Wagonjwa njooni mtoe kero zenu mnazokutana nazo kwa Madaktari na Manesi ili wahusika wajirekebishe

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
2,115
2,808
Natumaini wazima,

Hebu wagonjwa wetu ambao ndo sababu ya kuwepo kwetu, msingekuwepo nyinyi na sisi tusingekuwepo pia.

Leo niwakaribishe mje mseme kero ambazo mnakutana nazo mnapokuja kwenye matibabu hasa kutoka kwa manesi na madaktari na ikiwezekana toeni ushauri pia.

Karibuni, tunawasikiliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa Madokta wa kike waache nyodo, waache majibu ya hovyo kama wamekunywa maji ya mtaroni, sitasahau nilisusiwa kuchomwa sindano kisa nimechelewa kwenda kumaliziwa sindano muda wenyewe ni saa tano niliambiwa muda huo ni mchana hawezi kunichoma nikahama hospital nyingine kuchoma.
 
Hawa madokta wa kike waache nyodo, waache majibu ya hovyo kama wamekunywa maji ya mtaroni, sitasahau nilisusiwa kuchomwa sindano kisa nimechelewa kwenda kumaliziwa sindano muda wenyewe ni saa tano niliambiwa muda huo ni mchana hawezi kunichoma nikahama hospital nyingine kuchoma.
Pole sana, wengi wao ni wale wenye mtazamo wa kizamani, na mara nyingi huwa hivyo pale anapogundua upo juu zaidi yake labda kwa uzuri au simu uliyobeba au gari uliyokuja nayo, so nao hupenda kuonesha umuhimu wao mbele yako. Ni ukiritimba tu, anatakiwa akusikilize,kukuelekeza na kukushauri kwa upendo. Nadhani wamesikia na watajirekebisha

ni wazimu kiwango cha lami na wanawake sisi sijui tukoje kuna hospital moja nilienda nikaambiwa niende maabara kufika namkuta mama mtu mzima nikamsalimia nikisubiri vipimo sasa bahat mbaya niliangusha kikadi cha hospital nyingine akakiokota wakat nafata majibu akanambia yan wewe badala uhudumiwe hapa karibu unaenda huko mbali kote akitaja jina la hio hospital nikashangaa amejuaje nilienda kule tena kwa kukasirika nilisikitika tu nikaondoka zangu nikawa nafikiria hivi shida n nini? Kimemuuma nini kwenda huko? Na kwa nn akasirike
 
Time will tell
Screenshot_20200111-145836.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badala ya kumuita mtu ni mgonjwa bora wamuite ni “mteja”

Kumuita mtu mgonjwa unamfanya ajisikie kuumwa hata kabla ya vipimo kuonesha ugonjwa!

Cc: Chama cha madaktari nchini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maktari wenye kuwapa wateja kauli za kukatisha tamaa,

Mfano mteja kaonda kwa daktari wa macho badala ya kumtia moyo anampa maneno ya kumkatisha tamaa mfano macho yako yanakaribia kipofu sasa maneno gani hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani daktari akifanya kazi kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu anapendezaga sana sana!

Kila hatua anayofanya ktk kumhudumia mtu anaonesha kumtanguliza Mungu.

Kabla ya kufanya operation anamsihi Mungu amuongoze ktk kuifanya vyema na kwa wepesi wa ajabu sana!

Katika kuandikia vipimo au dawa daktari anaonesha kumtegemea Mungu ambaye ndiye mfinyazi wa binadamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maktari wenye kuwapa wateja kauli za kukatisha tamaa,

Mfano mteja kaonda kwa daktari wa macho badala ya kumtia moyo anampa maneno ya kumkatisha tamaa mfano macho yako yanakaribia kipofu sasa maneno gani hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app

That is totally unprofessional!

Wakati mwingine maneno mazuri tu ya daktari yanaweza msaidia mtu kupona haraka!

Hata kama presha ilishuka au kupanda yaweza kuwa kawaida baada ya maneno mazuri toka kwa daktari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vidaktari ndio vinaanza kazi havijui kitu....
Mi kuna kamoja kalitaka nipa dawa bila nipima nikagombana nako kakakubali nikakataa maana kangeweza nipa dawa za hovyo....

Tokea siku hiyo lazima nisome na kuelewa tatizo langu kabla sijaenda andikiwa diagnosis na hata dawa lazima nizielewe kabla sijazichukua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa Madokta wa kike waache nyodo, waache majibu ya hovyo kama wamekunywa maji ya mtaroni, sitasahau nilisusiwa kuchomwa sindano kisa nimechelewa kwenda kumaliziwa sindano muda wenyewe ni saa tano niliambiwa muda huo ni mchana hawezi kunichoma nikahama hospital nyingine kuchoma.
Kibaby kinaendeleaje dear?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau daktari alimwambia mgonjwa wetu ugonjwa wako huwezi kupona bila kumpatia kwanza ushauri au kupitia kwa ndugu!

Jamaa yangu alilia usiku kucha, daktari akatimua mbio haonekani tumuhoji kwa nini kafanya hivyo direct kwa mgonjwa asiye na uvumilivu!

Ilipelekea jamaa kufa mapema maana alikata tamaa kabisa, akawa hali anasema bora ajifie mapema kabla hajatufilisi daah!
 
Ni kweli kabisa muda mwingine wafanyakazi wa afya (sio madaktari pekee) wanaweza wasitoe huduma nzuri.

Tunapaswa tujue kuwa hata wao ni wanadamu na wana moyo na hisia kama binadamu wote. Kuna maadili wanapaswa kuyafuata na ndio maana wanasoma Customer care huko mavyuoni.

Lakini, sio muda wote wanakuwa wanafanya kwa makusudi. Muda mwingine unakuta hata wao wamechoka, unakuta wanapitia stress kama wanadamu wengine, unakuta sisi tunawa-attack, n.k. Hata kama ungekuwa wewe inaweza kukutokea.

Ndio, hawapaswi kufanya hivyo kwa mujibu wa maadili yao, lakini muda mwingine tutumie ubinadamu, tusiwachukulie katika mtazamo hasi. Wengi wanafanya hivyo mara chache sana, huu ni uthibitisho kuwa nao pia wanapambana na hali yao.

Kikubwa ninawasihi tu wafanyakazi wote wa afya; wafanye kazi kwa mujibu wa maadili yao, wamtangulize Mungu, wafanye kazi kwa upendo na wajitahidi ku-control hisia zao.

Hii ipo katika ofisi nyingi, hasa za uma: halmashauri, bank, nida, n.k.
 
asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MI KERO YANGU KUBWA NI MKE WA MTU KUHUDUMIWA NA DR MVULANA AU MWANAMME KWA KILA AINA ZA MAGONJWA. KWANINI POLIS TU NA UKALI WA KIKAZ LAKIN WANAHESHIM JINSI KUPEKUA TU! SEMBUSE KUANGALIWA SEHEM ZA SIRI. KILA JINSIA ITIBIWE NA JINSIA YAKE. NDO MANA WANABAKA KILA LEO. NDO MANA MWARAB ALIMNYUKA RISAS DR MWANAUME ALIYEMZALISHA MKE WA RAFIK YAKE.
 
Hii tabia ya ma docta na kutongoza na kumlengesha mgonjwa ili akubali inaudhi mno... ...anakufanya umuone yeye ndio kila kitu...ndipo.....

Na hawa manesi..kugombania wagonjwa wa kiume waliolazwa na kuchukua waume wa wenzao ..wakome...wafanye walichosomea !

Wana takiwa kufanya vituko vyao nje ya ofisi... ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MI KERO YANGU KUBWA NI MKE WA MTU KUHUDUMIWA NA DR MVULANA AU MWANAMME KWA KILA AINA ZA MAGONJWA. KWANINI POLIS TU NA UKALI WA KIKAZ LAKIN WANAHESHIM JINSI KUPEKUA TU! SEMBUSE KUANGALIWA SEHEM ZA SIRI. KILA JINSIA ITIBIWE NA JINSIA YAKE. NDO MANA WANABAKA KILA LEO. NDO MANA MWARAB ALIMNYUKA RISAS DR MWANAUME ALIYEMZALISHA MKE WA RAFIK YAKE.
Mkuu hii ya kila jinsia itibu jinsia yake ni ngumu kdg, maana mafunzoni unajifunza kutibu wagonjwa wote, hakuna masuala ya jinsia, sema kikubwa washike ethics na wawe professional

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau daktari alimwambia mgonjwa wetu ugonjwa wako huwezi kupona bila kumpatia kwanza ushauri au kupitia kwa ndugu!

Jamaa yangu alilia usiku kucha, daktari akatimua mbio haonekani tumuhoji kwa nini kafanya hivyo direct kwa mgonjwa asiye na uvumilivu!

Ilipelekea jamaa kufa mapema maana alikata tamaa kabisa, akawa hali anasema bora ajifie mapema kabla hajatufilisi daah!
Poleni sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maktari wenye kuwapa wateja kauli za kukatisha tamaa,

Mfano mteja kaonda kwa daktari wa macho badala ya kumtia moyo anampa maneno ya kumkatisha tamaa mfano macho yako yanakaribia kipofu sasa maneno gani hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kinyume na maadili ya kazi kabisa. Anatakiwa kukupa ukweli ila sio kukuvunja moyo.
 
Back
Top Bottom