Wagombea wa Urais 2020 waingie JF kama verified members

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Wanajamvi,

Nawaza wagombea urais wa mwaka huu waingie humu kama verified members ili kuongea na wananchi kupigwa maswali, kujibu hoja kila inapowezekana.

Members watatakiwa kuwa na staha ya kuuliza, sio kwa sababu ya ID Fake ukakurupuka na mijitusi isiyo na msingi.

Tuwe na muda walau mara moja kwa wiki kwa wagombea hao kukaa kikaangoni kuelezea maswala tofauti tofauti na wajibu maswali ya wananchi.

Nadhani ni njia nzuri kutokana na tishio la Corona tukianza kukusanyika inakuwa sio, so tuweke mbele matumizi ya TEHAMA.

Pia ni rahisi kwa wananchi kuuliza hata maswali yenye ukakasi bila kuwa na hofu.

Tuwe tunapewa ratiba ya siku ambayo mheshimiwa atakuwa live, then tuseme naye, baada ya muda uzi husika ufungwe ili mtu asije changia jitusi.

Hili ni kama wazo, ni kama ombi kwa sababu zifuatazo:

1. Mtu anakuwa huru kuuliza akiwa na ID isiyojulikana
2. Kutokana na tishio la Corona tukianza kukusanyika kuwasikiliza tutahatarisha maisha ya wengi

Ni mawazo tu
 
Jambo zuri ila hawa wanasiasa mara nyingi huwa wagumu sana kukubali kukutana na watu wao tena wakiulizwa mambo mazito na wakizingatia Jf ni fake ID ndo wataogopa kabisa.

Hawa jamaa ukiwaandalia sehemu kama ukukmbi uwaambie waache watu wawaulize wanachotaka,lazima pazuke mengine.
 
Wazo zuri,ikishindikana wafanye mdahalo kipitia tv wakiwa pamoja, Wananchi tupate muda wa kuwauliza maswali.
 
Wanasiasa wa Bongo hawapendi maswali kutoka kwa great thinkers, wanataka waulizwe na raia wenye uelewa mdogo ili iwe rahisi kuingiza siasa

Sent from my TECNO LB8a using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana nikaweka moja ya condition wawe verified, ili tujue tunaongea na watu halisia, wasitumie ID fake kama sisi
anajiuliza kwa ID fake na kujijibu vizuri utajuaje halafu anachagua maswali matano muhimu lako analiacha ....
 
Simaanishi hivyo ila hapa ndani wapo great thinkers nimewashuhudia kabisa,hivyo mijadala hiyo ikija ni wazi GT watawapiga spana za kutosha.

Sent from my TECNO LB8a using JamiiForums mobile app
 
2020 hakuna uchaguzi wa Rais, hakuna wagombea walio tayari... tusipotezeane muda.
 
"Blaza" wazo zuri ila humu halitafua dafu.Humu kuna watu wana vyama vyao,Hata Lisu aongee vizuri unadhani( Bia yetu,USSR,MAGONJWA MTAMBUKA....) watakubali? au Magufuli atoe nondo unafikiri akina (Tindo,Erthocytes....)wataacha kumsindikizia matusi? Hapo hata iweje kila mtu atabaki na mgombea wake.



amini! amini! nawaambieni mbowe ni ccm aongozaye chadema
 
Hawawezi kuja labda waje kwa njia ya uwakilishi but muendesha page ni msaidizi wake -possible.
 
"Blaza" wazo zuri ila humu halitafua dafu.Humu kuna watu wana vyama vyao,Hata Lisu aongee vizuri unadhani( Bia yetu,USSR,MAGONJWA MTAMBUKA....) watakubali? au Magufuli atoe nondo unafikiri akina (Tindo,Erthocytes....)wataacha kumsindikizia matusi? Hapo hata iweje kila mtu atabaki na mgombea wake.



amini! amini! nawaambieni mbowe ni ccm aongozaye chadema
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom