Wagonjwa wa Corona wadaiwa kuvunja geti hospitali ya Amana na kutoroka. Mwananyamala waleta vurugu wakitaka waruhusiwe

...wakuu hii tarifa ni ya kweli au tetesi naombwa nijuze wengine tunatumia free basic nimeshindwa kuupitia vizur Uzi wote ?


ni hayo tu ahsanteni
 
Muwe mnaweka picha
.
IMG_20200423_073158.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani jana usiku wagonjwa wa corona zaidi ya nusu wametoroka hospitali ya Amana. Wamevunja geti wamekimbia. So please kuweni makini huko mitaani.

Nashindwa kuwalaumu maana DM yangu imejaaa malalamiko ya ndugu za watu waliokuwa Amana wanasema wanafanywa kama wanyama. Hakuna huduma, hakuna nesi au madoctor wanaowasogelea. Yani you are on your own there. Na kama unagonjwa lingine litakuua maana hakuna huduma wanayoto.

Na vile covid-19 haina dawa so wanachukulia hiyo kama sababu ya kutowasaidia wagonjwa na dawa za kupunguza makali ya dalili za covid-19 kama dawa za kifua, au kupunguza homa au dawa za kichwa. Watu wanazidiwa wanashindwa kuhema ila hawapewi oxgen wala hawapelekwi ICU wanajifia wodini.

@ummymwalimu I know you are trying mama. You are doing your best but please do something kuhusu treatment ya wagonjwa wa corona kwenye mahospitali la sivyo watu wataogopa kuja hospitali watafia nyumbani kama huduma ndo hivyo na Matokeo yake yatakuwa maambukizi kuzidi.

Kaka wa shemeji yangu alikuwa Amana toka majuzi kisukari kimepanda hakuna treatment anayopewa anaambiwa asubiri majibu ya covid-19. Kwanini asipate huduma ya kisukari wakati wakisubiri majibu? Majibu yakatoka na bado hakuna huduma ya kisukari.

Ni mmoja kati ya watu waliotoroka jana usiku, sababu yake ya kutoroka ni anataka kwenda hospitali ingine kutafuta huduma ya kisukari na kasema akifika huko hatowaambia ana covid-19 ili wamsaidie. Na sasa anakaa gesti. Now this is dangerous jamani. This can’t be happening. Yani mpaka nimesisimka. Yani wagonjwa wanaogopa kusema wana corona ili wapewe huduma ya magonjwa yao mengine. 😭😭😩

@ummymwalimu Tafadhali toa elimu kwa wahudumu wa afya wasiwaogope wagonjwa. .Hiyo ndio Kazi yao walioichagua,cha maana muwe mnawapa PPE. Kuwafungia wagonjwa wodini kama wanyama bila huduma yoyote sio kabisaaaa. Hakuna daktari wa zamu anapita kuangalia wagonjwa, wanawachungulia madirishani tu. Wanawasubiria wafe wakawazike.
 
Labda wameona huduma haziwaridhishi na wakijitibia nyumbani wanaweza kupona....hata hivyo mgonjwa anawezaje kuvunja geti?hao sidhani kama ni wagonjwa...watakua wamepona lakini bado wanaendelea kushikiliwa na kuhesabiwa kama wagonjwa.

Mgonjwa wa mafua hawezi vunja geti? AU unafikiri wagonjwa wote ni serious wapo ICU?

Wale wagonjwa wa Corona Kenya waliotoroka wawili wamekamatwa Bar wakijipongeza na kudai kuwa hawawezi kuwekwa karantine na kulipa Ksh 2000
 
Hizi ni propaganda nyingine tu zisizo na tija kwa jamii, Haiingilii akilini habari kama hii ikose hata uthibitisho wa Picha ya geti lililovunjwa...

Habari kama hizi ni za kupuuza, maana zimejaa chuki na kutia hofu watanzania..

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe acha kukurupuka unataka uambiwe habari zipi, aliye kuambia tupo salama nani? Huoni corona inavyo sambaa hata kwa mfano wa nchi zingine?
 
Back
Top Bottom