tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,796
- 18,217
Tunapojadili kuhusu kushuka kwa elimu yetu na kupungua kwa ubora wa wahitimu tusisahau kuangazia vinu vinavyozalisha wasomi hao. Juzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) tukabahatika kubadilishana mawazo ya hapa na pale kuhusu elimu inayotolewa chuoni siku hizi.
Moja ya sababu aliyonieleza inayopelekea kushuka kiwango cha elimu yetu ni wahadhili vilaza ambao huzalisha wasomi vilaza. Kwa kusisitiza hili jambo, ilinilazimu kufanya maarifa ya ziada ili kujiridhisha na maelezo yake. Ndipo nilipobahatika kupata paper iliyowahi kutungwa kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa pili katika Idara ya Sayansi ya Chakula na Tekinolojia kama inavyoonekana hapo chini.
Nilipoona paper hiyo nilishikwa na butwaa. Nilidhani huenda ilitungwa kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na sio wa mwaka wa pili. Kwa mitihani ya kipuuzi kama hii tutarajie kuzalisha wasomi wa aina gani? Nilichogundua ni kuwa wahadhiri wengi wana uwezo mdogo sana. Ndio maana wanatunga mitihani hafifu kwa sababu hawana uwezo wa kutunga mitihani “akili kubwa”.
TUJADILIANE
Ni nani alaumiwa hasa kwa uuaji huu wa elimu ya taifa? Je ni serikali, wahadhiri, wanafunzi, sayansi na teknolojia, wazazi au jamii nzima ya watanzania?
Serikali ilaumiwe?
Kwa mujibu wa utafiti (usio rasmi) uliofanyika hivi karibuni, serikali ina mkono wake katika kudorora kwa elimu ya nchi hii kwa kuingiza siasa kwenye elimu, kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.
Kivipi? Ili kujijenga kisiasa serikali iliamua kwa makusudi kabisa kurahisisha elimu yetu kwa maana ya kupunguza viwango vya ufaulu (au kutanua goli) ili wanafunzi wengi zaidi wapate nafasi za kuingia sekondari. Mitihani ilirahisishwa mno kwa lengo la kuwafanya wanafunzi wafaulu kwa wingi ili kujaza shule za kata (sema makaburi ya kuzikia elimu) zilizoanzishwa kisiasa na serikali.
Lengo hasa lilikuwa ni kujaza shule za sekondari zilizokuwa zimefunguliwa kwenye kata, hata kama hazina walimu. Ndipo wakaibuka wanafunzi wanaofaulu kwenda sekondari ilhali hawajui kusoma na kuandika. Msumari wa kwanza wa sanduku la kuzikia elimu yetu uligongewa hapa.
Wanafunzi vilaza wakafaulu kwenda sekondari na huko sekondari pia mitihani ikarahisishwa ili wanafunzi wengi zaidi wafaulu kwenda vyuo vikuu. Matokeo yake, wanafunzi vilaza wakaingia vyuo vikuu.
Sababu nyingine inayopelekea serikali kulaumiwa katika hii kadhia ni uzembe wake wa kuwahudumia wanafunzi kwa maana ya kuwapa mahitaji yao ya msingi (boom) kwa wakati hivyo kupelekea wanafunzi hao kuishi katika mazingira ya njaa na kukata tamaa.
Na kwa sababu hiyo, wahadhiri wao huwaonea huruma na kuwatungia mitihani rahisi kwa kuwa hawasomi vizuri kwa sababu ya njaa kali waliyo nayo.
Baadhi ya wahadhiri wanalinda ajira zao au nao ni vilaza?
Ili kulinda ajira zao, wahadhiri nao wakaamua kutunga mitihani rahisi ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa (discontinue) kuendelea na masomo. Jambo hili tunaweza kulitazama kwa kutumia dhana mbili: Mosi, wahadhiri huamua kutunga mitihani rahisi kwa sababu ya kulinda ajira zao.
Kwamba kama wakiamua kutunga mitihani migumu, na kwa kuwa wanafunzi ni vilaza, wanaweza kufeli darasa zima hivyo mhadhiri kukosa kazi ya kufanya. Kwa hiyo, ili kuhalalisha uwepo wake, inambidi mhadhiri atunge mitihani rahisi kuwawezesha wanafunzi wengi kufaulu.
Dhana ya pili ni kwamba wahadhiri wengi inawezekana kabisa wakawa vilaza, hasa ukizingatia namna wanavyopatikana, hivyo hutunga mitihani rahisi kulingana na uwezo wao mdogo.
Sayansi na teknolojia imechangia?
Kufuatia kukua kwa sayansi na teknolojia asilimia kubwa ya wanafunzi wanamiliki na kutumia vifaa vya intanet (kompiuta, simu, laptops, ipads, nk), hivyo hutumia muda mwingi kuchat na kutafuta wapenzi kwenye mitandao badala ya kujikita kwenye masomo.
NINI KIFANYIKE?
Serikali ichukue maamuzi magumu ya kufufua elimu kuanzia ngazi ya chekechea hadi chuo kikuu. Utaratibu wa kupata wahadhiri uangaliwe upya. Aidha, serikali ikaze uzi kwenye mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya kati ili kuwachuja vizuri wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu.
Tusiangalie zaidi takwimu za kisiasa. Ule utunzi wa mitihani migumu kama ilivyokuwa zamani urejewe. Hata ikibidi wanafunzi 100 ndio wafaulu kwenda chuo kikuu na iwe hivyo. Kusiwepo na uchakachuaji wa matokeo ili kuongeza kiwango cha ufaulu kisiasa.
MJADALA UMEFUNGULIWA….
Tujadiliane kwa ufasaha kuhusu hili tatizo la ukilaza vyuoni mpaka tupate jibu. Shambulieni hoja badala ya kumshambulia mtoa mada. Hata kama kuna mtu ataona hii hoja inamgusa moja kwa moja, awe mvumilivu…asitukane au kuchangia kwa jazba.
Sote tunajenga nyumba moja, tusigombee fito kamwe. Mods naomba mnilinde maana nina hakika kuna watu wanaoniona mbaya kwa kuwa wanadhani kitumbua chao nimekitia mchanga. Aidha kuna wanaopenda mteremko ambao hawependi kuona wanakaziwa kwa namna yoyote ile.
Nawasilisha.