Wahadhiri udom waendelea kulalama na maisha ya kunyanyaswa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahadhiri udom waendelea kulalama na maisha ya kunyanyaswa.....

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by only83, Dec 18, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...Habari ambazo ni za uhakika nilizozipata juzi ijumaa ni kuwa wahadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma wanaendelea kulalama juu ya maisha magumu na kunyanyaswa na DVC PFA Prof.Shabaan Mlacha...Mteule huyu wa raisi ameendelea kuwatesa na kutowatendea haki wafanyakazi wa chuo kile hasa wale upande wa Taaluma.....Na kwa takribani miezi sita tayari amekwisha watimua karibu wahadhiri 6 tena wengi wao bila hata kufata utaratibu wa sheria za kazi.Na uongozi wa chuo hiki umeendelea kutoa vitisho kuwa kama mnataka yawakute ya wenzenu wa Ustawi wa jamii gomeni muone.Katika kikao chao walichofanya siku ya Alhamisi inasemekana baadhi ya wahadhiri waliongea kwa uchungu na kwa hisia kali juu ya manyanyaso hayo,na wengine kuapa kuwa ni bora sasa kufukuzwa kuliko kuendelea kuona hali hii ikiendelea....nje ya tabia ya kufukuza ambayo sasa imekuwa kama desturi ya vyuo vya umma,madai mengine ya msingi kwa hawa wahadhiri ni kukaa muda mrefu bila promotion,na hata wale waliopata promotion bado mishahara yao haijabadilika..na la pili ni lile ni juu ya tofauti ya mishahara kati ya UDOM na vyuo vingine vya umma,ambalo lilipigiwa kelele hata kwenye mgomo wa kwanza ambao Waziri Pinda alikuja kusuluhisha..baya zaidi wakati wa mgomo wa kwanza Prof Mlacha ndio alikuwa anamaliza mkataba wake wa kwanza,wakati wahadhiri na wanafunzi wapo kwenye mgomo wa kumtoa huyu mungu mtu Prof Mlacha huku nyuma ikulu ilikuwa inasaini nae mkataba wa miaka mingine minne..kwangu mimi hii ni dharau kubwa kwa hawa wahadhiri...

  Maadhimio:
  Taarifa nilizozipata ni kuwa wahadhiri hao watachukua hatua zifuatazo ili kurudisha heshima iliyopotea kwa muda hapa chuoni;

  1. Wamewapa menejimenti mpaka tarehe 28/01/2012 kujua hatma ya promotion na malimbilizo ya mishahara yao,ambapo inaonekana kuna kurushiana mpira kati ya Hazina,UDOM na wizara kwa upande mwingine..
  2. Kutoa tamko kwa vyombo vya habari ili watanzania na umma wa dunia ujue maovu na unyanyasaji unaofanyika pale UDOM kwa muda mrefu sasa...
  3. Kutangaza mgogoro na uongozi wa chuo wa milele mpaka hapo watakapofanya maamuzi ya kuwatimua viongozi wakubwa hasa DVC PFA...
  4. Kuingia kwenye mgomo usio na kikomo wakati wa mitihani ya mwisho wa semister ili kuwaonyesha wanafunzi na watawala namna ambavyo hawatendewi haki....
  5. Kuwahasa watanzania kuwa UDOM sio mahala salama na pazuri pa kufanya kazi kwasasa...na hata wale wenye mawazo ya kutafuta kazi UDOM wajue na wawe wamejiandaa kuingia JEHANAMU ya mateso na taabu...
  Nawasilisha!!!

  Source:mwanachama wa UDOMASA...
   
 2. M

  Mzalendoo Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tanzania bila migomo haiendi,yaan wanasubir muandamane kwanza ndo waje kuwaskiza,wamelewa madaraka.
   
 3. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Wakigoma tunatimua na kuajiri wengine.
   
 4. nyambari

  nyambari JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 324
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  ha ha mzee umekwisha kabisaaaaaaaaa
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  huyo jamaa hakomi,kama kutukanwa humu jf anatukanwa sana lakni haachi kuandka pumba.
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  umekwisha wewe!
   
 7. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Je tutegemee graduate bora????
   
 8. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Umeona senetor ee! Hili sijui ni bwabwa? Halipo kwenye u great thinker kabsaaaa,ukili2kana lenyewe ndo linafurahi,
   
 9. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sasa kwa hali hiyo 2nategemea graduate wa udom awe na ujuz kweli mbal na kutokwenda field bado na darasan shalo,mana kwa hal hiyo walim hawafundish kwa moyo,mitihan na assgnmnt zinakuwa below standard,graduates wakibaguliwa huku kwenye soko la ajira maneno yanakuwa meng,
   
 10. N

  Nyadunga Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Tutalalamika sana.......wa Tanganyika lakini hali itaendelea.............kumbuka....maneno haya.....tutawasha mwenge tuueweke juu ya mlima Kilimanjaro uangaze na kumulika..................UDOM ni kama jeshini.lazima umheshimu kamanda mkuu hata kama ana mabo ya kipuuzi...taa ya wasomi ilizimwa na wafanya siasa kitambo tu..........sasa imebaki kusema yes mzee yess mzee.Watafukuzwa sana bcoz anayehoji anambiwa huyo ni adui wa waislamu........ndo maana vitengo vyote nyeti wanawajaza....ukiuliza mhhhh...............!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mzee anaumwa ugonjwa wa kuhara na kupoteza kiasi kikubwa na uwezo wa kufikiri..hapo anapoandika hizo hoja zake,yupo kitandani....
   
 12. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Days are numbered! mlacha anasitahili gharika akiwa hai au mfu.
   
 13. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  kumbe. Nashukuru kwa kunijuza hilo ndg.
   
 14. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,759
  Likes Received: 7,044
  Trophy Points: 280
  Prof.Ludovick Kinabo Deputy
  Vice-Chancellor in charge of
  academic,Research and
  Consultancy.Prof.Shaaban Mlacha was
  appointed Deputy Vice-Chancellor in
  Charge of Planning and Finance. So anaehusika na taaluma ni kinabo not mlacha. Hebu wataje majina hao wahadhiri walofkuzwa
   
 15. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Hao wana chuki binafsi na Mlacha. Mlacha anahusikaje na kufukuza walimu? Hiyo siyo private company ambayo mtu anaweza kufukuza wafanya kazi hovyo hovyo. Kuna procedure zinafuatwa kwenye kufukuza. Waache kutuletea umbea umbea tu hapa.
   
 16. M

  Malboro Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa tunazopewa na wahusika, kale kajamaa (Mlacha) kana nguvu sana kwa sababu ni rafiki wa karibu na JK. Hata Kikula anamgwaya, Kinabo ndio kabisaaa. Tusubiri tuone mwisho wake
   
 17. MUIKOMA

  MUIKOMA Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani UDOM kigeuzwe kuwa Makao makuu ya OUT kwani kwa serikali Dodoma imeshidwa kuwa makao makuu ya nchi
   
 18. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Upande huu akiwa anacheza mlacha na upande ule anacheza mrs sawasawa, mbona malalamiko hayawezi kuisha pale UDOM.
   
 19. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Umeambiwa tatizo wa wahadhiri ni pamoja na kulipwa mishahara pungufu kulingana na vyuo vingine. Sasa toka lini DVC-Academics akahusika na mishahara? Acha uboya
   
Loading...