Wagombea wa Uspika na Naibu Spika kupitishwa leo na Kamati kuu ya CCM

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo inatarajia kufanya kikao chake jijini Dodoma kwa ajili ya kupitisha jina la atakayegombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania na naibu wake.

Kwa mujibu wa Katiba ya CCM kifungu cha 104(h), kamati hiyo ina jukumu la kufikiria na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama wa CCM walioomba kugombea nafasi ya Spika wa Bunge, Spika Baraza la Wawakilishi, Meya wa Halmashauri ya Jiji na Manispaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Bashiru Ali, alisema mbali na kutoa uamuzi kuhusu nafasi hizo, kikao hicho pia kitapokea taarifa ya awali ya utekelezaji wa mpango wa CCM wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

“Agenda ya pili ni kupitia majina ya wanachama waliomba nafasi ya uspika katika Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na muda umeongezwa kwa uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uwakilishi zoezi limekamilika na vikao vya awali vimefanyika.

“Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, imeshaketi na kutoa mapendekezo yatakayojadiliwa katika kikao cha sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,” alisema.

Alisema kwa upande wa Uspika wa Baraza la Wawakilishi, walikuwa wamejitokeza watano akiwamo aliyekuwa Spika Zuberi Ali Maulid.

Kwa mujibu wa Katibu Msaidizi, Mkuu wa Oganizesheni wa CCM Taifa, Solomon Itunda, katika nafasi ya Uspika wa Bunge, wanachama 10 wamejitosa akiwamo aliyekuwa Spika wa Bunge la 11, Job Ndugai na naibu wake, Dk. Tulia Ackson.

Wengine waliojitosa kwenye kinyang’anyiro hicho ni mwanachama wa CCM kutoka Mkoa wa Songwe, Stamina Mdolo, Mwanasheria wa Kujitegemea, Barua Mwakilanga, na David Meshack ambaye aliwahi kutia nia kugombea Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, baadhi ya wanachama waliochukua fomu Ofisi Ndogo ya CCM Dar es Salaam, majina yao bado hayajawekwa wazi huku upande wa Ofisi ya Zanzibar, mwanachama Abdallah Mwinyi akichukua fomu na baadaye kujitoa kugombea nafasi ya uspika.
 
Kikao cha uteuzi . Udumu mfumo wa chama kimoja, idumu ccm asante JPM hakuna kama wewe.
 
Back
Top Bottom