Wagonjwa waendelea kumiminika Mloganzila

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1549893468436.png

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili, tawi la Mloganzila, imeendelea na ongezeko la asilimia 17.8 la wagonjwa wa nje wanaopata matibabu licha ya kuwapo na changamoto mbalimbali

Katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka, wamehudumia wagonjwa 20,173 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita walipohudumia wagonjwa 17,116. Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk. Julieth Magandi, aliyaeleza hayo juzi katika kikao cha bodi ya uongozi wa MNH kujadili mafanikio na changamoto za tawi la Mloganzila katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha. Dk.

Magandi alisema upande wa wagonjwa waliolazwa kulikuwa na ongezeko la asilimia 29.6 kutoka wagonjwa 1,459 hadi 1,891, wakati upande wa huduma za upasuaji jumla ya wagonjwa 649 walifanyiwa upasuaji ukilinganisha na upasuaji wa wagonjwa 267 katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha ambalo ni ongezeko la asilimia 143 .

Kwa upande wa huduma za tiba shirikishi inayojumuisha maabara na huduma za radiolojia alisema maabara ilipokea jumla ya sampuli za vipimo mbalimbali 28,907 kwa wagonjwa waliolazwa na wa nje ukilinganisha na sampuli 16,233 katika robo ya kwanza ya mwaka .

Dk. Magandi alisema katika huduma za radiolojia zinazojumuisha vipimo vya CT Scan, MRI na X-ray kulikuwa na ongezeko la asilimia 47 na vipimo 5,221 vilipimwa katika kipindi hicho ukilinganisha na vipimo 3,541 na huduma katika maeneo yote ya hospitali zinaendelea kuimarishwa siku hadi siku. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MNH, Prof. Charles Majinge, iliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuboresha huduma za afya kwa wananchi tawi la Mloganzila

“Nafahamu kumekuwa na changamoto kadhaa katika hospitali hii ya Mloganzila, lakini nafurahi kuona kila siku menejimenti inavyotatua changamoto hizo na hivyo wananchi kuitikia wito wa kutumia huduma zinazopatikana hapa,” aliema Prof. Majinge.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru, alisema pamoja na hospitali hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali, menejimenti imejipanga kuhakikisha inatoa huduma za kibingwa na za kibobezi kama ilivyokusudiwa. Oktoba 3, mwaka 2018, serikali iliiweka Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC) Mloganzila chini ya Mamlaka ya Usimamizi na Uendeshaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hospitali ya Mloganzila ina vitanda 608 na inatoa huduma za tiba za kibingwa na kibobezi, mafunzo na utafiti na ilifunguliwa Novemba 25, mwaka 2017 na Rais John Magufuli.
 
Mjinga pekee atakae furahia ongezeko la wagonjwa sio Mloganzila pekee hata hospitali Za kawaida,chukeni hatua watu wanazidi kuugua mnafurahi baada ya kusikitika, Poor African minds.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea point sana.
Hata pale Benjamin Mkapa Hospital Dodoma wanaurahi wagonjwa wameongezeka. Same to KCMC, Bugando, Kitete, Dodoma General hospital, Muhimbili, Mount Meru, Ocean Road e. t. c
Jamani tuwekeze pia kwenye elimu ya Afya kuliko kuja kuziba paa ilahali nyumba inatitia msingi haupo.

Waendelee kutibu lakini kutaja takwimu kubwa kubwa hivi kuna tatizo kwa nguvu kazi yetu hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, aisee Hospitali nimetibiwa mi hapa mwezi ulopita huo, tena kabla ya hapo nilipelekwa kwenye kipimo kama hicho kwenye picha, we acha tu ni Mungu pekee ndiye aliyeninusuru maana nilitakiwa nisiuone mwaka huu wa 2019.
Hongera kwa kunusurika mkuu.
 
Kweli watanzania tunazidi kuwa wajinga kama siyo wapopomo maana tunafurahishwa na ongezeko la wagonjwa badala ya kusikitika na kutafuta njia mbadala wa kupunguza wagonjwa sisi tunataka wagonjwa waongezeke
 
Wako sahihi kufurahia mkuu, maana yake apo kama watu walikuwa hawatibiwi maana yake wengi walikuwa wanafia majumban kwa kukosa vipimo na matibabu sahihi. Maana sio magonjwa yote yanazuilika kwa kutoa elimu na kinga.
Kumiminika kwa wagonjwa wengi ndo kupona kwa wengi pia hope uliona meli matibabu ya wachina Ilipotia nanga daresalaam ile nyomi. Kuokoa maisha ya mtu ni kitu cha kufurahia ofcoz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjinga pekee atakae furahia ongezeko la wagonjwa sio Mloganzila pekee hata hospitali Za kawaida,chukeni hatua watu wanazidi kuugua mnafurahi baada ya kusikitika, Poor African minds.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wameongezeka kwa sababu ya kufuata huduma ambapo awali ilikuwa ngumu kupata watu wanakufa kwa magonjwa yasiyo ambukizwa kwa sababu hospitali ni chache inapojengwa hospitali watu hukimbilia kupata huduma huko ulaya kwenyewe hospitali ni nyingi na bado wagonjwa ni wengi kwa hiyo na wao ni wajinga
 
Hongera kwa kunusurika mkuu.
Mkuu we acha tu yani, ilikua tarehe 17 mwezi wa 12 siku ya jumatatu, asubuhi saa 12 navuka kwa miguu pale Ubungo mataa naelekea Mawasiliano, ghafla nikagongwa na bodaboda alikua anaelekea Ubungo Terminal, bodaboda alinigonga nikarushwa kwenye lami nikadondokea kichwa halafu kichwa kikapasuka halafu damu zinaruka na zinatoka mdomoni masikioni na puani na nikawa nimeshapoteza fahamu, bahati nzuri siku hio matrafiki walikua wengi eneo hilo wakanibeba mpaka kituoni kwao wakaniandikia fomu wakanipeleka Mwananyamala Hosipital, nikalazwa hapo mpaka saa nne na madakika ndo nikazinduka nikawa sijielewi nikaelezwa kua niligongwa na pikipiki asubuhi Ubungo mataa Trafiki wakanileta hapo Hospitali.
 
Kweli watanzania tunazidi kuwa wajinga kama siyo wapopomo maana tunafurahishwa na ongezeko la wagonjwa badala ya kusikitika na kutafuta njia mbadala wa kupunguza wagonjwa sisi tunataka wagonjwa waongezeke
Kuongezeka kwa wagonjwa hosipitalini kama hakuna magonjwa mlipuko kama kipindupindu n.k, kuna sababu tofauti;
- Uelewa wa wananchi juu ya magonjwa na
tiba.
- Wagonjwa kuwa na imani na matibabu pamoja
na huduma zinazotolewa.
- Wagonjwa wanamudu gharama za
matibabu(Bima ya afya!?)

Ukweli ni kwamba watu kutokuonekana hosipitali/vituo vya afya sio kwamba hawaumwi...wengine huwa wanatumia tiba mbadala au kwa waganga wa kienyeji.
 
Mkuu we acha tu yani, ilikua tarehe 17 mwezi wa 12 siku ya jumatatu, asubuhi saa 12 navuka kwa miguu pale Ubungo mataa naelekea Mawasiliano, ghafla nikagongwa na bodaboda alikua anaelekea Ubungo Terminal, bodaboda alinigonga nikarushwa kwenye lami nikadondokea kichwa halafu kichwa kikapasuka halafu damu zinaruka na zinatoka mdomoni masikioni na puani na nikawa nimeshapoteza fahamu, bahati nzuri siku hio matrafiki walikua wengi eneo hilo wakanibeba mpaka kituoni kwao wakaniandikia fomu wakanipeleka Mwananyamala Hosipital, nikalazwa hapo mpaka saa nne na madakika ndo nikazinduka nikawa sijielewi nikaelezwa kua niligongwa na pikipiki asubuhi Ubungo mataa Trafiki wakanileta hapo Hospitali.
Poleee Sana mkuu!!! Mungu hakika amekupa nafasi nyingine

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
 
Pole sana mkuu, kwa hiyo kupelekwa huko ni mpaka rufaa ama watu wanaenda tu.?
Mkuu we acha tu yani, ilikua tarehe 17 mwezi wa 12 siku ya jumatatu, asubuhi saa 12 navuka kwa miguu pale Ubungo mataa naelekea Mawasiliano, ghafla nikagongwa na bodaboda alikua anaelekea Ubungo Terminal, bodaboda alinigonga nikarushwa kwenye lami nikadondokea kichwa halafu kichwa kikapasuka halafu damu zinaruka na zinatoka mdomoni masikioni na puani na nikawa nimeshapoteza fahamu, bahati nzuri siku hio matrafiki walikua wengi eneo hilo wakanibeba mpaka kituoni kwao wakaniandikia fomu wakanipeleka Mwananyamala Hosipital, nikalazwa hapo mpaka saa nne na madakika ndo nikazinduka nikawa sijielewi nikaelezwa kua niligongwa na pikipiki asubuhi Ubungo mataa Trafiki wakanileta hapo Hospitali.
 
Lakini pale mwananyamala kuna vipimo vilikosekana ikabidi mida ya saa 11 jioni wanihamishie Mloganzila ndo nikaenda kulazwa pale siku tano nikaruhusiwa na kupewa ratiba za kuhudhulia pale hosipitalini kwaajili ya uchunguzi, lakini bado mpaka sasa kichwa changu hakipo sawa, nawaasa ndugu zangu wana jamii forum kuweni makini na VICHWA, hakuna kitu chenye thamani kama kichwa
Pole sana mkuu, kwa hiyo kupelekwa huko ni mpaka rufaa ama watu wanaenda tu.?
Hapana siyo mpaka rufaa kuna wengine wanaenda tu.
 
Lakini pale mwananyamala kuna vipimo vilikosekana ikabidi mida ya saa 11 jioni wanihamishie Mloganzila ndo nikaenda kulazwa pale siku tano nikaruhusiwa na kupewa ratiba za kuhudhulia pale hosipitalini kwaajili ya uchunguzi, lakini bado mpaka sasa kichwa changu hakipo sawa, nawaasa ndugu zangu wana jamii forum kuweni makini na VICHWA, hakuna kitu chenye thamani kama kichwa

Hapana siyo mpaka rufaa kuna wengine wanaenda tu.
Asante kwa ushauri mkuu, naamini na wewe ulikuwa makini na ajali yoyote ile...ila ndio hivyo umesababishwa.

Mhimu ni kumwomba Mungu atuepushe na majanga ya duniani.
 
Back
Top Bottom