Wahandisi tunataka kila anayejenga ghorofa lazima usanifu na ujenzi atumie wahandisi

fazam

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,716
2,000
Ukienda mtaani unakuta mtu anajenga nyumba ya kigorofa kimoja, chini anasimamisha nguzo za zege alafu analaza tofali zote za ile sehemu ya chini. huku ni kuongeza gharama za ujenzi ambako kama wangekuwa wanatumia wataalamu bila shaka gharama zingepungua.

Unakuta mtu anajenga nyumba kwa kujitahidi kuweka choo cha public na masta ya nyumba karibu ili etu kupunguza gharama. gharama anazopunguza ni bomba za maji machafu ambazo gharama yake ni ndogo sana na akienda kuezeka anaezeka kama kanisa.

Jamii inatumia umbumbumbu katika ujenzi ambao wataalamu wakitumika gharama za ujenzi zitapungua na ubora utaongezeka
Kumbe mna bei nafuu hivo...mbna hamsemi....watu wanaogopa gharama zenu
 

Queen matty

Member
May 14, 2016
69
125
Ninawafaham mafundi wa mitaani waliochora na kujenga nyumba vizuri zaidi kuliko hao mainjinia wenu. Elimu ya kwenye daftari na ya field ni vitu viwili tofauti.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,726
2,000
Kwani Sheria zinasemaje?

Wewe Mhandisi alafu haujui Sheria?, Ramani mpaka ipitishwe na mipango miji n.k. lazima structure engineer awe amefanya kazi yake.., sasa kwa kutokupitisha huko au mtu kupiga muhuri kabla ya kufuata vigezo vyote (soil test n.k.) sio mapungufu ya Sheria bali utekelezaji...

Na kama bei zinazowekwa sio rafiki unategemea nini kama watu sio ku-cut corners....

Ni mambo mengi hata wiring / electrical installations mwisho wa siku zitakuwa zinafanywa na certified electrician ambaye kila mwaka anatakiwa kufanya checjk-up..., bila kufanya hivyo hata kama una Bima unaweza kujikuta Ukipatwa tatizo haulipwi sababu umekiuka vigezo

Anyway huko ni mbali sana kufika ukizingatia kipato cha walengwa ni cha kubangaiza kwahio sheria haziwezi kuwa strictly sana
 

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,773
2,000
Kama kufungua biashara ya duka la dawa ni lazima udhaminiwe na dakitari inakuwaje shughuli za kihandisi zinafanyika bila kuhusisha wahandisi.

Kufungua gereji, ujenzi wa majengo ya gharama, sehemu za kuchomelea, n.k yote haya yanafanyika holela.

Kama madaktari wameweza hivi sisi wahandisi tunashindwa nini?

Nadhani tofauti kubwa ni madaktari wanacho chama strong kinachowatetea na sisi wahandisi tupo tupo tu.

Ni lazima jamii ijenge mazingira ya kujiri wataalamu inaowasomesha.
Wewe Mhandisi ili nikuamini unaweza wewe umefanya nini cha kihandisi ukiondoa ile project uliyopewa na instructor wako aka propesa
 

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,773
2,000
Na akija Mhandisi kwangu lazima na mwanasheria awepo, tusainishane mkataba wa kazi na ikiharibika uweze kulipa gharama zote
 

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,517
2,000
Mkuu beam 45(450mm) walikuwa wanajenga ghorofa moja(Residential) ndiyo standard ni kama kwenye tofali 6" za kulaza kwenye ghorofa zinacheza 15 mpaka 16 ndiyo unapiga beam au za kusimama kawaida kozi 10/11 kisha beam(linta) hizo ni standard,sasa engineer wa TBA akamwambia fundi la 7 beam kwenye mchoro imeandikwa 70 ,ndipi std 7 akakataa akamwambia beam 70 ukifunga box lake unaweza ikafika kwenye kitovu na nondo utaweka 8 ndipo akakubali waweke 45.

Professional yeye ni kwenye makaratasi ndiyo mtaalam ila field(Site) mweupe.
Hao walitaka kumuibia fundi
 

Frank mtanganyika

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
213
500
Wewe Mhandisi ili nikuamini unaweza wewe umefanya nini cha kihandisi ukiondoa ile project uliyopewa na instructor wako aka propesa
Wahandisi wana board inayowasimamia inaitwa ERB( engineer registration board) ili usajiliwe lazma wamethibitisha capability yako ya ufanyaji kazi pamoja na kaz ulizozifanya kwahio ili mtu aitwe mhandisi be lazma amethibitiswa na board na anaruhusiwa kufanya shuhuli za kiuhandisi . Ukihitimu tu chuo na degree yako bado hujawa mhandisi mpaka board itakapo kusajili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom