Wahariri na Rais Kikwete: Yametimia yaliyotabiriwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahariri na Rais Kikwete: Yametimia yaliyotabiriwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Baija Bolobi, Aug 2, 2012.

 1. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 930
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 180
  Serikali imelifungia gazeti la MWANAHALISI. Wiki hiyo hiyo Rais Kikwete akawaalika wahariri kwenda kuongea nao Ikulu. Akawaagiza waandike maswali na kuyatuma mapema. Wakatii na kuyatuma. Orodha ya waalikwa ikachambuliwa. Ni sawa na kusema, ili uwe mhariri ni lazima ikulu ikubali kuwa wewe ndiye mhariri. Haya tuyaweke pembeni, tujikumbushe yaliyowahi au kutabiriwa/ kusemwa kuhusu waandishi wa Tanzania.

  -Kwamba, ni wavivu wa kufikiri
  -Kwamba, hawajui kuuliza maswali ya maana,
  -Kwamba, hawajui kufanya uchunguzi na kuandika vizuri habari za uchunguzi,
  -Kwamba, ni "vijibwa" vya watawala na wenye fedha,
  -Kwamba, ni "makanjanja" wanaochafua tasnia ya habari, n.k.

  Kwa kitendo cha wahariri kutii kwenda Ikulu na kukubali kuandaa maswali na kuyatuma mapema, wakati gazeti mojawapo limefungiwa kibabe, kimewadhalilisha sana wahariri wetu. Kimedhihirisha kwa dhati kuwa waandishi hawana umoja wala mshikamano na kwa hiyo ni ruksa kwa dola kuwafanyia itakavyo.

  Hata katika nchi zilizoendelea, marais na viongozi wa nchi hizo, wakiitisha mikutano na wahariri au waandishi, huwapa uhuru wa kuulizwa maswali hata kama wanaweza kufanya mbinu ya kuwainua na kuwapa fursa ya kuuliza wale ambao hurusha "friendly fire" kwa watawala. Huu utaratibu wa wahariri wetu kukubali "kuandikiana barua za mapenzi" na rais ukome maana unaidhalilisha tasnia ya habari. Kama rais anataka maswali yaliyoandikwa, basi na yeye ajibu kwa maandishi na awatumie waliouliza.

  Kukosekana kwa umoja na mshikamano miongoni mwenu, kunawafanya muishi kwa matumaini ya kuteuliwa ua kuingia katika siasa ili muendeleze michezo michafu mnayoipiga hivi sasa mkiwa mmevaa glovu. Jamani mnashindwa kumwuliza Rais, ikiwa serikali haikumteka Dr. Ulimboka kwa nini haichunguzi utekaji huo? Mnakubaliana na kujiumauma kwake kuwa "maneno yako mengi na yataendelea kuwapo"!

  MMENISIKITISHA SANA.

   
 2. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Waziri Mkuu MSTAAFU Frederick Sumaye alionya katika mbio za kusaka Urais nwakati huo kwamba kuna mtu alikuwa akitumia kalamu(soma WAHARIRI na Waandishi wa HABARI) kuwachafua wagombea wengine na kwamba mtu huyo akishaingia IKULU atatumia risasi!Haya nayo yametimia
  Pia sitasahau KATUNI iliyowahi kuchapishwa kwenye The East African ikiwaonesha waandishi wa habari wakilamba soli ya viatu vya bwana mkubwa le president.Hii nayo imetimia waziwazi!
  Wahariri husika mtajisafisha vipi?
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hatua ya serikali dhidi ya gazeti la 'MwanaHalisi' ni dalili tosha ya mambo ya hatari mno yanayotarajiwa kutufika kama jamii ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutetea DHULUMA nchini.

  Hivyo, ni vema sote tukaelewa kwamba hadi sasa Uhuru wa Maoni na haki za binadamu nchini sasa ziko mashakani. Hata hivyo kamwe hatutokaa kimya na kuyaachia yaendelee kivile. Kila mmoja tuanze kuchukua hatua katika vijikundi vyetu na kusema HAPANA!!

  Kubenea anayo haki ya kutoa maoni na gazeti lake pia. Endapo serikali haijaridhika na jambo ni juu yao kwenda mahakamani ila hili la kufungiana ni mambo ya kizamani kweli kweli.
   
 4. koo

  koo JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yana mwisho yote hayo mungu pamoja na taifa letu naamini tutafika tunapopataka siku sio nyingi wote walio watumwa wa wenye fedha watafunguliwa na ubora wa fani zao utakuwa chachu ya maendeleo.
   
 5. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama waliweza kukubali kuitwa hotelini na mwarabu wa Dowans na kukatazwa kumpiga picha ili tu wapate posho ya laki tano...sishangai kwa hili!

  Waandishi wa habari wa bongo wanaendekeza mno njaa hadi inatia aibu!
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Heeee,,,,kumbe yale maswali yalitumwa b4????????astaghfilullah
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  waandishi watanzania mmeaibishwa sana na hao ******* mliowatuma ambao mnawaita wahariri .....hapakuwa na cha maana cha kuonesha kwenye mkutano wa waaandishi wa dar.....ni kama vile wahariri mmekuwa reduced to "wazee wa mkoa wa dar es salaam"
  kuanzia leo wahariri wataitwa jina jipya " wazee wa mkoa wa dar es salaam"
   
 8. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Walifuata wali. wanajua ukiandika kuikosoa serikali, siku nyingine huitwi, lakini pia, ukilamba viatu vya mkubwa, iko siku atakuteua kuwa Mkuu wa Wilaya, nani hataki ukuu wa Wilaya????????
   
 9. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  sawa kabisa wana njaa sana jamaa issue ya kufungiwa mwanahalisi wangekaa kimya na wangesusa kwenda kabisa
   
 10. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawana maana.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Ditto.

  Kukubali kupeleka maswali in writing ni kukubali ukandamizaji wa Ikulu.
   
 12. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Inasikitisha, lakini ndiyo ukweli wenyewe; waandishi na wahariri wa magazeti ya Tanzania wameisaliti kabisa fani yao, hawana umoja kama waalimu na madaktari na wameiaibisha kabisa fani yao kwa kuitikia wito wa kwenda kuhongwa "chai na maandazi' pale magogoni. Huu ndiyo wakati ambao wahariri wangepeleka ujumbe "Mzito" kwa wababe wa ikulu, madikteta na wakoloni mambo leo kwa kugomea kwenda kule , isipokuwa mavuvuzela yao tu; yaani Daily News, Uhuru, na vijigazeti walivyovianzisha kuupotosha umma. Kususia kungetuma ujumbe kwamba vitendo vyao madikteta hawa wa magogoni havikubaliki wala havivumiliki.
   
 13. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Jamani nani asiyetaka ukuu wa wilaya. Ni walimu wangapi wamechaguliwa kuwa wakuu wa wilaya toka shule za kata? lazima wajikombe, sioni ajabu kuwaita na wakashindwa kumuuliza maswali ya maana. Kwanza walikuwa wanatetemeka!
   
 14. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Duh kama hii habari ni ya kweli basi kazi ipo,
  Nilishangaa sana tangu lini kikwete ajibu maswali ya papo kwa papo?
  pamoja na yote majibu ya EPA aliyoyaaandaa bado hayaridhishi, sitaki kuamini kuwa jk hapa ndo mwisho wake wa kudanganya kwenye epa
   
 15. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hizi ndizo siasa za madikteta, mafashisti na wakoloni CCM za "Divide and rule" baadhi ya waliohudhuria hapo utakuta wakizawadiwa u DC na hata u RC! Shame on them all!
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  i)Muhariri wa Tzdaima- kuhusu swali alivyomuuliza Kikwete kuhusu Serekali kuhusika Kumdhuru dk Ulimboka lilikuwa ni la kitoto sana.

  ALIULIZA HIVI.
  Mh kuna baadhi ya Vyombo vya habari vinadai serekali imehusika
  Ningalipata mimi nafasi ningaliuliza hivi.
  Mh rais. hivi karibuni baadhi ya magazeti na yalimtaja mtumishi wa Ikulu (Ningalimtaja jina )ndio wahusika wa utekaji wa Dk Ulimboka. Swali. kwa kuwa Ikulu ni pahala patakatifu , Jee mh kweli mtumishi huyu alietajwa yupo kweli Ikulu? na kama yupo nini msimamo wa serekali yako kama hayupo Ikulu wala haimjui kwanini serekali imekaa kimya kukanusha habari hizo kupitia Msemaji wa Ikulu kama tulivyozoea kusikia kupitia Kurugenzi ya mawasiliano?

  b)Kwanini Mh rais umeshindwa kuunda tume huru kuondoa wingu hili
   
 17. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mbona hata wewe umeshindwa kumtaja?
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ndio maana BWM anawaita makanjanja woote waaandishi wa Tanzania!anawakwepa sana maana anasema wavivu kujisomea!!
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  i)Muhariri wa Tzdaima- kuhusu swali alivyomuuliza Kikwete kuhusu Serekali kuhusika Kumdhuru dk Ulimboka lilikuwa ni la kitoto sana.

  Huwa najiuliza sana. Kwanini tzdaima huwa linaandika mambo makubwa na ya kiuchokozi sana kuhusu Serekali ya JK . Lkn huwa nashangaa kila mara wakikutana uso kwa uso na JK huwa mdomo wa muhariri huyu huingia kitetemeshi . kazi wanayofanya huwa ni nyepesi sana na maswali yake hata Katibu tarafa wa CCM anaweza kuijibu tena huku akicheka. Inaonekana baadhi ya habari za TZDAIMA zinaandikwa na watu makini kama wabunge wa Chadema na muhariri hupitishiwa. kibaya zaidi ndie mwenyekiti wa jukwa la wahahariri tz


  ALIULIZA HIVI JANA.
  Mh kuna baadhi ya Vyombo vya habari vinadai serekali imehusika Kumteka Dk Ulimboka.

  Ningalipata mimi nafasi ningaliuliza hivi.
  Mh rais. hivi karibuni baadhi ya magazeti na yalimtaja mtumishi wa Ikulu (Ningalimtaja jina )ndio wahusika wa utekaji wa Dk Ulimboka. Swali. kwa kuwa Ikulu ni pahala patakatifu , Jee mh kweli mtumishi huyu alietajwa yupo kweli Ikulu? na kama yupo nini msimamo wa serekali yako kama hayupo Ikulu wala haimjui kwanini serekali imekaa kimya kukanusha habari hizo kupitia Msemaji wa Ikulu kama tulivyozoea kusikia kupitia Kurugenzi ya mawasiliano?

  b)Kwanini Mh rais umeshindwa kuunda tume huru kuondoa wingu hili
   
 20. V

  VUZOMUNDO JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 315
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Ni kweli wengi ni wanafiki walikuwa wanachekacheka! sijui walikuwa wanafikiri atawatangazia kuwateua baadhi yao kuwa wakuu wa wilaya,maana huelewi unakuta mtu an confidence za kuandika makala za kukosoa serikali na mkuu wa nchi akifika mbele yake anshindwa kuuliza maswali ya kumeweka mkuu wa nchi akione kile kiti ni cha moto!
   
Loading...