instanbul
JF-Expert Member
- Jun 26, 2016
- 11,381
- 14,186
Wangekuwa wanalipwa vzr wasingebuni vikai vya ajabu ajabu ili wapate posho.Nakuelewa sana tu. Hata hivyo sometimes ni lazima ukweli usemwe ili nchi yetu ipige hatua kwa ajili ya future ya nchi yetu, watoto wetu na vizazi vyetu vijavyo.
Vyuo vyetu vikuu ni sehemu ya ujinga mwingi uliomo kwenye nchi yetu wa kutumia pesa za umma bila tija yoyote ya maana inayoonekana kwenye jamii. Ungekuwa umo ndani ya system ya vyuo vikuu vya umma vya Tanzania ungeshangaa kuona jinsi wakuu wa vyuo wanavyoprioritize maslahi yao binafsi kuliko agenda halisi za uwepo wa vyuo vikuu.
- Utashangaa kuona magari ya viongozi wa vyuo yakiharibika kesho yake linaenda kutengenezwa fasta au kununuliwa jipya kabisa (pesa hiyo huwa haikosi), lakini vifaa vya maabara vikiharibika hiyo ndio ntolee.
- Utashangaa kuona vyuo vikuu vyenye idara za sayansi (kama biolojia, chemia na fizikia) havina maabara functional yenye vifaa hata basic katika kufanyia tafiti, lakini vyuo hivyo havikosi bajeti ya kununua magari mapya.
- Utashangaa kuona vyuo vinakaa vikao mbali mbali vinavyolipa mapesa mapesa lakini wakati huo huo havina bajeti ya kufanya tafiti.
- Na mifano mingi kama hiyo.
Vyuo vya umma vipo kwa ajili ya kufanya tafiti, kufundisha na kuleta innovations za maana kwa faida ya nchi, na matumizi ya pesa za serikali huko vyuoni yanapaswa kuakisi hilo.
Ni kweli mishahara ya wahadhiri wa vyuo vya umma ni miduchu lakini pia kazi zao za msingi hawaonekani kama wanazifanya kwa ufanisi. Wapo wapo tu yaani.