Wahanga wa Mafuriko wafukuzwa kambini na RC

Mi ndo nilikuwa narudisha vyombo kumalizia kodi yangu ndo maana hapa jf mnanipata kimachale leo usiku mvua isipo nyesha hawa watabili tuwaeleweje?
 
Hivi huyu RC kayasema haya akiwa na akili zake timamu; au alikuwa amelewa??Watu bado wanaomboleza; yeye analeta lugha ya kuwatusi, badala ya kuwafariji.Kwa nchi za wenzetu hii ilikuwa tosha kufukuzwa kazi mara moja.

Viongozi wa nchi hii wanajiona kama miungu.. Ndiyo maana wengine wameendelea na mapumziko yao bila kujali kwamba kuna watu wengi sana wameathiriwa na haya mafuriko.

Mbaya zaidi wanazidisha kejeli....Kama hizo za kuwaambia kuwa watawapa viwanja tu na kuwahamisha. Hakuna anayesumbua kichwa chake kuhakikisha hawa watanzania wenzetu wanapata makazi ya maana!
 
Mi ndo nilikuwa narudisha vyombo kumalizia kodi yangu ndo maana hapa jf mnanipata kimachale leo usiku mvua isipo nyesha hawa watabili tuwaeleweje?

Labda walitaka watu waendelee kubaki kwenye makambi ili misaada ya kukwapua iongezeke!
 
Kwa kadri ya matangazo ya TBC1 saa 2 usiku, RC wa Dar amewapa week moja wahanga wa mafuriko ambao ni wapangaji waliohifadhiwa kwenye makambi mbali mbali, waondoke wakatafute nyumba nyingine. Kwa maoni yake, serikali haina haja ya kuendelea kuwahifadhi watu hawa!

My take,

Kama wameathirika na mafuriko na kupoteza mali zao, watawezaje kupanga nyumba mpya???

Ndiyo swali la kujiuliza!
Ni kama vile wanafikiria kuwa hawa waathirika wana pesa imekaa tu haina kazi.
Watu hawa wametumia akiba zao kujenga makazi kwa sababu serikali haijaweza kuwa na mpango kabambe kuwapa wananchi maskini makazi yenye staha.Kukosekana huku kukapelekea wananchi 'kuvunja"sheria kwa kujenga sehemu zisizoruhusiwa na serikal hiyo hiyo ikawaangalia wakijenga, wakamalIza na kuhamia bila kuwafanya kitu!
KWELI ng'ombe wa maskini hazai!
 
Watanzania wenzangu, hii ndiyo CCM tuliyoichagua wenyewe! Baada ya uchaguzi kwisha haikumbuki tena wanyonge. Wamesahau jinsi walivyokuwa wakitupigia magaoti kutuomba kura. Sasa wametugeuka na hawataki kutuona hasa wakati huu tukiwa kwenye shida. Wakati ule wa uchaguzi tulifikiria kuwa ni wenzetu ambao wangetujali, tukacheka nao huku tukiwakebehi wapinzani na hatimaye tukawapa kura zetu, walahi hatukujua kuwa tulikuwa tukicheka na nyani! Nchi inauzwa, viongozi wanajilimbikizia mali, wezi wanatukuzwa na kutunzwa, wenye kashfa, mfano genge la akina Luhanjo, Jairo na wengine bado wanakula kuku ikulu kana kwamba hakuna kuna kibaya walichofanya kwa taifa. Hata uteuzi wa mabalozi umekwenda kwa uswahiba, wale tuliowakataa kwenye kura zetu kwa sababu hawafai, bado wanaendelea kupiganiwa na mkulu. Kinyume chacke ni wanyonge kukandamizwa, wanafunzi wananyimwa mikopo, tukilalamika tunapigwa na polisi, mahakamani wanyonge ndo anayechukuwa hukumu za mvua, watoto wa wanyonge mashuleni hawana madawati, waliomaliza vyuo vikuu hawana elimu, waliopatwa na majanga kama haya ya mafuriko wanafukuzwa kambini n.k.Sasa wanyonge tuache kulalamika, tujipange upya 2015 watakapokuja tena kutupiga magoti kuomba kura zetu. Kuna mnyonge gani atakayecheka na nyani tena 2015? Mimi hapana.

Ccm ni noma! hawafai hata kwa kulumagia.
 
Kipindi hii hawajapata "chochote kitu" kwenye misaada maana haipitii mikononi mwao kwa asilimia kubwa. Sasa hasira ndio kuwaondoa chap.

Jiulize mbona wasiwatimue wakimbizi walokaa for ages? Ni kamradi kao kula misaada
 
Hawakuwapigia magoti kuomba kura waliwapa tshirt, kanga na pilau nanyi mkawapa kura na 2015 watawapa pia nanyi mtatatoa kura mpaka mje mpate kujithamini na kujua kuchagua viongozi bora mtakuwa mmeumia sana
 
Kwa kadri ya matangazo ya TBC1 saa 2 usiku, RC wa Dar amewapa week moja wahanga wa mafuriko ambao ni wapangaji waliohifadhiwa kwenye makambi mbali mbali, waondoke wakatafute nyumba nyingine. Kwa maoni yake, serikali haina haja ya kuendelea kuwahifadhi watu hawa!

My take,

Kama wameathirika na mafuriko na kupoteza mali zao, watawezaje kupanga nyumba mpya???

Vile viwanja 20,000+ visha yeyuka au visha jaa?
 
DarkCity,
Habari nayoipata ni kwamba RC amewaambia waondoke ktk maeneo ya mafuriko na sio sehemu walizohifadhiwa... Ila inasikitisha tu kwamba kambi nyingine zimewekwa sehemu zilezile zenye mafuriko...
 
ivi wandugu,tv zenu zina makengeza au ni macho yenu hayaoni sawasawa.mbona tafsiri zenu za mambo zimekaa kizushi zushi na kinyume nyume?au ndo kazi ya chuki binafsi.kwa macho yng na maskio nimemskia mkuu wa mkoa kasema tayari kuna viwanja mia 7 kwa ajili ya waathirika wenye nyumba na wapangaj watafTe nyumba zingine govt itawasaidia laki 5 each 4 kodi.andikeni taRifa Sahh watu wajue uhaliSia wa mambo jama.
 
Nina wasiwasi anatumia staili ya U-RC wa LINDI hapa DSM,
"
if the only tool you have is a hammer then you will be tempted to see every problem as a NAIL"
 
Ndiyo swali la kujiuliza!
Ni kama vile wanafikiria kuwa hawa waathirika wana pesa imekaa tu haina kazi.
Watu hawa wametumia akiba zao kujenga makazi kwa sababu serikali haijaweza kuwa na mpango kabambe kuwapa wananchi maskini makazi yenye staha.Kukosekana huku kukapelekea wananchi 'kuvunja"sheria kwa kujenga sehemu zisizoruhusiwa na serikal hiyo hiyo ikawaangalia wakijenga, wakamalIza na kuhamia bila kuwafanya kitu!
KWELI ng'ombe wa maskini hazai!

Tatizo kubwa ni viongozi wetu wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao na pale madhara yanapojitokeza, wanaanza kukwepa kuwajibika. Pamoja na hilo jukumu lao kwa mujibu wa kazi yao, hawa viongozi/watawala wanawajibika pia kutenda utu. Jambo la kusikitisha ni kitendo chao cha kukosa ubinadamu kwa wenzao ambao wamepata matatizo makubwa kiasi hicho!!

Maneno kama hayo ya RC, hakustahili kuwambia watu ambao wengine wamepoteza ndugu zao hata wk 2 hazijapita!!
 
Kipindi hii hawajapata "chochote kitu" kwenye misaada maana haipitii mikononi mwao kwa asilimia kubwa. Sasa hasira ndio kuwaondoa chap.

Jiulize mbona wasiwatimue wakimbizi walokaa for ages? Ni kamradi kao kula misaada

ndivyo yalivyo!...
 
DarkCity,
Habari nayoipata ni kwamba RC amewaambia waondoke ktk maeneo ya mafuriko na sio sehemu walizohifadhiwa... Ila inasikitisha tu kwamba kambi nyingine zimewekwa sehemu zilezile zenye mafuriko...

Hapana Mkuu,

Nimemskia RC akisema tena kwa msisitizo kwamba wale ambao walikuwa wapangaji wakatafute nyumba nyingine. Tena akakemea kuwa amesikia wengine wakidai kwamba bado kodi yao ilikuwa haijaisha na kwamba serikali haitavumilia kauli za namna hiyo. Na ndio akasema kuwa anawapa week moja waondoke makambini wakatafute nyumba nyingine za kupanga.

I stand to be corrected ila ndivyo nilivyosikia na kumwelewa RC wa Dar!
 
Duh!!! hapa mtu unaweza kukata tamaa ya maisha kabisa. Mwenyezi Mungu awanusuru.
 
ivi wandugu,tv zenu zina makengeza au ni macho yenu hayaoni sawasawa.mbona tafsiri zenu za mambo zimekaa kizushi zushi na kinyume nyume?au ndo kazi ya chuki binafsi.kwa macho yng na maskio nimemskia mkuu wa mkoa kasema tayari kuna viwanja mia 7 kwa ajili ya waathirika wenye nyumba na wapangaj watafTe nyumba zingine govt itawasaidia laki 5 each 4 kodi.andikeni taRifa Sahh watu wajue uhaliSia wa mambo jama.

Samahani Mkuu,

Nimemwona RC kwenye TBC1, ila sijasikia akitamka lolote kuhusu serikali kuwalipia wapangaji kodi. Kama una taarifa kamili naomba uiweke. Ila nimeandika kile ambacho nimeona na sina sababu ya kudramatize suala nyeti kama hili!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapana Mkuu,

Nimemskia RC akisema tena kwa msisitizo kwamba wale ambao walikuwa wapangaji wakatafute nyumba nyingine. Tena akakemea kuwa amesikia wengine wakidai kwamba bado kodi yao ilikuwa haijaisha na kwamba serikali haitavumilia kauli za namna hiyo. Na ndio akasema kuwa anawapa week moja waondoke makambini wakatafute nyumba nyingine za kupanga.

I stand to be corrected ila ndivyo nilivyosikia na kumwelewa RC wa Dar!
Sasa mkuu wangu mbona unajichanganya... Waliohifadhiwa ktk kambi itakuwaje walipe kodi..Hii ina maana RC anazungumzia wale waliokuwa wakiishi Jangwani kabla ya mafuriko walikuwa wamepanga nyumba zile na mafuriko yalipokwsha walirudi ktk maeneo hayo kinyume wakidai hawana pa kwenda, wengine wamelipa kodi na kadhalika..

Hawa ndio wanaozungumziwa sidhani kama ni wale waliohifadhiwa ktk kambi maana hawalipi kodi hawa watu. Na kama kweli inahusiana na hawa watu wa Jangwani na Kigogo maeneo hatarishi sidhani kama tunatakiwa kuwapa support hata kidogo isipokuwa kuisisitiza serikali iwatafutie mahala pa kuishi kwa muda wakati mipango ikifanyika...
 
Sasa mkuu wangu mbona unajichanganya... Waliohifadhiwa ktk kambi itakuwaje walipe kodi..Hii ina maana RC anazungumzia wale waliokuwa wakiishi Jangwani kabla ya mafuriko walikuwa wamepanga nyumba zile na mafuriko yalipokwsha walirudi ktk maeneo hayo kinyume wakidai hawana pa kwenda, wengine wamelipa kodi na kadhalika..

Hawa ndio wanaozungumziwa sidhani kaa ni wale waliohifadhiwa ktk kambi maana hawalipi kodi hawa watu. Na kama kweli inahusiana na hawa watu wa Jangwani na Kigogo maneneo hatarishi ktk maisha sidhani kaa tunatakiwa kuwapa support hata kidogo isipokuwa kuisisitiza serikali iwatafutie mahala pa kuishi kwa muda wakati mipango ikifanyika...

Sina hakika kama kuna mahali nimejichanganya au kuongelea kitu ambacho kimekaa ndivyo sivyo.

Nimeelewa kuwa kati watu ambao wametoka katika maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko, wapo ambao walikuwa wanamiliki nyumba na kuna wale ambao walikuwa wapangaji. Na wote hawa wamepewa hifadhi kwenye makambi. Kwa maelezo yake, RC aliwalenga wale ambao walikuwa wapangaji. Ikiwa na maana kwamba waliokuwa wapangaji hawatapewa viwanja. Badala yake wakatafute nyumba nyingine wapange. Na hiyo process waikamilishe ndani ya week moja ili waondoke makambini.

Hivyo ndivyo nilivyomwelewa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar!
 
Safi sana! Waondoke bwana maana serikali yao ni sikivu. Haya haya ndo yanawarudisha madarakani kila uchaguzi. Namwomba RC akaze hukumu kabisa!
 
Back
Top Bottom