Wahanga wenzangu, njoeni tuilaumu Serikali

Mkuu katika kipindi hiki unachopitia maisha ya ki 'jehnamu' em jaribu kujishughulisha na kazi ndogo ndogo au biashara ndogo wakati ukiwa unasubiri kazi ya ndoto yako.

Kumbuka cheti chako cha bachelor hakiwezi kulipa bills zako while you are unemployed.

Siku yako ipo tu..
Najua, ila ujue huwa kuna safari ndefu sana kufikia "mwanzo"
 
Sasa hapo unapopaona pagumu ndipo suluhisho lilipo.

Hakuna mtu atakufuata kukuuliza una skills gani kisha akupe kazi.

Lazima kuumiza kichwa.

Kwa mfano andaa mada kadhaa kuhusu ujuzi fulani unao uelewa kisha toa Elimu kuhusu ujuzi huo hata hapa Jf kisha uone matokeo yake ndani ya miezi mitatu tu mfululizo.

Watu wanatafuta wenye skills, ila wenye skills hawajui njia gani za kukutana na watu sahihi.
Umeshawahi kupitia nyuzi zangu?
 
Habari za wikiend

Naomba nianze.

Zamani nilikuwa nikiamini kadir8 ninavyozidisha juhudi kunoa ubongo wangu, kuelewa mambo kwa haraka zaidi, kupata stadi nyingi zaidi ndio nazidi kujiwekea unafuu wa maisha hapo baadae.

Sasa imekuwa kinyume, habari hiyo ilikuwa zamani, hivi sasa mambo ni tofauti.

Kuna wakati huwa najiuliza huenda ni kutokana na mifumo yetu ya elimu, au mfumo mama wa jamii. Sijaelewa bado.

Napiga taswira ya matokeo ya juhudi za kila aliyejituma katika taaluma hapo zamani naishiwa nguvu.

Ngoja niwe case study.
Nikiwa shule nilikuwa nikijiona mbali sana, sio utani nilifikiri mimi ni mtu ambaye ningetoboa mapema mno.

Mimi sikuwa mtu wa kujifunza jambo mara mbili. Na kila kitu nilikuwa nikifanya vizuri Kwa ustadi wa hali ya juu.
Nilijifunza stadi mbali mbali nikawa nafikiri zitanikwamua.

Kuna zile clubs za shule za masomo, elimu ya jinsia na mahusiano pamoja na zile za mazingira. Zote nilikuwa naomb2a kuwa kiongozi. Nikikuwa na ushawishi mkubwa, nilikuwa ni mfano wa mwanagunzi hodari sana.

Kama nikikuambia baada ya chuo kikuu naishije utashangazwa.

Kuna wakati najiuliza maisha yako mfumo wa "kisengelenyuma" najutia skills zote nilizonazo, naumizwa na muda niliotumia kulala macho nikisoma, nakumbuka starehe nilizozikosa nikiweka mbele masomo na taaluma.

Wanasena elimu ni amali isiyochuja thamani. Ila tulijifunza pia kuwa muda ndio kipimo na usahihi.

Uzi tayari, karibuni wahanga wenzangu tuilaumu serikali
Tupo wengi,ingawa mimi nimeshajua cha kufanya.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Niibie siri.
Huku mtaani sio pazuri hata kidogo
Mchezo sijausoma
Angalia uwezo wa asili ambao Mungu kakuumbia(Vipaji). Namaanisha vitu ambavyo ukivifanya unavifanya kwa ubora wa kipekee na unafurahia kufanya(Hapa kuna njia kama 7 hivi za kukusaidia kugundua Vipaji vyako). Orodhesha vyote. Kisha weka vipaumbele katika kuviboresha. Halafu andaa mkakati wa kuviuza.

VIPAJI VYAKO NDIO BIASHARA YAKO BORA KABISA CHINI YA JUA. KAZI YA MUNGU HAIJAWAHI KUWA NA MAKOSA. ALIPOAMUA UJE DUNIANI,ALIANDAA NA NAMNA BORA YA WEWE KUUFURAHIA UWEPO WAKO. KABLA HAKUKUUMBIA MAPAFU,ALIUMBA KWANZA OXYGEN.

Nakuelewa vzr kabisa.

Nimeshapitia hapo tayari. Ila kumbe mfumo mbovu hauko serikalini tu. Hata mtaani pabovu pia, mtaa unahitaji dhamana.

Ukipitia uzi huu nikiowahi kuuandika

Utagundua kuwa mbali na kada nilizosomea, nilirudi mtaani nikatafuta vitu nilivyovipenda, muda na gharama vikatumika mpaka nikawa na stadi tayari. Ila bado. Hali haijaimarika.

Amini kwamba uthubutu ninao ila nchi hii ina vigezo tofauti vinavyotazamwa
 
Nikishajifunza vitu hivyo vitanidai kianzio kama mtaji. Mfumo haukutuandaa, wala haukutudhamini
Usiwe adui na kikwazo wa maisha yako mwenyewe. Anza na ulicho nacho.Ulicho nacho ndicho kitakacholeta pesa na zaidi sana kitawavuta watu sahihi wa kukushika mkono. Sikwambii maneno matupu. Unayoyapitia,nimeyapitia pia.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom