Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,890
Mama, mtoto wafia mapokezi ya hospitali kwa kukataliwa huduma
* Ni baada wauguzi kukataa kumhudumia mjamzito
Na Jackson Odoyo
MAMA mjamzito, Teddy Kimoso amefia katika mapokezi ya Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam wakati akijifungua, baada ya wahudumu waliokuwa zamu kugoma kumhudumia kwa vile hakuwa na vifaa vya huduma hiyo.
Mama huyo amekufa pamoja na mtoto wake ambaye alikuwa tayari anaanza kutoka.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya mjazito huo kufika hospitalini hapo akiwa na ndugu zake, huku hali yake ikiwa mbaya na wahudumu waliokuwa zamu wakagoma kumpatia huduma muhimu kwa wakati unaotakiwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hospitalini hapo jana, mmoja wa ndugu za marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Kimoso, alisema alipigiwa simu usiku wa kuamkia jana kwamba, wauguzi wamekataa kumsaidia mgonjwa huyo mpaka wapewe fedha za kununulia vifaa vya kujifungulia.
Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, alianza kuwasiliana na baadhi ya ndugu zake ili waangalie jinsi ya kumsaidia mgonjwa huyo na kwamba, wakati wote huo hali yake ilizidi kubadilika.
Alisema kutokana na muda, aliweza kuwasiliana na ndugu waliokuwa karibu na hatimaye wakafanikiwa kufika hospitali hapo na kununua vifaa hivyo.
Alitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na 'glovu' (mipira ya kuvaa mikononi), pamba, sindano, dawa za maumivu na maji ya uchungu.
Alisema baada ya vifaa hivyo kupatikana, walimchukua na kumpeleka katika wodi ya Karume, lakini wahudumu hao waliendelea kuwa wazito kumpatia mgonjwa wao huduma kwa wakati unaohitajika.
Alifafanua hata walipoamua kwenda kwa hiyari yao, walikuwa wakitoa maneno ya kejeli kwamba anawapigia kelele wakati anafahamu utaratibu wa hospitali ulivyo.
Alisema wakati huo mtoto alikuwa ameshaanza kutoka, huku hali ya mgonjwa ikizidi kuwa mbaya.
''Siwezi kuzungumza mengi ndungu mwandishi, kwani nina huzuni sana kutokana na hali hii kwani siku hizi watu wa hali ya chini tunakufa kwa sababu ya kukosa fedha, kwani kama ndugu yangu angekuwa na fedha pengine asingefariki dunia,'' alisema Kimoso na kuongeza:
''Mimi si msemaji wa familia, msemaji ameshaondoka na tunakwenda kukusanyika ili tujue cha kufanya, tumeshangazwa na tukio hili na hiki ni kizazi cha tatu cha marehemu. Na kuhusu mazishi, tunategemea kumsafirisha leo kwenda Morogoro,'' alisema.
Ndugu mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Yekonia Gabrieli alisema kuwa wanatarajia kumsafirisha marehemu kwenda Morogoro kwa mazishi na baada ya mazishi wataanza kufuatilia kwa undani wa kifo cha ndugu yao.
Mazingira ya kifo cha marehemu huyo, yaliwashangaza wangonjwa wengi waliokuwa hospitalini hapo, huku wakisema kuwa mama huyo alihangaika kwa muda mrefu bila kupatiwa huduma.
Mama mmoja aliyekuwa katika wodi ya Karume, alisema marehemu alipelekwa wodini hapo akiwa hajitambui huku mtoto akiwa ameanza kutoka, lakini wauguzi hao hawakuonyesha jitihada za kumsaidia.
Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake gazetini, mgonjwa huyo alisema yeye alipelekwa hospitalini hapo tangu juzi asubuhi na akajifungua usiku na kubainisha kwamba, katika kipindi alichokaa hospitalini hapo, amejionea uzembe mwingi unaofanywa na wahudumu wa hospitali hiyo.
Alisema mbali na kifo cha marehemu Kimoso, kuna akinamama wawili walifariki dunia hospitalini hapo wakati wa kujifungua kutokana na uzembe wa wauguzi.
''Marehemu aliletwa hapa wodini akiwa na hali mbaya na ninadhani alishafariki kwani alipoletwa akalazwa kitandani kisha akazungushiwa pazia la kijani na ndani ya pazia hilo kulikuwa na wauguzi watatu huku mmoja akiingia na kutoka. Na baada ya hapo hawakuelewa kilichoendelea,'' alisema na kuongeza:
''Ilipofika asubuhi tukaona anatolewa na kuingizwa kwenye mkokoteni. Ndipo tukagundua kuwa amefariki dunia kwani hali ya uzembe katika hospitali hii inatisha''.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Asha Mahita alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa hafahamu kama kweli mgonjwa huyo alifariki kutokana na uzembe wa wauguzi.
Mahita alisema hawezi kupinga wala kukubaliana na taarifa hiyo kwa sababu hospitali hiyo ina wahudumu zaidi ya 400 na kati yao, wapo waadilifu na wasio waadilifu.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Beatrice Byarugaba alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema hana taarifa yoyote juu ya tukio hilo na kwamba atafuatilia ili kufahamu undani wake.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji, Judith Kahama alisema hana taarifa japo kutwa nzima alikuwa akiwasiliana na hospitali hiyo pamoja na manispaa na kuahidi kuwa atafuatilia kwa undani suala hilo.
Tuma maoni kwa Mhariri
Habari katika picha na Matangazo