Wahamiaji haramu 36 wakamatwa Dar, RC Kunenge atoa onyo kwa wanaowahifadhi na wanaowasafirisha

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es salaam vimefanikiwa kuwatia mbaroni Wahamiaji haramu 36 raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini kinyume na taratibu ambapo Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa onyo Kali kwa Raia wa Tanzania wanaoshiriki kuwafadhili na kuwasafirisha kwa ili wapate fedha.

RC Kunenge amesema Wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia November 15 kwenye fukwe za Mbweni ambapo kati yao 30 wanatoka nchini Ethiopia na Sita wanatokea nchini Somalia.

Aidha RC Kunenge amesema hata utaratibu unaotumika kusafirisha watu hao unakiuka Sheria, haki na utu wa binadamu sababu wengi wao wanafungiwa kwenye kontena zisizokuwa na hewa na pindi wanapobainika kufariki Dunia maiti zao hutupwa kwenye vichaka.

Pamoja na hayo RC Kunenge amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.

Kwa upande wake Afisa uhamiaji Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishina Msaidizi Edmund Mrosso amesema kinachofuata baada ya wahamiaji hao kukamatwa watafikishwa Mahakamani kwa kosa la Kuingia nchini kinyume na taratibu.

Aidha Kamishina Mroso amesema kwa wale wanaowasafirisha au kuwahifadhi wahamihaji hao adhabu inaelekeza kifungo Cha miaka 20, faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizotumika.

1605700369705.png
 
Muafrika ndani ya Afrika anaitwa muhamiaji haramu?!!!?. Kabla ya mkoloni kuja Afrika wakushi walitembea Afrika yote leo kuja Mzungu Tunawaita Wahamiaji haramu!!!!!!!!?. Najiuliza walikuwa wanapita kwenda kwa Madiba au Wamekuja kwa Nyerere. Bila shaka wanakwenda kwa Madiba sasa nyie Uzao wa Nyerere mnaumia nini?.
 
Ethiopia Wana mafrayiova Kama yote,treni SGR na Mindege zaidi ya 120,lakini wananchi wanaisoma namba.
 
Back
Top Bottom