Nini maana ya Wahafidhina?

Ni mtu hasiyependa mageuzi au mabadiriko ya kimaisha, mara nyingi utumika kwenye siasa (conservative)
 
MUHAFIDHINA ni mtu anaetumiwa kukwamisha jitihada za mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi au hata kijamii.
 
yy
Ni mtu hasiyependa mageuzi au mabadiriko ya kimaisha, mara nyingi utumika kwenye siasa (<i>conservative</i>)
kwa kuongezea tuu ni ma-conservative wenye misimamo mikali wasiotaka mabadiliko (fundamentalists), hivyo wako tayari kufanya lolote ili kuhakikisha wanalotaka wao ndilo.
 
yy kwa kuongezea tuu ni ma-conservative wenye misimamo mikali wasiotaka mabadiliko (fundamentalists), hivyo wako tayari kufanya lolote ili kuhakikisha wanalotaka wao ndilo.
Mi nilifikiria Fundametalists ni watu wenye kufuata misingi ya ukweli wa jambo wanalo liamini.

Kama mtu ni doctor nadhani ni bora kwake kufuata fundamental of physician ili hawe daktari mzuri au wewe unaonaje mkuu.
 
Kwa kweli mimi nafikiri kwamba kuwa "mhafidhina" kunabeba wazo la kuhifadhi mambo yanoyodhaniwa ni yenye ubora maishani. Zaidi ya hayo, mtu mhafidhini hukaribisha maendeleo mapya kama hayapingi wazo lake kuhusu anachofikiri kitafaa kulingana na falsafa yake. Siku hizi neno "mhafidhina" huchukuliwa mara nyingi kama neno lenye kudharau au kubeza maoni fulani ya mtu. Ni lazima dhana hili litofautishwe na dhana la "fundamentalist". Mawili hayo si visawe hata kidogo.
 
Heshima mbele wakuu
Naomba kuuliza WAHAFIDHINA maana yake nini?je neno ni la lugha gani?ni sifa zipi zinazomtambulisha mhafidhia kwa jamii?

anayependa kuenzi mambo/taratibu/desturi za zamani. kwa kiingereza conservative. ni neno la kiswahili

kumtambua ni mpenda desturi za kitambo na mara nyingi huwa watu ambao umri umesogea
 
Back
Top Bottom