Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,597
Kwa kadri ya matangazo ya TBC1 saa 2 usiku, RC wa Dar amewapa week moja wahanga wa mafuriko ambao ni wapangaji waliohifadhiwa kwenye makambi mbali mbali, waondoke wakatafute nyumba nyingine. Kwa maoni yake, serikali haina haja ya kuendelea kuwahifadhi watu hawa!
My take,
Kama wameathirika na mafuriko na kupoteza mali zao, watawezaje kupanga nyumba mpya???
Updates:
Wakazi mabondeni vichwa ngumu
na Datus Boniface
WAKATI baadhi ya wakazi wa mabondeni wakikaidi agizo la kuwataka kutorejea kwenye maeneo yao kwa muda, Serikali imeapa kuchukua hatua kali kwa atakayekaidi amri hiyo.Aidha, imesema inatarajia kulisafisha eneo la bonde la Jangwani na Msimbazi ili litumike kwa ajili ya kilimo.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, wakati akizungumza na waandishi wa habari.Mkuu wa mkoa huyo alihoji utimamu wa wakazi hao wa mabondeni kupingana na serikali kwamba hawako tayari kuhama.
"Inaonekana wananchi hao hawana akili timamu kutokana na msimamo wao wa kung'ang'ania kukaa maeneo ya mabondeni ambayo ni hatarishi kwa maisha yao. Lakini pia watu hawa walishindwa kesi mahakamani waliyoifungua wakipinga kuhamishwa na serikali mwaka 2002, lakini bado wameng'ang'ania," alisema RC huyo.
Aliendelea kusema kuwa: "Maeneo ya bonde la Jangwani, Mto Msimbazi awali katika ramani ya uendelezaji mji wa Dar es Salaam, yalitengwa kama maeneo hatarishi, pia kwa mujibu wa sheria za ardhi zilipiga marufuku shughuli zozote kufanyika, lakini wananchi hawa walivamia na kukaidi amri ya kuwataka waondoke katika maeneo hayo.
"Lakini cha ajabu ni kwamba mwaka 2001, walifungua kesi Mahakama ya Ilala wakipinga hatua hiyo, hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri ambaye kwa sasa ni marehemu, aliwataka waondoke kwani maeneo hayo ni hatarishi lakini wameshindwa kuondoka hadi juzi mafuriko yalivyowaondoa kwa nguvu," alisema.
Alisema: "Kama wana akili timamu wangetoa vitu vyao. Hawana akili timamu kutokana na kushindwa kuhama na badala yake wanataka wapewe misaada."
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa huyo, kutokana na wakazi hao kukaidi amri hiyo, serikali haitakuwa na urafiki katika hilo na wameamua kuweka doria kwa lengo la kumkamata mwananchi yeyote atakayerudi kuishi au kufanya shughuli katika maeneo hayo.
Mkuu wa mkoa huyo alisema, huduma za nishati ya umeme, maji, barabara na hospitali zimepigwa marufuku katika maeneo ya mabondeni. Alisema kama kigezo ni kumaliza kodi zao za mwaka, ni bora wakaenda kwenye vyombo vya sheria kudaiana. Alisema hakuna haja ya wakazi hao kung'ang'ania maeneo hatarishi wakati tayari kuna viwanja 700 vimetengwa kwa ajili yao.
"Wananchi wa mabondeni, waondoke kwa hiari yao, hakuna taasisi itakayoruhusiwa kufanya shughuli zake katika eneo hilo," alisema.
Kuhusu kugawiwa viwanja, alisema awali serikali ilitoa viwanja maeneo ya Yombo Dovya, lakini waliviuza na sasa itatoa vingine katika eneo la Mabwepande, Machimbo na Kunduchi.
Alisema viwanja hivyo vitagawiwa kwa mpangilio maalumu ili kuepuka uchakachuaji, lakini alionya kuwa si jukumu la serikali kuwajengea nyumba kwani itawapa ardhi bure.
Katika hatua nyingine, Serikali imewataka wananchi waliopanga nyumba maeneo ya mabondeni, waondoke mara moja katika makambi ya waathirika wa mafuriko.
Mkuu wa mkoa alisema serikali haitaendelea kuwabeba wananchi wa aina hiyo kwani wana uwezo wa kijitegemea.
Alisema wapangaji hao watafute nyumba za kupanga badala ya kuendelea kukaa katika makambi bila sababu za msingi.
Kwa upande mwingine serikali imetoa muda wa wiki mbili kwa wananchi wanaohifadhiwa katika makambi hayo kuondoka kabla ya shule hazijafunguliwa.
Mecky Sadick amesema, kama watashindwa kutii amri hiyo watahamishiwa eneo la Mabwepande, Kunduchi ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kuendelea na masomo yao.
Source: Tanzania Daima (http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=31306)