Wahafidhina CCM wanapoikana misingi ya TANU, ASP


B

Bayana

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Messages
433
Points
0
B

Bayana

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2012
433 0
Si mbaya ukisoma na kuchukua kile ambacho kitakufaa maishani. Hii ni makala kutoka katika gazeti la leo la Mwananchi:


KATIKA kitabu 'Tujisahihishe' kilichoandikwa na Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1962 ukurasa wa pili, anaeleza dhana nzima kuhusu ukweli.

Anasema, “Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa walamdogo, haujali adui au rafiki wote kwake ni sawa. Pia ukweli una tabia yakujilipiza kisasi kama ukipuuzwa.

“Ukiona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa nidongo au mpira, natumaini utanionya.

“Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo aukwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole, japo ningekuwanani.

“Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa! Wakati mwingine mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli, lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake.

“Nikisema mbili na tatu ni sita nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha.

“Ni kweli mbili mara tatu ni sita, lakini mbili na tatu ni tano,siyo sita.

“Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu nakukubali yako kwa kusema meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwaunatumia hoja ambazo hazina maana.

“Huu ni mfano wa upuuzi, lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu,huwa hazihusiana kabisa na mambo tunayojadili,” anasema Mwalimu katika kitabuchake hicho.

Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume katika Mkutano Mkuu wa nane wa CCM Mjini Dodoma uliomalizika hivi karibuni analia na mtindo wa baadhi yawatu ndani ya chama kupuuzwa hata kama wanasema ukweli.

Anasema kumezuka mtindo ambao sio uliojenga misingi ya TANU naASP wa baadhi ya watu kupuuzwa wakati wa kutoa maoni au kuchangia hojambalimbali, na wakati mwingine kupachikwa majina ya ajabu ambayo hayahusiani kabisa na hoja inayojadiliwa.

Karume anahimiza kuvumiliana katika utoaji wa maoni kuhusu Katiba kwani watu wamegawanyika kuhusiana na kile ambacho wanataka kiwemo katika Katiba mpya hususani suala la Muungano. Mwisho wa makala.

Hivi nitakosea nikisema kuzomewa kwa Karume kulikuwa na baraka za viongozi wakubwa wa CCM akiwemo m/kiti? Kama hivyo ndivyo, rais Kikwete anapata wapi ujasiri wa kusema kuwa ataheshimu maoni ya Watanzania bila ya hila zozote ikiwa ameshindwa kurekebisha ndani ya chama chake?
 

Forum statistics

Threads 1,294,399
Members 497,915
Posts 31,174,714
Top