Wahabeshi 82 walimwa faini kwa kuingia bila kibali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahabeshi 82 walimwa faini kwa kuingia bila kibali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 6, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro, imewahukumu Raia 82 wa Ethiopia kwenda jela miaka miwili kila mmoja , ama kulipa faini ya Sh 100,000 kila mmoja baada ya kukiri makosa yao ya kuingia nchini bila kibali na kufuata sheria za Serikali ya Tanzania .

  Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate , baada ya watuhumiwa kukiri makosa ya kuingia nchini bila kufuata sheria za Uhamiaji pia kutokuwa na vibali halali vinavyowapa ruhusa ya kupita hapa nchini.

  Akisoma hukumu hiyo , Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo alisema, pamoja na kusikiliza utetezi wao , amefikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kifungo cha miaka miwili kila mmoja ama kulipa faini ya fedha ya Kitanzania Sh 100,000 kila mmoja .

  Mwendesha Mashitaka wa Idara ya Uhamiaji mkoani Morogoro, Kalunga Juma, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa raia hao walikamatwa Aprili 27, mwaka huu saa 3 asubuhi kwenye msitu wa Kijiji cha Mtumbatu , Tarafa ya Gairo , wilayani Kilosa, mkoani hapa.

  Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka huyo wa Idara hiyo, raia hao walipohojiwa na maofisa wa Idara yake na wa Polisi walidai walitokea nchini mwao kupitia Kenya na kuingia Tanzania wakiwa na lengo la kuelekea nchini Malawi.

  Alidai Mwendesha Mashitaka huyo wa Idara ya Uhamiaji Mahakamani hapo, kuwa raia hao walipokamatwa walishindwa kuthibitisha uhalali wao wa kuingia nchini kufuatia kutokuwa na nyaraka wala hati za kusafiria , ambapo walikiri mahakamani kuwa hawakuwa na nyaraka hizo.

  Wahabeshi hao mara baada ya kukamatwa Aprili 27, mwaka huu walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Aprili 29, mwaka huu ambapo walishindwa kusomewa shitaka lao kutokana na kukosekana kwa mkalimali.

  Hata hivyo Wahabeshi hao walifikishwa kwa mara nyingine mahakamani hapo , juzi baada ya Idara ya Uhamiaji kumpata mkalimani wa kutafasiri lugha ya Kiingereza kwenda Kihabeshi.

  Wahabeshi hao walipopewa na Mahakama fursa ya kujitetea mmoja mmoja wengi wao walimuomba Hakimu awahurumie na pia kuiomba Serikali ya Tanzania iwahurumie na kuwasamehe kwa kosa hilo kwa vile wao bado wanategemewa na familia zao huko makwao.

  Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja kwa Mahakama hiyo kutoa hukumu kwa wahamiaji wa kihabeshi wanaoingia nchini kinyemela wakidai kuelekea Kusini mwa Afrika.

  Aprili mosi mwaka huu, Mahakama hiyo iliwahukumu raia 21 wa Ethiopia kwenda jela miaka miwili kila mmoja baada ya kukamatwa Machi 23, mwaka huu wakiwa nchini kinyume na sheria wakitokea nchi ya jirani ya Kenya wakielekea nchini Afrika Kusini.
   
Loading...