Wahariri na Rais Kikwete: Yametimia yaliyotabiriwa?

Huyu muhariri akiwa anaongea kwenye TV kwa ukali lakini nashangaa sana jana kapata nafasi ya kumuuliza JK swali uso kwa macho lakini kauliza swali dhaifu sana...JK sijui aliwapa nini wahariri alikuwa akicheka na wenyewe wanacheka.

Wahariri walikuwa wanauliza maswali dhaifu sana utadhani wapo kwenye kipindi cha malumbano ya hoja.
Ndiyo ujue sasa kuwa habari za Majungu hazimjengei mwanadishi ujasiri pale anapokutana na Kiongozi na hasa kiongozi ambaye unazushia uongo. Afadhali hata huyo ametapa tapa, Kubenea hata kuhema angeshindwa.
 

i)Muhariri wa Tzdaima- kuhusu swali alivyomuuliza Kikwete kuhusu Serekali kuhusika Kumdhuru dk Ulimboka lilikuwa ni la kitoto sana.

Huwa najiuliza sana. Kwanini tzdaima huwa linaandika mambo makubwa na ya kiuchokozi sana kuhusu Serekali ya JK . Lkn huwa nashangaa kila mara wakikutana uso kwa uso na JK huwa mdomo wa muhariri huyu huingia kitetemeshi . kazi wanayofanya huwa ni nyepesi sana na maswali yake hata Katibu tarafa wa CCM anaweza kuijibu tena huku akicheka. Inaonekana baadhi ya habari za TZDAIMA zinaandikwa na watu makini kama wabunge wa Chadema na muhariri hupitishiwa. kibaya zaidi ndie mwenyekiti wa jukwa la wahahariri tz


ALIULIZA HIVI JANA.
Mh kuna baadhi ya Vyombo vya habari vinadai serekali imehusika Kumteka Dk Ulimboka.

Ningalipata mimi nafasi ningaliuliza hivi.
Mh rais. hivi karibuni baadhi ya magazeti na yalimtaja mtumishi wa Ikulu (Ningalimtaja jina )ndio wahusika wa utekaji wa Dk Ulimboka. Swali. kwa kuwa Ikulu ni pahala patakatifu , Jee mh kweli mtumishi huyu alietajwa yupo kweli Ikulu? na kama yupo nini msimamo wa serekali yako kama hayupo Ikulu wala haimjui kwanini serekali imekaa kimya kukanusha habari hizo kupitia Msemaji wa Ikulu kama tulivyozoea kusikia kupitia Kurugenzi ya mawasiliano?

b)Kwanini Mh rais umeshindwa kuunda tume huru kuondoa wingu hili

Maswali yaliyoulizwa na wahariri ni maswali Pumba sana, na yalimpa wakati mwepesi Rais kuyajibu...Na aliweza kujibu vile alivyojibu kwakuwa yalikuwa maswali ya ujumla hivi (too general) .Swali Pekee kidogo ni lile lililomhusu Chenge, ambalo ni Kero ya muda mrefu iliyotaka majibu ya mwisho kabisa ili ile mada ichimbiwe kaburi.

Kuna maswali kama hilo ulilo uliza, swali kuhusu mafao ya wafanya kazi, swali kuhusu Serikali kuingilia uhuru wa habari kwa kufungia magazeti n.k.

Labda wahariri walikuwa kwenye swaumu kali...Sikuona swali la gumu na la maana pale kwakweli...Nilijuta kupoteza muda kusikiliza kipindi kile!!
 
Serikali imelifungia gazeti la MWANAHALISI. Wiki hiyo hiyo Rais Kikwete akawaalika wahariri kwenda kuongea nao Ikulu. Akawaagiza waandike maswali na kuyatuma mapema. Wakatii na kuyatuma. Orodha ya waalikwa ikachambuliwa. Ni sawa na kusema, ili uwe mhariri ni lazima ikulu ikubali kuwa wewe ndiye mhariri. Haya tuyaweke pembeni, tujikumbushe yaliyowahi au kutabiriwa/ kusemwa kuhusu waandishi wa Tanzania.

-Kwamba, ni wavivu wa kufikiri
-Kwamba, hawajui kuuliza maswali ya maana,
-Kwamba, hawajui kufanya uchunguzi na kuandika vizuri habari za uchunguzi,
-Kwamba, ni "vijibwa" vya watawala na wenye fedha,
-Kwamba, ni "makanjanja" wanaochafua tasnia ya habari, n.k.

Kwa kitendo cha wahariri kutii kwenda Ikulu na kukubali kuandaa maswali na kuyatuma mapema, wakati gazeti mojawapo limefungiwa kibabe, kimewadhalilisha sana wahariri wetu. Kimedhihirisha kwa dhati kuwa waandishi hawana umoja wala mshikamano na kwa hiyo ni ruksa kwa dola kuwafanyia itakavyo.

Hata katika nchi zilizoendelea, marais na viongozi wa nchi hizo, wakiitisha mikutano na wahariri au waandishi, huwapa uhuru wa kuulizwa maswali hata kama wanaweza kufanya mbinu ya kuwainua na kuwapa fursa ya kuuliza wale ambao hurusha "friendly fire" kwa watawala. Huu utaratibu wa wahariri wetu kukubali "kuandikiana barua za mapenzi" na rais ukome maana unaidhalilisha tasnia ya habari. Kama rais anataka maswali yaliyoandikwa, basi na yeye ajibu kwa maandishi na awatumie waliouliza.

Kukosekana kwa umoja na mshikamano miongoni mwenu, kunawafanya muishi kwa matumaini ya kuteuliwa ua kuingia katika siasa ili muendeleze michezo michafu mnayoipiga hivi sasa mkiwa mmevaa glovu. Jamani mnashindwa kumwuliza Rais, ikiwa serikali haikumteka Dr. Ulimboka kwa nini haichunguzi utekaji huo? Mnakubaliana na kujiumauma kwake kuwa "maneno yako mengi na yataendelea kuwapo"!

MMENISIKITISHA SANA.


Mwanahalisi na habari zake za kizushi halina hana ushirikiano na wenzake, hukusikia wakati akihojiwa na BBC alivyokandia vyombo vingine kuwa vinaogopa kuandika habari za alizoziita za kiuchunguzi. Wewe unafikiri kwa kitendo hicho yeye (KUBENEA) hajavidhalilisha vyombo hivyo? Walishamhamu kubenea kuwa ni feki ha ni mtu wa majungu tena majungu yenyewe anaandaliwa hana uwezo wa kuyaandaa mwenyewe.
 
Ulichotaka aulize au namna alivyo uliza,ndivyo alivyouliza.KiBANDA alifanya kazi ya kulikiza mh J.K.lNa waandish, pamoja na wahariri niliyowaona ni magwiji wa taaluma ya habari,kwa hiyo walikuwa wanasikiliza na kuchuja alichokuwa anakizungumza ambako uchambuzi wao ni endelevu.
 
Ni Mhariri gani asiyejitakia Mema aanze tangulia mabwepande, yaani wote, MaDr, Wapinzani wakifika pale ni mahali patakatifu,sio mahali km hapa jamvini maana hata jina la huyo Igho....i umeshindwa litamka sasa yeye Mhariri ulitaka atamkaje Abdul au hawawjui TISS
 
Mtoa mada kama anaanisha sifa alizotoa kuwahusu watu kama Salva Rweyemamu, Mhingo Rweyemamu, Manyerere Jackton, Charles Charles, na vijibwa wengine wanaojipendekeza kwake ili awape ukuu wa wilaya sawa lakini si waandishi wote niwajuao. Hivi unaweza kuwalinganisha waandishi nguli kama Jenerali Ulimwengu, Phil Karashani, Ahmed Rajab na wengine vijana waliochipukia na hizo sifa? Wanangu tuwatendeeni waandishi wa habari ambao naona ni bora kuliko wabunge wenu.
 
Ni kweli tuna tatizo la sisi wanahabari wa Tanzania kuandika hoja kali kwa maslahi ya taifa, lakini tunapopata fursa, huishia kuuliza maswali rahisi na ya kitoto ya kutoa jibu la ndio au hapana!.

Ile kitendo chuu cha kuitwa Ikulu, wanaona kama ni fadhila fulani, hivyo waheshimiwa wahariri wetu, wanaogopa kuuliza maswali magumu ili wasimprovoke JK!.
 
Maswali yote yanakuwa yameshatangulizwa kwake
na anakuwa ameshatoa msimamo wake kwamba ulizeni hivi,
vinenevyo ni nidhamu ya woga tu.
 
Hivi waliitwa Ikulu kufanya nini si afadhali kutokwenda kuliko uende halafu ushindwe kuuliza swali la kuondoa dukuduku ulizo nazo?
IKULU ni mahali patakatifu in the sense kwamba haki na ukweli unatakiwa utawale short of that hilo neo patakatifu halina maana!
 
Maswali yote yanakuwa yameshatangulizwa kwake
na anakuwa ameshatoa msimamo wake kwamba ulizeni hivi,
vinenevyo ni nidhamu ya woga tu.

Naona utaki kukubali ukweli unaamua kutumia akili yako unataka kutuaminisha kuwa yale maswali walikuwa wanauliza Wahariri walipangiwa na rais...wote tumeona kwenye TV baada ya kumaliza hotuba yake akatoa nafasi kwa Wahariri kuuliza maswali, maswali tulisikia ni maswali dhaifu kabisa wale Whariri ambao magazeti yao ndio wanaongoza kuichana serikali hakuna walichofanya zaidi ya kuchekacheka.
 
Naona utaki kukubali ukweli unaamua kutumia akili yako unataka kutuaminisha kuwa yale maswali walikuwa wanauliza Wahariri walipangiwa na rais...wote tumeona kwenye TV baada ya kumaliza hotuba yake akatoa nafasi kwa Wahariri kuuliza maswali, maswali tulisikia ni maswali dhaifu kabisa wale Whariri ambao magazeti yao ndio wanaongoza kuichana serikali hakuna walichofanya zaidi ya kuchekacheka.
Yalipangwa, usitudanganye hapa. wangemuita kubenea na wanaofanana nae. Mambo ya kupanga panga tu. Kuwapa watu vimishiko, kama huyu jamaa ambeye yuko JF (Ritz).
 
Wahariri pamja na mtoa mada mmeshindwa kumuuliza rais swali kuhusu Rama au jack zoka kweli?

Mtoa mada ume act kama mhariri lakini umeogopa kumtaja, sasa ulitegemea mhariri aliye kuwa karibu na rais amtaje jack zoka au Rama?

Tanzania ni nchi ya wanafiki kila sehemu kuna nuka unafiki tu! Walishindwa kuuliza swala la uhuru wa vyombo vya habari alaf wanatoka hapo wanapinga kufungiwa kwa mwana halisi huu ni unafiki.

kuchekacheka tu kinafiki ndio kazi iliyo wapeleka pale siku hiyo.
Kwanza tunatakiwa tutibu ugonjwa wa unafiki ndio tuendelee na ukombozi.
 
Mwanahalisi na habari zake za kizushi halina hana ushirikiano na wenzake, hukusikia wakati akihojiwa na BBC alivyokandia vyombo vingine kuwa vinaogopa kuandika habari za alizoziita za kiuchunguzi. Wewe unafikiri kwa kitendo hicho yeye (KUBENEA) hajavidhalilisha vyombo hivyo? Walishamhamu kubenea kuwa ni feki ha ni mtu wa majungu tena majungu yenyewe anaandaliwa hana uwezo wa kuyaandaa mwenyewe.
Sema usemalo, utawapata waliwao, lakini heshima ya Gazeti la Mwanahalisi iko palepale. Liko juu sana. Labda zungumzia magazeti ya udaku uliozoea kusoma.
 
Wahariri pamja na mtoa mada mmeshindwa kumuuliza rais swali kuhusu Rama au jack zoka kweli?

Mtoa mada ume act kama mhariri lakini umeogopa kumtaja, sasa ulitegemea mhariri aliye kuwa karibu na rais amtaje jack zoka au Rama?

Tanzania ni nchi ya wanafiki kila sehemu kuna nuka unafiki tu! Walishindwa kuuliza swala la uhuru wa vyombo vya habari alaf wanatoka hapo wanapinga kufungiwa kwa mwana halisi huu ni unafiki.

kuchekacheka tu kinafiki ndio kazi iliyo wapeleka pale siku hiyo.
Kwanza tunatakiwa tutibu ugonjwa wa unafiki ndio tuendelee na ukombozi.
maneno haya ndio ukombozi wa watz na wala sio vyama vya siasa.
 
Hujaeleweka unachezea timu gani Mkuu..

Kama wewe ulikuwepo kilikushinda nini kuuliza huo ujinga wako? Na kwa hotuba ya kizushi kama ile ya jana ulitegemea Dhaifu angejibu nini zaidi ya utumbo alioutoa kwa maswali mengine aliyoulizwa? Wacha kujifanya wewe mjuaji, wewe ni kanjanja wa kutupwa! Swali uliloliweka hapo kama mbadala ni la kijinga zaidi!
 
alivyokuwa anajibu nilijua moja kwa moja aliandaliwa maswali before especially kwenye swali la rada na la umeme alipoanza kutaja vile vituo na megawatts zinazozalishwa...huyu kilaza ni dikteta kama idd amin asiyetaka kuonekana hajui kitu...angekuwa na uwezo angejipa u-profesa
 
Back
Top Bottom