rais ni lazima ipewe ulinzi fikilia kama kuna baya lolote likimpata member wa familia ya rais lazima rais ataathilika ktk utendaji wake wa kazi labda kama tulalamike mambo aliyotoka kufanya huko alikotoka lkn ulinzi ni lazima
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,666
  Likes Received: 21,892
  Trophy Points: 280
  Soma uelewe wewe acha kukurupuka. Watu wanazungumzia Mwanza wewe uko Dodoma.
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nadhani familia ya rais inabidi ipewe ulinzi, kwa kungalia posts za humu jamvini tu inaonyesha kuna chuki na vitisho vya hapa na pale.
  Wengine tunadhania utani, ila kuna watu nadhani wako serious kufanya kitu mbaya.
  So I.m not suprised.
   
 17. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hii hatari sana yani mtoto wa Raisi anakua kana ndio Raisi mwenyewe,da wewe ngoja tutawatia adabu muda ukifika
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi bongo ilivyo hakuna la kushangaza.

  La kushangaza ni viongozi na hao watoto wao.Kwa kusema ukweli hakuna tofauti kabisa na hao watawala ambao wameondolewa kwa nguvu ya umma.

  Kuna kitu flani kama ganzi hivi ndani ya mbongo za watawala.There is something that just dont click once they are in power.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nao wahariri walikubali kuondoka? kama waliondoka na hawatofungua kesi ya anti-discrimination wanastahili kufukuzwa mahali popote ambapo kuna uwezekano wa Ridhiwani kupita.
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mkuu vyovyote vile lakini habari hii huwezi kumlaumu Ridhiwani...
  mwenye hoteli alikuwa na mamlaka ya kukataa ugeni wa Ridhiwani na kutetea wateja wake wengine
  tusikimbilie kulaumu watu tu.Kama yeye Ridhiwani yuko convinced anahitaji security
  ya uhakika kwa maisha yake sisi wengine tunaweza vipi kusema hakuna haja ya hilo??????

  wanaosema Ridhiwani ni nani ni wapumbavu, hata watoto wa Obama wanapewa security...
  muhimu ni kuzingatia hiyo security iko vipi, cost zake,na ni vipi haitakuwa kero kwa wengine
  kwa hili aliesababisha kero sio Ridhiwani ni wamiliki wa hoteli
   
Loading...