Wagombea wa UVCCM mkoa wa Iringa waingia mitini kuthibitisha umri wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea wa UVCCM mkoa wa Iringa waingia mitini kuthibitisha umri wao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Aug 15, 2012.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  WAGOMBEA WA UVCCM MKOA WA IRINGA WAINGIA MITINI KUTHIBITISHA UMRI WAO , KAMANDA WAO NA KATIBU WA CCM MKOA WATOA YA MOYONI ......  [​IMG]
  Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiwaomba wajumbe wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea kutenda haki katika kupendekeza majina
  [​IMG]
  [​IMG]

  Mwanahabari na Mwanachama wa UVCCM Bi Tumain Msowoya ambaye ni mgombea nafasi ya kiti UVCCM mkoa wa Iringa


  [​IMG]

  Mwanachama Geofrey Lukuvi anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa wa Iringa


  [​IMG]

  Mwanachama Fauzia Jemedari anayegombea kiti


  [​IMG]

  Mwanachama Gaudence Kabwabwalika anayegombea baraza kuu la UVCCM mkoa


  [​IMG]

  Hawa ndio wagombea wa nafai ya UVCCM na ndio vijana wenyewe wa CCM


  SAKATA la kashfa nzito kwa wana chama wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kutuhumiwa kudanganya umri wao wa kuzaliwa limechukua sura mpya baada ya idadi kubwa ya vijana waliojaza fomu za kuomba nafasi mbali mbali katika UVCCM kukimbia kikao cha usaili kwa wagombea hao.

  Huku kamanda wa umoja wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emmanuel Mteming'ombe wakipigilia msumari kwa kutaka haki itendeke katika kuchuja majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali bila kuwepo upendeleo wowote na wale waliochakachua miaka kuwajibishwa .

  Hatua hiyo imekuja baada ya mtandao huu kuibua siri nzito ya robo tatu ya vijana hao kujaza umri wa uongo ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma miaka ya kuzaliwa ili iweze kuendena na kanuni ya UVCCM inayomtaka mgombea kuanzia miaka 14-30. Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu juzi wakati wa kikao cha mapendekezo ya majina ya wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya UVCCM mkoa wa Iringa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa chini ya mgeni rasmi kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas.

  Sehemu kubwa ya wanachama hao walioojaza fomu hizo kushindwa kutokea katika kikao hicho nyeti cha kuhakiki taarifa walizojaza katika fomu zao za kuomba nafasi mbali mbali.

  Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho ambazo zimethibitishwa na baadhi ya wanachama zinadai kuwa walioshindwa kutokea katika kikao hicho ni baadhi ya wale wanaodaiwa kufanya uchakachuaji wa umri katika zoezi la ujazaji wa fomu hizo . habari kamili tafuta gazeti la Tanzania Daima kesho ama hapa   
 2. D

  Dislike Senior Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wote wanaonekana wametumwa.
   
 3. m

  moseskwaslema Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu kijana wa lukuvi ni wa lukuvi tunayemjua au ni mwingine? mnisaidie jamani
   
Loading...