Wahadhiri wa COET UDSM badilisheni mfumo wa ufundishaji Chuoni.

Kategele

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
960
2,220
Moja kwa moja kwenye mada kwa ufundishaji huu mnaotumia mtaendelea kuzalisha Wahandisi wasio na uwezo kwenye utendaji kazi.
Haiwezekani mwanafunzi anamaliza chuo kichwani ni mweupe yani ukimpa kazi za field anazidiwa na fundi mchundo ambaye hajaenda shule kabisa.
Ushauri wangu,
1.Mwaka wa kwanza na wa pili mwanafunzi asome theory tu.
2.Mwaka wa tatu vijana wajifunze kazi za usanifu(Design Works)
3.Mwaka wa nne vijana wakae site mwaka mzima wakifanya kazi kwa vitendo na kuandaa project za mwisho
Mfumo huu utazalisha wahandisi wenye uzoefu tofauti na sasa kijana anamaliza chuo hawezi kufanya kazi kwa vitendo.
 
Nini maana ya field practical training? Mwaka wa 4 mwanafunzi anafundishwa Management, unataka akae site then Management's afundishwe mwaka gani?
Erb wameeka Miaka mitatu ya Graduate Engineer kujifunza kazi, na hii systems ipo duniani kote,
 
Ninachoshangaa Engineer anaendaje huko Site na SUTI na wapigapicha pick up nzima? Hapo bado ni Admin group kadhaa za Whatsapp.
Mchina SITE Hapo Hapo anajenga kibanda akihitaji nyapu wanachangia moja ya Mama Ntilie anayewapikia
 
Hilo tatizo sio la Jalalani tu kwakweli

Elimu ya Tanzania imejikita zaidi katika Nadharia kuliko Vitendo.

Ndio maana tumeanza kuzalisha Makandarasi kwa miongo mingi tangu baada ya Uhuru wa Taifa hili lakini mpaka Leo hii serikali iliyowasomesha hao Wakandarasi inaona bora kuwaajiri wafungwa wa huko China wanaokuja kutumikia vifungo vyao vya mwisho huku kuliko kuwaajiri Wabongo.

Hebu nipe kampuni moja tu ya Wabongo pekee inayoweza kushikilia tenda ya kujenga Daraja kubwa kama la kigamboni au Flyovers au jengo kama la Ngorongoro Arusha na kulimaliza.

Hili tatizo lipo hata SUA, ambapo wanasomea utaalamu wa kilimo kwa miaka na miaka lakini mpaka leo tunaagiza mbegu kutoka Israel, South Africa, Holland n.k

Hata Mbolea za viwandani eti tunakuja kutengenezewa pale Minjingu na Kalasinga.

Madaktari nao ni kuagiza Madawa kutoka India, UK, na hata Kenya achilia mbali vifaa vya gharama za kupimia.

Hata katika Kiswahili chetu wakija wageni hapa AFRICA basi utakuta Trainers wao wakubwa ni Wakenya.

Hata Kwenye michezo hatuwaamini Makocha wetu badala yake tunamwamini Shindikana kutoka Nigeria.

Tasnia ambayo inafanya vizuri Tanzania naona ni SHERIA peke yake kwa kiasi.

WABILLAH TAWFIQ
 
unaajiri engineer unataka afanye kazi za technician au fundi mchundo, wewe ndio hujui unachokifanya.
 
Mkuu. Bongo izi mambo za engineering bado sana na in real sense wanaoporomosha mifumo hii ni viongozi hawajui engineering ni practical zaidi ya hizo theory japo theories nazo ni muhimu kuna project nyingi zinaendelea maeneo ya karibu na vyuo vyetu ivi umeona kuna wanafunzi wanapata muda walau kwenda kupata experience, field miezi miwili au mitatu sio inshu kwa mwaka yani kwenye ratiba ya kawaida ya darasani iwekwe muda wa wanafunzi siku moja yote wakae site kujifunza. Nina rafiki yangu mcanada anasoma Civil kwa wiki anaingia mara tatu site na still ni mwanafunzi na anapata posho kidogo
 
Moja kwa moja kwenye mada kwa ufundishaji huu mnaotumia mtaendelea kuzalisha Wahandisi wasio na uwezo kwenye utendaji kazi.
Haiwezekani mwanafunzi anamaliza chuo kichwani ni mweupe yani ukimpa kazi za field anazidiwa na fundi mchundo ambaye hajaenda shule kabisa.
Ushauri wangu,
1.Mwaka wa kwanza na wa pili mwanafunzi asome theory tu.
2.Mwaka wa tatu vijana wajifunze kazi za usanifu(Design Works)
3.Mwaka wa nne vijana wakae site mwaka mzima wakifanya kazi kwa vitendo na kuandaa project za mwisho
Mfumo huu utazalisha wahandisi wenye uzoefu tofauti na sasa kijana anamaliza chuo hawezi kufanya kazi kwa vitendo.
Mainjinia wa Yudisimu wanafundishwa Wizi site na Rushwa makazini, Ulevi na Anasa, Umalaya na Kiburi cha kujiona wanajua kazi kuliko wengine waliotoka vyuo tofauti na wao.

Hiki chuo kimeliingiza taifa hili kwenye umasikini mkubwa sana na ni chuo cha ovyo kuwahi kutokea duniani.

Mainjinia wanaoongoza kula rushwa makazini ni wanaotoka huko! Kwa mbaali anafuatia St. Joseph!

1. UDSM
2. ST. JOSEPH
3. ARDHI
4. ST. AUGUSTINE
5.
6.
7.
Kwa mbali unawakuta Arusha Tech, DIT na MUST. Hapa wanajua kazi tuu. Mengine labda person characters.
 
Kwanza ujue fundi mchundo ni technician mwenye FTC ambae anafanana na mwenye Ordinary diploma nta 6...

Shida ninayoiona mimi kwa wakufunzi wetu ni wao kujua sana theory kuliko practical.Ilitakiwa mwalimu wa umeme awe anatokea kiwandani kwenda kufundisha chuoni.Au mwalimu wa masomo ya civil awe anatokea site.Pia wa masomo kadhaa ya mechanical awe anatokea kiwandani kwenda kufundisha chuoni..Mwanafunzi ataelewa kwa usahihi kile alichokuwa anatakiwa akijue..Maana Mwanafunzi ukimwambia kazi ya MCCB halafu ukaileta darasani ukamwelekeza inavyoungwa na kufanya kazi hawezi kusahau labda awe hataki kuelewa.

Lingine wachina kampuni zao zinapewa ruzuku na serikali ndio Maana zinaweza kuhandle miradi mikubwa.Sisi kusajili campuni upite brela na crb ni mbinde haswa..na hata ushasajili unataka uapdate upate daraja kubwa zaidi ni process ya mwaka hadi mwaka na nusu.Huwezi kulaumu.Mfumo wetu una kasoro nyingi ila tunapambana nazo na wachina wanaojua kurahisisha bei tutawashinda tu.
 
Ninachoshangaa Engineer anaendaje huko Site na SUTI na wapigapicha pick up nzima? Hapo bado ni Admin group kadhaa za Whatsapp.
Mchina SITE Hapo Hapo anajenga kibanda akihitaji nyapu wanachangia moja ya Mama Ntilie anayewapikia
Naona hapo kwenye nyapu ndo imekuuma sana eeh?!
 
Moja kwa moja kwenye mada kwa ufundishaji huu mnaotumia mtaendelea kuzalisha Wahandisi wasio na uwezo kwenye utendaji kazi.
Haiwezekani mwanafunzi anamaliza chuo kichwani ni mweupe yani ukimpa kazi za field anazidiwa na fundi mchundo ambaye hajaenda shule kabisa.
Ushauri wangu,
1.Mwaka wa kwanza na wa pili mwanafunzi asome theory tu.
2.Mwaka wa tatu vijana wajifunze kazi za usanifu(Design Works)
3.Mwaka wa nne vijana wakae site mwaka mzima wakifanya kazi kwa vitendo na kuandaa project za mwisho
Mfumo huu utazalisha wahandisi wenye uzoefu tofauti na sasa kijana anamaliza chuo hawezi kufanya kazi kwa vitendo.
Una point nzuri Ila umeteleza kwa kusema fundi mchundo hajaenda shule. Fundi mchundo ni yule mwenye qualifications ya FTC I mean FTC holder au ordinary Diploma holder
 
Hilo tatizo sio la Jalalani tu kwakweli

Elimu ya Tanzania imejikita zaidi katika Nadharia kuliko Vitendo.

Ndio maana tumeanza kuzalisha Makandarasi kwa miongo mingi tangu baada ya Uhuru wa Taifa hili lakini mpaka Leo hii serikali iliyowasomesha hao Wakandarasi inaona bora kuwaajiri wafungwa wa huko China wanaokuja kutumikia vifungo vyao vya mwisho huku kuliko kuwaajiri Wabongo.

Hebu nipe kampuni moja tu ya Wabongo pekee inayoweza kushikilia tenda ya kujenga Daraja kubwa kama la kigamboni au Flyovers au jengo kama la Ngorongoro Arusha na kulimaliza.

Hili tatizo lipo hata SUA, ambapo wanasomea utaalamu wa kilimo kwa miaka na miaka lakini mpaka leo tunaagiza mbegu kutoka Israel, South Africa, Holland n.k

Hata Mbolea za viwandani eti tunakuja kutengenezewa pale Minjingu na Kalasinga.

Madaktari nao ni kuagiza Madawa kutoka India, UK, na hata Kenya achilia mbali vifaa vya gharama za kupimia.

Hata katika Kiswahili chetu wakija wageni hapa AFRICA basi utakuta Trainers wao wakubwa ni Wakenya.

Hata Kwenye michezo hatuwaamini Makocha wetu badala yake tunamwamini Shindikana kutoka Nigeria.

Tasnia ambayo inafanya vizuri Tanzania naona ni SHERIA peke yake kwa kiasi.

WABILLAH TAWFIQ
Hadi FISIEM itoke ndo mabadiliko yatatokea..
Kwanza ni hivi:
Serikali ya fisiem aka mafia haijawekeza kwa vyovyote katika vyuo vikuu. Hakuna karakana mpya, hakuna kumbi za mihadhara, hakuna vifaa vipya wala mitaala mipya iliyotengenezwa. Vilivyopo ni vya zamani sana tena vingine vya miaka ya 70/80s ambapo wanafunzi walikuwa wachache. Kikubwa zaidi, wakufunzi na wahadhiri ni watu waliokata tamaa kabisa, hawana motisha pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu sana.

Matokeo yake yamekuwa na athari kubwa sana.
Kijana anahitimu chuo kikuu akiwa mweupe, mtupu kabisa. Hata saa nyingine katika nadharia nako hamna kitu kwani uelewa katika nadharia hutegemea kiwango cha mafunzo kwa vitendo. Mhitimu wa chuo kama huyo, bila shaka hawezi kuwa na umahiri katika jambo lolote, hawezi kujiamini kwa lolote kwa sababu na yeye akijiangalia huwa anagundua kuna vitu vingi havifaham. Vilifundishwa kwa nadharia kwa hiyo hana uelewa wa moja kwa moja.

Mhitimu kama huyu hawezi kuwa na msaada kwa taifa, ukiondoa tu kwamba anaweza kuganga njaa hapa na pale ili mradi siku ziende.

Kingine ni kukosa dira kwa maccm, yapo tu kama madudu yanayokula mbao.. hayana mipango ya siku za usoni. Kuwekeza katika elimu na katika mnyororo wa thamani ya elimu inalipa sana. Kutokana na elimu mbofu, miradi mikubwa hufanywa na wageni, kutokana na kuwa serikali haiamini kabisa kama watu wake wanaweza kufanya kazi kwa ustadi stahiki kwani inaelewa vema kuwa wahitimu wa ndani hawakupikwa ipasavyo wakiwa vyuoni, hivyo wanaweza kuharibu..

Niishie hapo kwa leo, ila tumefika hapa si kwa bahati mbaya.. ni fisiem..
 
The whole Tanzania Education System needs overhaul..ila watu wamepiga kelele wee humu..seems like kila mtu anamnyooshea kidole mwenzie afanye.in the end hakuna kinachofanyika
 
Hilo tatizo sio la Jalalani tu kwakweli

Elimu ya Tanzania imejikita zaidi katika Nadharia kuliko Vitendo.

Ndio maana tumeanza kuzalisha Makandarasi kwa miongo mingi tangu baada ya Uhuru wa Taifa hili lakini mpaka Leo hii serikali iliyowasomesha hao Wakandarasi inaona bora kuwaajiri wafungwa wa huko China wanaokuja kutumikia vifungo vyao vya mwisho huku kuliko kuwaajiri Wabongo.

Hebu nipe kampuni moja tu ya Wabongo pekee inayoweza kushikilia tenda ya kujenga Daraja kubwa kama la kigamboni au Flyovers au jengo kama la Ngorongoro Arusha na kulimaliza.

Hili tatizo lipo hata SUA, ambapo wanasomea utaalamu wa kilimo kwa miaka na miaka lakini mpaka leo tunaagiza mbegu kutoka Israel, South Africa, Holland n.k

Hata Mbolea za viwandani eti tunakuja kutengenezewa pale Minjingu na Kalasinga.

Madaktari nao ni kuagiza Madawa kutoka India, UK, na hata Kenya achilia mbali vifaa vya gharama za kupimia.

Hata katika Kiswahili chetu wakija wageni hapa AFRICA basi utakuta Trainers wao wakubwa ni Wakenya.

Hata Kwenye michezo hatuwaamini Makocha wetu badala yake tunamwamini Shindikana kutoka Nigeria.

Tasnia ambayo inafanya vizuri Tanzania naona ni SHERIA peke yake kwa kiasi.

WABILLAH TAWFIQ
Naomba huuu Uzi umfikie JPM! Anaweza kutusaidia
 
Kwenye uhandisi kila kitu kinafanywa na computer. Unafeed parameter nini unataka, computer inakupa jibu. Mambo yooote animation and transition, priority, cost, n.k. sasa kama mainjinia wenzangu bado wanatumia drawing board niliyojifunzia 1996 first year!!! Nawapa pole!
 
The whole Tanzania Education System needs overhaul..ila watu wamepiga kelele wee humu..seems like kila mtu anamnyooshea kidole mwenzie afanye.in the end hakuna kinachofanyika

Fisiem wako tayari kulipa billion 50 kununua wabunge wa upinzani na kurudia uchaguzi. Lakini hawawezi kutoa billion 40 kurekebisha mfumo wa elimu. Upgrading ya elimu inahitaji maboresho katika raslimali watu, miundombinu na mifumo mingine. Kutenga hata bilion 40 kwa mwaka na kwa miaka 5 mfululizo ili kuongeza tija katika reforms hakuna aliyeko tayari kwa sababu tu haoni hilo likichangia upatikanaji wa kura..

Tuna shida aisee.. hadi sielewi viongozi wa tz vichwani mwao kuna kiny.esi au ubongo wa kawaida..
 
I agree mkuu,Fisiemi ni janga kwa taifa letu,halafu hata humu kuna wanaokipigia chama debe..hivi hawa ni watanzania kweli???...sijui wengine mnaonaje ila mie naona kilimo,biashara,teknolojia,vikiwa priority vitaleta matokeo mazuri....tuendelee kuwapigia kelele tusinyamaze sababu wako passive,tupige kelele siku moja wataamka...lol
 
Hilo tatizo sio la Jalalani tu kwakweli

Elimu ya Tanzania imejikita zaidi katika Nadharia kuliko Vitendo.

Ndio maana tumeanza kuzalisha Makandarasi kwa miongo mingi tangu baada ya Uhuru wa Taifa hili lakini mpaka Leo hii serikali iliyowasomesha hao Wakandarasi inaona bora kuwaajiri wafungwa wa huko China wanaokuja kutumikia vifungo vyao vya mwisho huku kuliko kuwaajiri Wabongo.

Hebu nipe kampuni moja tu ya Wabongo pekee inayoweza kushikilia tenda ya kujenga Daraja kubwa kama la kigamboni au Flyovers au jengo kama la Ngorongoro Arusha na kulimaliza.

Hili tatizo lipo hata SUA, ambapo wanasomea utaalamu wa kilimo kwa miaka na miaka lakini mpaka leo tunaagiza mbegu kutoka Israel, South Africa, Holland n.k

Hata Mbolea za viwandani eti tunakuja kutengenezewa pale Minjingu na Kalasinga.

Madaktari nao ni kuagiza Madawa kutoka India, UK, na hata Kenya achilia mbali vifaa vya gharama za kupimia.

Hata katika Kiswahili chetu wakija wageni hapa AFRICA basi utakuta Trainers wao wakubwa ni Wakenya.

Hata Kwenye michezo hatuwaamini Makocha wetu badala yake tunamwamini Shindikana kutoka Nigeria.

Tasnia ambayo inafanya vizuri Tanzania naona ni SHERIA peke yake kwa kiasi.

WABILLAH TAWFIQ
Hata sheria nako ni upupu tu. Wanaweza kesi za kuku na mikataba ya kupangisha chumba ama kuzoa takataka mitaani.

Mikataba ya kimataifa wanakodoa mijicho tu,
Kesi za kimataifa hawajawahi shinda hata moja.
Kesi za maana lazima uwapatie wazungu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom