Wahadhiri wagoma

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Wahadhiri Ustawi wa Jamii wagoma kufundisha

Wahadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam wamegoma kuingia darasani kufundisha wakiushinikiza uongozi wa chuo uondoke na bodi yake iundwe upya.


Aidha, wamesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wenzao kumi kufukuzwa kazi katika kipindi cha miezi mitatu bila sababu za msingi.

Uamuzi huo wa kutoingia madarasani ulitangazwa jana baada ya kukaa kikao ambacho kiliamua kitakuwa kikifanyika kila siku kuanzia jana hadi madai yao yatakapopata ufumbuzi.

Mwenyekiti wa kikao hicho, Faustine Nzigu, alisema wameamua kutoingia darasani baada ya juzi wenzao saba kupewa barua za kufukuzwa kazi.

Nzigu ambaye aliongoza kikao hicho, alisema sababu zilizotajwa kwenye barua za wenzao waliofukuzwa sio za msingi ndio maana wameamua kutofundisha.

Alisema Februari mwaka huu, walienda ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, kumuelezea malalamiko yao kuwa chuo hicho hakina uongozi na kwamba waliopo wanakaimu nafasi zilizokuwa wazi, lakini aliwaeleza kuwa analifanyika kazi suala hilo na kwamba hadi Machi 2011 litakuwa limeshapatiwa ufumbuzi lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji.

Endelea kusoma bofya hapa
 
Ni bora wagome mana wana sababu za msingi kugoma. Nchi hii bila kugoma hupati haki kwa wakati
 
nami nawaunga mkono. Bora wagome chuo kinaendeshwa kizandiki sana
 
Back
Top Bottom