Wah: Wabunge na madiwani mnakumbuka wajibu wenu???

Kimboko

Member
Nov 16, 2010
56
0
Nawasalimu kwa Upendo kabisa.

Sijambo lakini naomba ujumbe huu uwafikie wah. madiwani John Mnyika na wenzake wa kata ya golani na saranga hasa hasa madiwani maana ndo vingozi walio karibu na wananchi kumfikishia mbunge husika matatizo yetu.

Tumeona barabara zote za mitaa ya wenzetu zinatengenezwa kwa kiwango cha changarawe lakini hii ya kwetu ya kutoka kimara suca kwenda golani hadi kinyerezi imesahaulika kabisa na kipindi hiki cha mvua si tunapata tena adha ya daraja bali gari zetu za abiria kukataa kupakia kwa sababu ya ubovu wa barabara yetu.

Tunaomba mtusaidie kuuliza kama ni manispaa au tanroads; ni ile ahadai ya Mh. Raisi inatekelezwa ya kutuwekea lami au tumesahaulika kabisa? na kama ahadi ya Raisi bado kuna tatizo gani la kutuwekea barabara hii iweze kupitika kipindi chote cha mwaka. Je huku hakua walipa kodi??

Tunaomba mtukumbuke kwenye vikao wah. madiwani maana kama la maji mmeshindwa basi tusaidieni tupate pa kupitisha ata gari za kutuletea maji.

Asanteni kwa kunielewa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom