Wagonjwa wote wa Corona wa Faeroe Islands wapona, hakuna kifo, Waziri Mkuu aanika siri ya mafanikio

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,794
18,512
Wagonjwa wote 187 walioambukizwa covid-19 katika kisiwa cha Faeroe kilichopo kaskazini mwa UK wamepona na hakuna aliyekufa. Faeroe ni nchi inayojitegemea sio sehemu ya UK.

Waziri mkuu wa Faero Bárður á Steig Nielsen awashukuru watu wake na kutaja siri ya ushindi huu:

1. Kufunga shughuli zisizokuwa muhimu (Lockdown)
2. Kufuata taratibu za kitabibu (respect of public health hygiene)
3. Weledi wa madaktari na manesi (high medical professionalism)
4. Kuchukua hatua mapema (timely implementation of appropriate measures)
5. Kujitenga na kukaa mbali na wengine (social distancing)
6. Kupima wagonjwa wote wenye dadili za corona (mass testing) wamepima hadi 10% ya watu wote
7. Kujitolea na uvumilivu (sacrifice and self discipline)

"Mapambano yetu makali sasa yamelipa ila tuendelee kuchukua tahadhari kubwa tusijerudi kwenye maambukizi"-Prime Minister.
1589646832768.png

1589646853525.png
 
Ina maana ma-doctor wa huko Faeroe islamd ni bora kuliko wa USA, KK, Italy na Spain au nao watumia Tanzanian style?
 
Waongo tu,

Corona unaugua unapona, then unaugua tena

Lakini huoneshi dalili zozote

Hukohoi, mafua hakuna, unaishi kama kawaida

Kwa upande mwingine unaweza kusema, huu ugonjwa ni propaganda za huko juu kutupoteza kiuchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi nnchi za dunia ya3 shida tuu, janja janja nyingi eti ohoo amana hosp. wamebakia wagonjwa 13 tuu Na wiki ijayo watapona woote, wakati kiuhalisia kila siku wagonjwa250 wana ‘perish’ na kufukiwa kama inzi tuu!
 
https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjACegQIDhAG&usg=AOvVaw2DyaISK7nJs35uZuXOGBE5

Population ya kisiwa hiki ni 49K. Umeelewa, yaani ni kijiji kidogo huku kwetu, so lockdown is 100% possible
Hakuna mahali ambapo lockdown sio possible, hata Marekani wamelockdown wakati ni nchi kubwa mara 20 ya Tanzania. Kuna aina nyingi za lockdown sio lazima kufanya total lockdown.

Kuna geographical lock down: unazuia tu movement za watu ila mambo mengine yanaendelea kama kawaida

Kuna activity lockdown; unazuia mambo flanflan yasiyo ya lazima kama vilabu vya pombe, mikutano ya siasa, dini, michezo, etc
 
hiko kisiwa cha Faeroe mwaka 2018 population ilikua watu elfu 48 tu. Wakati population ya Buza mwaka 2012 ilikua watu elfu 55.

Wasistutishe hao majamaa.
 
Back
Top Bottom