Wahadhiri Chuo cha Uhasibu Arusha wagoma


Belo

Belo

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2007
Messages
11,928
Likes
5,281
Points
280
Belo

Belo

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2007
11,928 5,281 280
Wahadhiri Chuo cha Uhasibu Arusha wagoma
WAHADHIRI wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wamegoma kufundisha chuoni hapo kutokana na uongozi kushindwa kuwapa nyongeza ya mishahara yao iliyotolewa na Hazina.
Mgomo huo ambao ulianza rasmi jana umesababisha kuathirika kwa shughuli za kitaaluma chuoni hapo kwani wanafunzi wameshindwa kuingia madarasani kuendelea na vipindi vya masomo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wahadhiri hao alieleza jana kuwa mgomo huo umefikiwa baada ya uongozi wa chuo kupuuza malalamiko yao ya muda mrefu kuhusu nyongeza ya mishahara.
Pamoja na Hazina kuwaongezea mishahara yao kwa asilimia 20 uongozi wa chuo hicho umekuwa ukiwalipa kwa viwango vya chini, alisema.
Alisema malalamiko mengine ni uongozi kujumuisha fedha za posho nyingine za kikazi katika mishahara yao kinyume cha utaratibu wa kawaida ambapo fedha hizo hutengwa na kulipwa kwa mtumishi huku malipo yakiainishwa wazi.
Akizungumzia madai hayo Mkuu wa Chuo hicho, Fredrick Manangwa alikanusha kuwapo kwa mgomo huo na kueleza kuwa uongozi ulikuwa kwenye mkutano na wawakilishi wa wahadhiri hao.

CHANZO NI HABARI LEO
 
mbinguni

mbinguni

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Messages
1,921
Likes
217
Points
160
mbinguni

mbinguni

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2013
1,921 217 160
Anakanusha hata kilichoandikwa na gazeti la magamba?watampeleka guantanamo
 
I

ilisha juniour

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Messages
678
Likes
35
Points
45
I

ilisha juniour

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2012
678 35 45
Wapeni chao wapge kazi
 

Forum statistics

Threads 1,239,203
Members 476,441
Posts 29,345,577