Wagonjwa wa Ukimwi Wala Mavi ya Ng'ombe Swaziland | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagonjwa wa Ukimwi Wala Mavi ya Ng'ombe Swaziland

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 30, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][TABLE]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Wagonjwa wa Ukimwi Wala Mavi ya Ng'ombe Swaziland[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #e1e1e1"]
  [TD] [​IMG]
  Mfalme Mswati III wa Swaziland[/TD]
  [TD] Friday, July 29, 2011 2:42 AM
  Njaa inayolitikisa bara la Afrika hivi sasa imepelekea baadhi ya wagonjwa wa ukimwi nchini Swaziland kula kinyesi cha ng'ombe kabla ya kumeza dawa zao za kurefusha maisha.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"] Imeripotiwa kuwa wagonjwa wa ukimwi nchini Swaziland wanakula kinyesi cha ng'ombe kabla ya kumeza dawa zao za kurefusha maisha.

  Taarifa iliyotolewa na wanaharakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya HIV, ilisema kuwa njaa ndiyo inayosababisha waathirika wale kinyesi cha ng'ombe.

  Wanaharakati hao walisema kwamba kwakuwa dawa za kurefusha maisha huwa hazifanyi kazi tumbo linapokuwa tupu mtu akiwa na njaa, waathirika wanalazimika kula kinyesi cha ng'ombe baada ya kukichanganya na maji ili dawa zao ziweze kufanya kazi.

  Mmoja wa wanaharakati hao, Sipho Dlamini akiongea na shirika la habari la BBC la Uingereza alisema kwamba njaa kali inawalazimisha waathirika wa HIV/ Aids kula kinyesi cha ng'ombe ambacho kimekuwa kikichukua nafasi ya chakula kwenye sehemu zilizokumbwa na uhaba mkubwa sana wa chakula.

  Swaziland ni mojawapo ya nchi zenye waathirika wengi wa HIV duniani. Swaziland ina jumla ya watu milioni 1.2 lakini watu 230,000 ni waathirika wa gonjwa hilo sugu.

  Siku ya jumatano, mamia ya watu waliandama mjini Mbabane wakipinga hali ngumu ya uchumi inayoikabili nchi hiyo.

  Serikali ya Mfalme Mswati III ilikiri kuwa imeanza kuishiwa na pesa za kuiendesha nchi hiyo na imeomba msaada toka kwa jirani zao Afrika Kusini.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]
  Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii kali......mbona mfalme wao anaishi maisha ya kifahari?? Hawawezi kumuondoa madarakani?
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Mkuu, umesahau kwamba Rais wako anaishi maisha ya kifahari na kutembea sana wakati sehemu nyingi ktk Tz wanakula mlo mmoja na kukazia kwa chai au uji. Kwingine kuna njaa ya kufa mtu.
  Rais wako amejiweka madarakani ktk awamu hii, kikatiba wananchi wanayomamlaka ya kumwondoa. Mfalme Mswati amerithi madaraka wananchi hawawezi kumvua.
  Ipi rahisi unafikiri, kumpiga chini Rais au Mfalme?
   
 4. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  habari inasikitisha aisee...
   
 5. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  KJ wa Swaz huyo
   
Loading...