SoC02 Wahadhiri wa Elimu ya juu na Matumizi mabaya ya ratiba za masomo

Stories of Change - 2022 Competition

Triceb

New Member
Sep 4, 2022
4
3
WAHADHIRI WA ELIMU YA JUU NA MATUMIZI MABAYA YA RATIBA ZA MASOMO.



UTANGULIZI
;

Kwa kawaida, miaka ya masomo kwa elimu ya juu huwa ina mihula miwili yaani muhula wa kwanza na wa pili wa masomo. Wahadhiri wengi wamekuwa wakitumia vibaya muda uliowekwa wa masomo na hivyo kupelekea malimbikizi mengi ya mada za kusoma na wakati mwingine malimbikizi mengi ya mitihani.

Changamoto hio inasababisha wanachuo wengi kujikuta na mambo mengi ya kujisomea ilhali muda wa mitihani ya mwisho wa muhula ukiwa umekaribia sana. Mbali na hayo, matumizi mabaya ya muda unaofanywa na wahadhiri hupelekea alama za mitihani midogo ya muhula ambayo hutumika kutengeneza “koziweki" kuchelewa kutoka na hivyo kusababisha mara kadhaa wanafunzi kuingia kwenye mitihani yao ya mwisho wa muhula bila kujua alama zao za mitihani midogo yaani “courseworks”. Kwani kujua ni alama ngapi ulipata husaidia sana kujua ni nguvu kiasi gani uweke ili uweze kufaulu vizuri mitihani ya mwisho wa muhula.

Lakini pia, kuna baadhi ya kozi katika vyuo vikuu ambazo hazifuati ratiba zilizowekwa za mitihani midogo ya muhula, badala yake wahadhiri wa kozi hizo wamekuwa wakitoa mitihani hio kwa kufuata ratiba zao yaani kwa kuangalia ni lini wao wana nafasi ya kutoa mitihani hio kwa wanafunzi, hii inapelekea wahadhiri wengi kujikuta wamechelewa sana kutoa mitihani hio au kazi (assignments) kwa wanafunzi na hivyo kulazimika kuwapa mitihani na kazi hizo kwa wakati mmoja, na hivyo wanafunzi kujikuta wakiwa na mitihani na kazi nyingi za kufanya ndani ya muda mfupi sana, ili koziweki za masomo hayo ziweze kupatikana kwa haraka kabla mitihani mikubwa ya mwisho wa muhula kuanza. Kwa mfano, inaweza ikawa wiki mbili kabla ya mitihani mikubwa ya chuo kuanza, wahadhiri wanne wa kozi moja wanakumbuka kuwa hawajakamilisha idadi inayotakiwa ya mitihani midogo ya muhula inayotengeneza koziweki na hivyo kutoa mitihani hio au kazi binafsi (individual assignments) kwa haraka na kwa pamoja bila kuwaza msukumo mkubwa wanaowapa wanafunzi hawa ili kuhakikisha wanakamlisha kazi hizo, na kwa wakati huo huo kujiandaa kwa ajili ya mitihani mikubwa ya mwisho wa muhula, hii hupelekea wanafunzi kufanya kazi na mitihani hio kwa kiwango kisicho ridhisha sana kwa sababu huzifanya kwa uharaka sababu ya muda mdogo waliopewa.

Jambo hilo, yaani ufanyaji wa mitihani hio kwa muda mfupi na kwa uharaka linapelekea wanafunzi wengi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani hio midogo na hivyo kuingia kwenye mitihani mikubwa wakiwa na koziweki ndogo na hatimaye kuishia kupata jumla ya alama ndogo na zisizoridhisha sana.

Lakini pia, alama hizo ndogo zinazotolewa na wahadhiri husababishwa na usahihishaji wa haraka na usio ridhisha wa kazi na mitihani hio inayotengeneza koziweki ili tu waweze kutoa alama hizo kabla ya mitihani mikubwa ya chuo kuanza, na hivyo kupelekea wanafunzi kupewa alama ndogo na ambazo huenda zingekuwa kubwa kama usahihishaji ungefanyika vizuri na mapema.

Ni wazi kuwa ili kufaulu darasani, wanafunzi wanapaswa kuwa na juhudi sana yaani kujisomea na kujiandaa vizuri kabla ya mitihani lakini si mara zote inakuwa rahisi kufanya hivyo hasa pale wahadhiri wanaposhindwa kufuata ratiba za muhula husika wa masomo na hivyo kupelekea wanafunzi kuwa huru sana mwanzoni mwa muhula sababu vitu vingi wanakuwa hawajavisoma bado darasani, na kinyume chake kuwa na mambo mengi ya kujisomea mwishoni mwa muhula ambapo wahadhiri ndipo huona umuhimu wa kumaliza mada hususa za muhula huo. Jambo hilo linapelekea mada hizo nyingi kufundishwa mwishoni mwa muhula huku wahadhiri wakikimbizana na muda ili kumaliza mada hizo, na hivyo kujikuta wakizifundisha juu juu tu na kwa haraka sana.

Kufanya hivyo pia kunawalazimu wanafunzi kujisomea mambo mengi ndani ya muda mfupi ili kuwa na chochote cha kujibu ikiwa mada hizo zitaulizwa katika mitihani ya mwisho wa muhula licha ya kuwa mada hizo zinakuwa zimefundishwa wakati mitihani ya mwisho wa muhula ikiwa karibu sana.

Nini kifanyike?

Ni wazi kuwa ratiba za masomo kwa elimu ya juu huandaliwa mapema kabla ya mwaka husika wa masomo kuanza hivyo ratiba hizo huwa zinafahamika mapema kwa wahadhiri na hata wanafunzi. Na hio inafanya iwe rahisi kwa wahadhiri kujua idadi ya mada anazopaswa kufundisha na jinsi gani atazimaliza ndani ya muda sahihi bila kuleta shida kwa wanafunzi au hata kushindwa kuzimaliza.

Kwa hiyo, wahadhiri wa elimu ya juu, wanawajibu wa kupanga vizuri ratiba zao binafsi ili kuepuka kushindwa kuhudhuria vipindi mara kwa mara. Ni jambo linaloeleweka kuwa watu wote wana majukumu mengi mbali na majukumu ya kikazi, lakini jambo hilo halipaswi kuwa kisingizio cha kushindwa kuhudhuria vipindi au kutoa mitihani midogo ambayo ni ya lazima ili kukamilisha alama za koziweki.

Inaeleweka kuwa wahadhiri hao huwa na masomo mengi ya kufundisha chuoni, kwa mfano mhadhiri mmoja anaweza kuwa akifundisha somo moja kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, na akawa tena na somo lingine la kuwafundisha wanafunzi wa mwaka wa pili, na wa tatu n.k, pia anaweza kuwa anafanya kazi nyingine nje ya kuwa mhadhiri, mfano anaweza kuwa ni daktari au mwanasheria, na hivyo kuwa na majukumu mengi na ratiba inayobana sana, lakini bado sababu zote hizo hazimaanishi wanafunzi wanyimwe haki yao yaani elimu bora na si bora elimu.

HITIMISHO;

Ili kupata wataalamu bora katika nyanja mbalimbali, ni muhimu elimu inayotolewa katika ngazi mbimbali za elimu iwe yenye ubora wa hali ya juu. Hio inahusisha jitihada si za wanafunzi pekee bali na za wahadhiri ambao ndio watoa elimu hio.

Pendekezo langu ni wahadhiri hawa waone umuhimu wa kufuata ratiba zilizowekwa na kufundisha bila kukosa vipindi, ili kupunguza malimbikizi ya mada na mitihani ambayo hupelekea vyote kwa pamoja kufanyika mwishoni huku muda ukiwa sio rafiki tena, na hivyo kufanyika kwa njia ambayo si nzuri.



Naomba kuwasilisha.
 
Yaani King Msukuma alipwe mil 15. Afu Dr....alipwe million 2.5 afu umpangie kazi. Thubutu. Ukileta kiherehere. Una kula Supp. Ww jisomee vitabu na notes zake. Mambo ya ratiba achia management yake. Acha harakati chuo. Uta Disco.
 
Yaani King Msukuma alipwe mil 15. Afu Dr....alipwe million 2.5 afu umpangie kazi. Thubutu. Ukileta kiherehere. Una kula Supp. Ww jisomee vitabu na notes zake. Mambo ya ratiba achia management yake. Acha harakati chuo.

Yaani King Msukuma alipwe mil 15. Afu Dr....alipwe million 2.5 afu umpangie kazi. Thubutu. Ukileta kiherehere. Una kula Supp. Ww jisomee vitabu na notes zake. Mambo ya ratiba achia management

Yaani King Msukuma alipwe mil 15. Afu Dr....alipwe million 2.5 afu umpangie kazi. Thubutu. Ukileta kiherehere. Una kula Supp. Ww jisomee vitabu na notes zake. Mambo ya ratiba achia management yake. Acha harakati chuo. Uta Disco.
Pesa wanayolipwa sio ticket ya wao kukosa vipindi. Halafu unasema nijisomee vitabu, hebu niambie nimekuja chuo kusoma sheria na ndo nakutana nayo kwa mara ya kwanza, nitaelewaje hivyo vitabu bila muongozo wa mwalimu? Halafu kusema changamoto zetu haimaanishi ni kiherehere.
 
Pesa wanayolipwa sio ticket ya wao kukosa vipindi. Halafu unasema nijisomee vitabu, hebu niambie nimekuja chuo kusoma sheria na ndo nakutana nayo kwa mara ya kwanza, nitaelewaje hivyo vitabu bila muongozo wa mwalimu? Halafu kusema changamoto zetu haimaanishi ni kiherehere.
Nadhani umesoma Secondary Shule za Private level zote. Spoon feeding. Kila kitu mnaletewa. Ila unge soma Shule za Govt especially pure Boys hata hizo kelele usingekuwa una tupigia humu JF. Zile shule zina kujenga kwa vitu vingi- kimaisha, kupambana, kujitaftia, kufikiria nje ya box, kujisomea hata bila Mwl. Una soma shule ya Government, choo kimejaa. Hapo uta jiongeza..Either ulalamike JF au uende pori, maji hakuna, Mwl wa Basic Maths hakuna, Kunguni, Maharage yame oza 98%, nk.

Ila sikulaumu sna. Ndio Elimu ya miaka hii. Imesababisha reasoning Skills za watoto ipo chini sna. Hata kazi za nyumbani hawawezi.
 
Back
Top Bottom