Wagosi washerehekea kuondoka kwa mzee makamba ccm.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagosi washerehekea kuondoka kwa mzee makamba ccm....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MtazamoWangu, Apr 11, 2011.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Baadhi ya wagosi (watu watokao na wanaoishi mkoa wa tanga) wamefurahishwa sana na kitendo cha mzee makamba kutoka ndani ya ccm.
  Wengi wamefurahia suala hilo haswa kwa sababu ya ubabe,dharau,kebehi na matusi waliyokuwa wakipata kutoka kwa mzee makamba wakati wote wa uongozi wake.
  Mzee makamba analalamikiwa kutokuwa na msaada kwa watu wake na kuendekeza ubinafsi na unyanyasaji kwa wananchi wasio na uwezo, baaadhi ya yale yanayolalamikiwa ni pamoja na;
  1. Kutopeleka maendeleo hata eneo analotokea, hakuna barabara wala umeme
  2. Hakuwahi hata kuteua kiongozi katika chama kwa nafasi yake kutoka mkoa wa tanga tofauti na viongozi wengine
  3. Amekuwa akitukana watu bila kujali na kuwadharau haswa kwenye misiba,mikutano...
  4. Amelazimisha mwanae apate ubunge kwa lazima kwa kuwatisha viongozi wa chama na serikali kuhakikisha mwanae anashinda kwa njia yoyote, na hatimaye kufanikisha hilo na sasa wananchi wanalalamikia utendaji wa kijana wake huyo.
  5. Badala ya kujenga chama yey ndio amekibomoa zaidi kuliko mtu mwingine kwa kukosa umakini....

  Jana wagosi wengi walikuwa wakinywa na kula kwa furaha,huku wakisikika kusema...mungu hulipa hapahapa duniani....na kumlaani zaidi mzee makamba.

  Taarifa zinasema, kijana wake january akiwa jimboni alionekana asiye na furaha baada ya kupata taarifa na kususia kikao kilichokuwa kinaendelea....
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "wache wafu wazike wafu wenzao"
   
Loading...