Wahandisi mliopo madarakani: Jangwani inahitaji complete redesign

Pale wanipe mimi nilime mpungaaa tu .....
Any way ushauri wako ni mzuri umejikita kitaalam zaidi,i hope wamekusikia hawa wasiyopenda kushauriwa....
Tatizo mambo Yao wanafanya siasa nyingiii

Ova
 
Kaka mi naomba uelewe kuwa eneo la Jangwani ni almost Sea Level, yaani wakati wa High tides (Bamvua) maji ya bahari huwa yanatapikia hayo maeneo ya bonde la jangwani, Bonde la Mkwajuni, pamoja na Bonde la Magomeni, kiuhalisia hilo eneo alihitaji ujenzi wa aina yoyote zaidi ya kuachwa na kuwa hifadhi ya Mikoko tu
Hujaelewa mkuu! Mleta mada alichokisema, ni kuwa pale kutoka magomeni hadi fire owe ni kama flyover na MTO msimbazi uwe ni njia ya usafiri ya maji, yaani pawe na boat kama daladala, hata Mimi niliwaza hii ingekuwa ni bora zaidi, japo ni gharama" kumbuka nchi nyinginge zina mifereji kibao mjini inayotumika kama barabara za trip town, badala ya habari watu wanatumia boat"
 
Hatua muhimu ya kwanza ni kumnyonga hadharani mhandisi aliyeshauli ofisi na gereji za UDART ijengwe pale jangwani,angalau ningemuona ana akili timamu angechukua level ya muhimbili ndo angeinulia pale lakini kuruhusu majengo ya mabilion kujegwa bondeni vile ni kusudi na kuchokoza hasira za walipa kodi tu.Leo hii pale panahitaji marekebisho makubwa wakati mradi hata miaka mitano haijapita.
Nimekuelewa sana mkuu, hata Mimi nilikuwa natamani yule muhandisi Wa pale anyongwe hazarani, huenda ingesaidia wengine kubadilika na kuacha kututia hasara.
Akinyongwa hazarani itakuwa ni hata muhimu sana ktk maendeleo ya nchi hii!
 
Nimepita sehemu ya Jangwani juzi na hali ya pale inasikitisha.
Kwa sasa mapito ya mto yamebadilika kabisa, na mto Msimbazi haukidhi overland flow ya storm water-maji ya mvua.
Pale kumewekezwa rasilmali kadhaa, tena nzito, moja ni karakana ya UDART.

Kutokana na hali halisi ya mabadiliko ya maji yanayokusanywa upstream, tukumbuke kuwa eneo la kukusanya maji ya mto Msimbazi ni lile lile, lakini kutokana na ujenzi wa nyumba nyingi sana kadri miaka inavyoenda, ile tunaita percolation into the soil imepungua sana(maji kuingia ardhini).
Hivyo maji yote yanaelekezwa bonde la mto Msimbazi.
Daraja la mo Msimbazi si tu kwamba halitosh bali mchanga na vifusi vimepunguza sana ufanisi wa daraja.

Mimi ni mhandisi, kuna njia mbili au tatu kurekebisha hali hii.
Na njia zote zinahitaji uwekezaj mkubwa sana.
  1. Kutengeneza waterway toka Selander Bridge mpaka Kigogo. Yaani kuupanua sana mto, na isiwe kadaraja ka mita 50 pale Jangwani bali hata mita 100 au 150 ili hata boti ziweze kupita chini.
  2. Kunyanyua sana tuta toka Fire hadi Magomeni Mapipa, sambamba na kupanua daraja na kuondoa kifusi mtoni(dredging). Hii itafanya njia kupitika vipindi vyote.
  3. Kufanya protected river training kuanzia mwisho wa waterway hapo juu hadi Vingunguti.

Naamini tusipo badilisha mawazo jinsi ya kutatua matatizo ya kufurika Jangwani, tutaonekana kama wahandisi tusioenda na wakati.

Tukumbuke kwa waiofika Netherlands, karibia 26% ya eneo la nchi yote iiko below sea level.
Na 50% ya nchi nzima iko 1metre above sea level.
Yaani ni sawa na nchi nzima kuwa kama eneo la Coco Beach, lakini ni wahandisi waliookoa hali na nchi inakalika.

Lets try to think outside the box!!
Angalia usiwekwe ktk kundi lile lingine lisilotakiwa Msimu huu
 
Back
Top Bottom