Wagonjwa wenye VVU ambao waendi kuchukua dawa Kliniki kufuatwa nyumba kwa nyumba

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Seleman Msumi amesema halmashauri imeunda kamati maalum kwa ajili ya kuwafuatilia wagonjwa wenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) ambao wameacha kutumia dawa za kufumbaza virusi hivyo.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani amefafanua kuwa, Serikali inatoa dawa za kufubaza virusi hivyo bila gharama yoyote ili ziwasaidie wagonjwa lakini cha kushangaza baadhi yao hawahudhurii kliniki hali inayosababisha afya zao kudhorota.

"Halmashauri tumeundatimu maalum ambayo ina wataalam wa afya na timu hii itashirikiana na wadau kutoka asasi za kiraia zinazojihusisha na sekta ya afya kwa ajili ya kuwatembelea wagonjwa nyumba kwa nyumba kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuhudhuria kliniki na kutumia dawa, amesema.

Mkurugenzi amebainisha wagonjwa wengine watakofuatiliwa na timu hiyo ni pamoja na wagonjwa wa kisukari na wenye shinikizo la damu ambao wamepangiwa kliniki lakini wanahudhuria kwa kusuasua na wengine wameachaa kabisa kutumia dawa bila sababu za msingi.


Source: SwahiliTimes
 
Navuta Picha Haikuji,Ndio jamaa wamepiga hodi home...Mtu amekaa na familia yake hawajui kinachoendelea.
 
Hilo biti wadau lazima waende. Likitokea tu Cruza mtaani watu watasema nani tena huyo kafuatwa?
 
Kuna dokta mmj wa masuala ya wagonjwa wa akili,alikuwa anawatimbia wagonjwa wake majumbani,
Alikuwepo pale muhimbili
Wenye matatizo ya akili walikuwa wanamjua vzr,wakinuona wanakimbia

Ova
 
Back
Top Bottom