Wahariri majira na nipashe mnatumiwa na wanasiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahariri majira na nipashe mnatumiwa na wanasiasa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MADORO, Jan 14, 2012.

 1. M

  MADORO Senior Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakaazi wa Singida tulitoa tuhuma nzito dhidi ya Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Ndugu Lazaro Nyalandu. Kuwa Nyalandu aliwachukua wadogo zetu, watoto wetu kuwapeleka Arusha kukutana na wafadhili kutoka Marekani. Watoto wetu walichukuliwa wakalala shule ya sekondari inaitwa Nkwaranga, asubuhi yake walionana na wale wazungu Arumeru Lodge. Wakaimba, wakacheza, wakasoma risala kushukuru kuwapata wafadhili. Barua za kusafirisha watoto wale toka Singida hadi Arusha, yaani vibali vilivyotolewa na Afisa Elimu wa Mkoa Yusufu Kipengele, tunavyo.

  Barua (memo) toka kwa Katibu Tawala Rehema Vyas kwenda kwa Waalimu kuwambia waandike barua kuomba ruhusa watoto waende Arusha tunayo. Orodha ya majina ya watoto walioenda kudhalilishwa na Nyalandu tunayo, watoto hao waliofanyiwa unyama huo tupo nao ni ndugu zetu, wadogo zetu jirani zetu mbaya zaidi Singida ni kwetu. Tunayosema hatusingizii mtu, hatuchafui mtu ila tunalaani tabia hiyo. Inakuwaje ninyi mnaandika hadithi za kumsafisha mtu kwa kashfa hii.

  Kwanza hamtutendei haki sisi ambao ndio waathirika wa tukio hilo, lakini pili mnadhalilisha taaluma yenu, hata hivyo mnatushawishi tuungane kumkataa Mbunge wetu pamoja na magazeti yenu kwa kuwa ni wakala wa kutuangamiza badala ya kutumika vizuri kitaaluma. Mwandishi anayekuja na Naibu waziri kwa siku moja toka Dar na kurudi asubuhi je ana uwezo wa kuelewa hayo zaidi ya sisi tunaoathirika na hali halisi? Yaelekea hata waandishi wenu mnawawekea maneno yasiyo ya kweli ili muweze kumpendeza huyo Naibu waziri.

  Ni aibu...... endeleeni kutumika kuangamiza nchi. Fikirini kuwa watoto wenu ndo wangeonyeshwa kuwa yatima, masikini, wakachezeshwa ngoma, hela zikatolewa jamaa katia ndani, akaanza kutamba nazo mtaani na watoto wakafukuzwa shule.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Majira ni gazeti la hovyo kabisa.Fuatilia kila siku habari zake utashangaa
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,500
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  hii issue haipewi uzito lakini ni kashfa nzito! Hv hatuna wanahabari wa uchunguzi ili ukweli uanikwe wazi? The Romantic umesikia hili mkuu ?
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,500
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Mwenye gazeti alikufa nalo mkuu!
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hii habari umepewa na nani kamanda?hii ni vita na watu wako vitani,lazima tuwe makini,kwanini huu mti unapopolewa zaidi,kuna nini hapa kimejificha?mti huu una nini,mbona iko miti mingi haipopolewi kuna nini hapa?
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  huyu nyalandu si yule aliyekuwa kibaraka wa fisadi mama mkapa
   
Loading...