#COVID19 Wagonjwa 28 wa COVID-19 waongezeka Uganda. Watanzania wengine wanne wakutwa na maambukizi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Wizara ya Afya nchini humo imetangaza ongezeko la Wagonjwa wengine 28 na kufanya jumla ya visa vya #CoronaVirus Nchini humo kufikia 281

Wagonjwa 21 ni madereva wa malori walioingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu wakitokea Sudan Kusini huku 7 ni waliokuwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali

Kati ya madereva 21, 7 ni raia wa kigeni kutoka Tanzania (4), Congo (1), Burundi (1) na Eritrea (1). Wote wamekabidhiwa kwa Nchi zao

Aidha, Wizara hiyo pia imetangaza jumla ya Wagonjwa waliopona kuwa 69. Jumla ya sampuli zilizopimwa jana na kuleta matokeo hayo ni 2,004

Pia, soma Uganda yatangaza Visa vipya 31 vya COVID19, visa 16 ni Watanzania - JamiiForums
 
Hawatujui vizuri hawa. Ile sukari inayotokea Uganda bado haijawa kigezo cha wao kutushikia bango. Ni muda mchache tutawanyoosha na watatulia kama jirani zao Kenya.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom