GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,155
- 3,399
Uchaguzi wa serikali za mtaa wa msimu huu umekuja na mambo mengi sana ya kushangaza.
Baada ya vyama vya upinzani kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa, baadhi ya wagombea wao wameanza kushawishiwa kwa kupewa ahadi mbalimbali na fedha ili wapuuze maagizo hayo na wasimame katika uchaguzi huo.
Kuna baadhi wameahidiwa kugharamikiwa gharama zote za uchaguzi na wengine wameambiwa wasiwe wajinga wa kusikiliza matamko ya viongozi wao kwani matamko mengine hayana tija kwa nchi kama hili tamko la kujitoa ni lakupuuza.
Wagombea uenyekiti wa upinzani wameambiwa kwamba wasiogope kitu chochote kwani wakisimama kwenye uchaguzi hakuna mtu yoyote atakao watisha kwani watahakikishiwa usalama wa kutosha.
Mgombea mmoja kutoka CHADEMA alipoambiwa hivyo alisema kama atahakikishiwa usalama wake basi yeye yupo tayari kusimama.
Kuhusu chama kuwa mdhamini wa mgombea, wagombea hao wameambiwa kwamba hilo ni suala dogo sana watoe shaka kabisa.
Wakuu kumekucha mambo ni moto. Yajayo yanafurahisha.